gordon brown(GB) alikua anatetemeshwa na DAVID MILLIBAND(DM), na DM akafanya interview ambayo ikaleta mizengwe sana labour ikashidwa glasgow kwa mara ya kwanza, GB alichofanya ni kumrudisha adui wake mkubwa LORD MANDELSON (AKA PRINCE OF DARKNESS) kutoka europe. Lord M alivyofika wale blairites wote ikabidi wanyamaze na ndio GB alipoponea.
kuondoka kwa Tony Blair, ni kwa ajili ya Gordon Brown na Mshauri wake mkuu ED Balls.
GB kuna kipindi alikua anakataa kumuonyesha tonny blair budget kabla haijatoka......
Na sasa hivi GB anatetemeshwa na David Miliband, kama sio kuanguka kwa uchumi GB angekuwa kwenye hali mbaya kisiasa.
Kuondoka kwa Blair ilikuwa kwasababu ya nguvu kubwa za wananchama ambao walikuwa wamechoka na hawamtaki tena shauri ya Iraq. Kila uchaguzi walikuwa hawaendi au wanapiga Liberal makusudi. Hiyo sababu ndio ilimpa pressure kubwa Blair na wabunge wakaanza kumwambia akiendelea kubaki Labour itapoteza wabaunge wengi kwenye uchaguzi.
Brown alikuwa anafanya mambo yake kimya kimya lakini hakuna ushahidi hata mmoja kuonyesha Brown alimpinga Blair publically. Ingetokea hivyo angeambiwa ajiuzulu hapo hapo na kuomba uchaguzi na huenda asingelikuwa PM leo.
Kwa mantiki hiyo hiyo kuna wanaCCM hawataki Kikwete aendelee kwa kushindwa kupambana na mafisadi ndani ya CCM akina Chenge, Rostam, Lowassa, Mkapa na wengineo wengi. Siyo kweli kwamba Brown alifanya mambo yake kimya kimya na hiyo article niliyoiweka hapa ni uthibitisho wa hilo kwamba. Na hata kuna wakati akataka kumuondoa kama Waziri wa Fedha lakini akapingwa na wengi ndani ya chama kutokana na kazi nzuri ambayo Brown aliifanya.
Kama Brown asingemchallenge Blair aachia ngazi si ajabu hadi hii leo angekuwa madarakani lakini Waingereza walimchoka kutokana na kumuumga mkono Kichaka karibu katika kila issue pamoja na uvamizi wa Iran na opinion polls zilionyesha kwamba support yake ilikuwa ndogo sana. Na sisi Tanzania tunasikia vilio vya nchi kuyumba, nchi imetekwa na mafisadi, uchumi wetu uko mikononi mwa wageni. Hizi ni dalili tosha za kuonyesha vilio hivi ni kutokana na wananchi walio wengi kutoridhika na uongozi ulio madarakani ndiyo maana vinazidi kuongezeka kila kukicha. When you failed to deliver your promises, you should be kicked out of office. IT IS TIME FOR CHANGE, CHANGE THAT WE NEED FOR OUR BELOVED COUNTRY.
Kwani hairuhusiwi kutoa maoni yetu kama Watanzania kuhusu uongozi wa nchi yetu mpaka tuwe tunataka kumchallenge aliye madarakani? Nifurahishe baraza ili iweje!!!? Kuna sehemu chungu nzima hapa JF za kufurahisha baraza lakini huu ukumbi wa siasa si wa kufurahisha baraza. Ondoa dhana yako potofu kwamba michango yangu hapa ni ya kutaka kufurahisha Baraza.
Mifano ya mapungufu imeshazungumzwa na Watanzania wengi ndani na nje ya nchi na hata hapa JF ambao hawaridhiki na uongozi wa nchi yetu na hata Masheikh na Mapadri wameshawahi kutamka nchi inayumba. Sina haja ya kuyarudia mapungufu. Kama wewe huyajui mapungufu hiyo ni juu yako.
