.
Kile kile anachowafunza Chadema. waulize baraza kuu la Chadema watakwambia Nyanda jilili ni nini?
Ur still cryptic son.
Sihitaji baraza la CHADEMA kunieleza Nyanda Jilili ni nini, labda mimi naweza kufunza watu katika hilo baraza kuhusu siyo tu habari za Nyanda Jilili, bali pia hata habari za "Basumba Batale" na "Bafumo".
Tena unaleta mambo ya ukabila unnecessarily, which is a sign of being politically bankrupt. Wasukuma ni watu wenye akili na utulivu kushinda hizi petty tribalism antics and innuendos. Hata Shibuda kwanza kabisa alivyotaka urais alifikiri Wasukuma wataanguka kwa karata ya ukabila akawakuta hawaja respond, ndiyo maana aka withdraw bid yake. Kama Wasukuma wasingekuwa hivyo kanda ya ziwa ingekuwa nchi nyingine ile. Wangeweza kuwa na claim to statehood iliyo valid kuliko Zanzibar ambayo kwa population, area na resources haiifikii hata wilaya ya Kahama tu, but that is another ballgame.
Nimekuuliza swali rahisi tu, Shibuda ni mwanaume wa shoka kwa msingi gani? Umalaya wa kisiasa?
Mwanaume wa shoka anajua principle moja ya maisha, kwamba ukiwa ndani ya chama, hata kama hupendezwi na mambo ya chama, unayakemea mambo hayo ndani ya chama, sio kubwabwaja ovyo.
La sivyo, ukitaka kukishambulia chama publicly kwanza unajivua obligation ya "collective responsibility" kwa kujiuzulu nyadhifa zote za chama na kurudisha kadi kwa kujivua uanachama, then unaweza kubwabwaja unavyotaka kutoka nje ya chama.
Mwanaume wa shoka, akishaoa mke, hawezi kumsema mkewe vibaya pembeni. Mambo ya ndoa, pamoja na matatizo ya ndoa, yanamalizwa kwenye ndoa.
Shibuda ni kama mwanamme aliyeoa ( or more like mwanamke aliyeolewa) halafu anatangaza matatizo ya ndoa hadharani kabla ya kuyatafutia ufumbuzi ndani ya ndoa.
Mtu kama huyo unaweza kumwita mwanaume wa shoka? Habari za udhaifu wa mkeo ndani ya nyumba unaweza kuja kutuletea hapa JF kwa kumsuta kweli maalim ?