Labda ulimi uliteleza alitaka kutamka kwamba CCM ni chama cha matajiri.
BAK sidhani kama ni ulimi uliteleza,bali ni hulka ya viongozi kuwadanganya wadanganyika na ni hulka ya wadanganyika kudanganyika....Juzi waliambiwa bilioni moja ni vijisenti na bado mtu huyo huyo atawateuliwa mgombea raisi masikini hao.
OK, lets say ulimi uliteleza na badala ya chama cha matajiri ama masikini, sasa ni chama cha mafisadi,je wadanganyika wataona hilo?Ama watafuata utamaduni?
Hadi hivi sasa najaribu kuangalia ni wapi masikini wa Tanzania watapata pa kutokea, tusubiri tuone kama kuna wazalendo watakaofanya kweli ndani ya ccm ili tuweze kuondokana na utamaduni ulitufukarisha na kuendelea kuwa omba omba huku tukiwa na kila rasilimali na nguvu kazi....Inanishangaza sana kuona kuwa JK aliwaahidi wananchi maisha bora kwa mategemeo ya kutembeza bakuli....How on earth? Wadanganyika hawajiulizi maswali hayo?
Kunapokuwa na Rais anayeingizwa madarakani na iterest groups,hapo tunaona shida inakuwa kwenye utekelezaji wa issues zenye interest kwa wananchi kwasababu katiba ni ya kijamaa na mfumo wa uchumi ni wa kibepari,sasa tizama loophole hapo,watu binafsi(viongozi)na magroup yao wanadai ni usalama wa Taifa kujilimbikizia mali za Taifa na nyingine kuuza kwa wageni bila kuzingatia maslahi ya Taifa...Inashangaza sana kuona jinsi mambo yalivyo halafu kuna viongozi wanaoitwa wenye busara wame relax kabisa na kusema tuendeleze utamaduni wa umasikini,kukumbatia ufisadi na uomba omba,kabla hata hawajakubali kuwa tuko kwenye serious trouble na if we've made any progress to get out of the mess,wao wanadai tuendeleze utamaduni wa upofu na ukiziwi,tuendelee kutosikia na kutokuona kuwa tunadanganywa kuwa ccm ni chama cha masikini na kwamba mafisadi wanachota vijisenti tuu.....
Watanzania watakuwa wanajianganya kama wanadhani kuwa umasikini unaondolewa na woga na ukondoo,hilo wasahau...Haki ni haki, lakini haipatikani bure,na freedom always has a cost...Utamaduni wa ccm ni kama ule wa BAATH party ya Saddam,ni utamaduni ambao ni grupu flani ndio linachagua kiongozi, na wananch kupiga kura ni kama rubber stamping tu.....Kunatokea wababe flani tu ndani ya chama na wanasema nchi itatikisika....Viongozi hao waboronge wasiboronge,wananchi watapewa tu maelezo na mambo yataendelea,ni kama some sort of monarchy lakini ni within the circle of a certain class or group of people with the same interest etc kama ilivyo kwa ccm na baath party,badala ya family kama ilivyo kawaida ya monarchy.
Nina uhakika kama tungekuwa na viongozi makini basi tungekuwa mbali,hivyo basi naona mfumo ama utamaduni wetu ni wa kutizamwa upya,binafsi nimekataa kuendelea kudanganywa,lets wait and see kama wananchi ni kweli wamebadilika kama tunavyosikia kutoka kwa kina Mwandosya,Mwakyembe na wengineo kuwa wananchi sasa wameamka na si kama zamani.