Ha ha ha vita mimi na Kikwete wapi na wapi!!! Mimi si mwanachama wa CCM na TANU walishanikaribisha miaka chungu nzima lakini siasa mimi siziwezi kwa sababu ya unafiki uliojaa kwenye siasa, lakini pamoja na kuwa siasa siziwezi haininyimi haki yangu kama Mtanzania kushiriki katika mjadala wowote ule kuhusu hatima ya uongozi wa nchi yetu. Na kushiriki mjadala haina maana nataka kuwa Rais au kumchallenge Kikwete lakini wale wote wanaotaka kufanya hivyo basi wasitishwe wala kuwekewa mizengwe maana katiba ya CCM inawaruhusu kama wanachama hai kugombea nafasi mbali mbali ndani ya CCM ikiwemo ili ya kuwa mgombea wa Urais toka CCM, vinginevyo katiba hiyo ibadilishwe haraka sana na kuweka kipengele kinachosema, "CCM tuna utamaduni wetu wa kumuachia Rais wa Tanzania toka chama chetu akae madarakani kwa vipindi viwili hivyo wale wote wanaotaka kumpinga baada ya Rais huyo kumaliza awamu yake moja watakiona cha moto na wanaweza kufukuzwa chamani. IT IS TIME FOR CHANGE! CHANGE THAT WE NEED FOR OUR BELOVED COUNTRY.
Happy Good Friday
Huu ni ukweli ulio wazi, CCM siyo imechokwa, bali ilishachokwa tangu kitambo, tatizo hakuna altenative, bora CCM iendelee kutawala maisha, after all ni zimwi likujualo...!.Kwa mantiki hiyo hiyo kuna wanaCCM hawataki Kikwete aendelee kwa kushindwa kupambana na mafisadi ndani ya CCM.
Na sisi Tanzania tunasikia vilio vya nchi kuyumba, nchi imetekwa na mafisadi, uchumi wetu uko mikononi mwa wageni. Hizi ni dalili tosha za kuonyesha vilio hivi ni kutokana na wananchi walio wengi kutoridhika na uongozi ulio madarakani ndiyo maana vinazidi kuongezeka kila kukicha. When you failed to deliver your promises, you should be kicked out of office. IT IS TIME FOR CHANGE, CHANGE THAT WE NEED FOR OUR BELOVED COUNTRY.
Huu ni ukweli ulio wazi, CCM siyo imechokwa, bali ilishachokwa tangu kitambo, tatizo hakuna altenative, bora CCM iendelee kutawala maisha, after all ni zimwi likujualo...!.Kwa mantiki hiyo hiyo kuna wanaCCM hawataki Kikwete aendelee kwa kushindwa kupambana na mafisadi ndani ya CCM.
Na sisi Tanzania tunasikia vilio vya nchi kuyumba, nchi imetekwa na mafisadi, uchumi wetu uko mikononi mwa wageni. Hizi ni dalili tosha za kuonyesha vilio hivi ni kutokana na wananchi walio wengi kutoridhika na uongozi ulio madarakani ndiyo maana vinazidi kuongezeka kila kukicha. When you failed to deliver your promises, you should be kicked out of office. IT IS TIME FOR CHANGE, CHANGE THAT WE NEED FOR OUR BELOVED COUNTRY.
huyu atakuwa siyo shibuda tu.kuna watu wazito nyuma yake wanautaka urais 2010 baada ya kuona uwezekano wa kumuangusha kikwete upo kama watapata upenyo ndiyo mana hawa wazee wanajitahidi kwa nguvu zote kuwavunja nguvu maanake wakiacha italeta vurugu na hata kumuharibia kikwete na kumuweka katika wakati mgumu kama upinzani wataweka mgombea mzuri.
Bubu Ataka Kusema,
Any way lengo hapa sio kubishana, ila ukweli ni huo Brown hakufanya challenge yoyote publically au kwenye interview dhidi ya Blair.
Hata hiyo ya kutaka kumwondoa kuwa waziri wa fedha uko wrong. Wafuasi wa Blair walimshauri Blair amwondoe kwenye nafasi ya kuwa waziri wa fedha, lakini dakika ya mwisho Blair aligoma. Alihofia maasi kwenye chama na akachukua uamuzi wa busara kutokufanya hivyo. Brown alikuwa hana uwezo wa kikatiba kukataa anachofanya PM.
Hapa mimi simtetei JK , lakini ni muhimu kuweka records straight. Kama wanaompinga JK CCM wako wengi basi wagombee na kumwondoa. Kuongea kwa akima Malecela hakuzuii wao kugombea. Alichotoa Malecela na wengine ni maoni yao.
Kuna kipindi wafuasi wake wa Brown ambao sio mawaziri walijaribu kuandika barua, baadhi ya wakuu wa chama wakamwambia Brown kama watu wake wanataka kumwangusha Blair, yeye asahau kuwa PM. Ikabidi Brown mwenyewe awakane na zoezi hilo likafa.
Blair alikuwa sio mjinga, alikuwa anajua kusoma nyakati. Pia alikuwa anajua historia ya kuondolewa kwa Thatcher na akajua inaweza kuja kwake pia.
Wanachofanya hapa UK kuondoa kiongozi ambaye hawamtaki whether ni kwenye serikali au chama, wale watu wa chini wanaomuunga mkono kiongozi mmoja ndio wanaanzisha maasi. Wakifikisha idadi ya kura zinazotakiwa kufanya challenge basi kazi imeisha. Uchaguzi ukiitisha na kama watu wamekuchoka, kwenye kura ya siri unapigwa nje. Hicho ndicho kilichomtokea Thatcher. Tofauti tu kwa Thatcher, aliyeomba challenge alikuwa naibu wake. Ikaishia wote wawili wakakosa na Major akapata kuwa PM kirahisi.
Mimi wakati huo nilikuwa mshabiki wa Brown na nilikuwa nasubiri afanye kitu Blair aangushwa, lakini haikutokea mpaka Blair mwenyewe alipoona anakoenda ataangushwa kwa kura. Sio kawaida UK PM kuongoza zaidi ya miaka 10.
Kina Malecela walitoa maoni ama walisema ni utamaduni?
Nadhani ingekuwa maoni kama wangesema kuwa wanapendelea kuona rais akichaguliwa kugombea kwa mara nyingine kutokana na sababu hizi ama zile na si wazee wazima kuja na kusema eti ni "Utamaduni"
Mtanzani fikiria kwa makini na si tu kusema ni maoni yao,kwasababu maoni yao hayo yana malengo,sasa la kujiuliza ni kama malengo hayo yana manufaa kwa Taifa na si tu kuana mambo kwa mazoea. Ni muhimu sana kuleta mabadiliko kwenye siasa zetu kwasababu hao wazee wametufikisha hapa tulipo kwasababu ya tamaduni hizo hizo.
Semilong,
Inaelekea kweli hujui siasa za UK au ni msomaji wa SUN na umbea wa mitaani unachukulia ndio ukweli.
Ni kweli David Millibabd alitoa speech yake ambayo watu walitafsiri kama mwanzo wa kampeni ya kuongoza chama (kumwangusha Brown). LAKINI, alipoulizwa alikataa kata kata na kusema yeye anaongelea renewal chini ya Brown.
KUSHUKA KWA POPULARITY GB NDIO SABABU YA BAADHI YA VIONGOZI KUTAKA AONDOLEWE NA AJE MILIBAND. LORD MANDELSON NDIO BLAIR RITES #1, NA AMEWANEUTRALISE BLAIR RITES WENZAKE, NIMTENDAJI WA KAZI MZURI PIA. NA SIO LORD MANDELSON TU AMERUDI HATA ALISTAIR CAMPBELL ANAMPA USHAURI NA HAWA NI MASWAIBA WAKUBWA TONY BLAIR.Semilong,
Kumrudisha Mandelson sio kwa ajili ya upinzani ndani ya Labour, ni kwasababu popularity yake ilikuwa inatelemka na Conservative kuongezeka. Kamrudisha Mandelson kama njia ya kuboresha utendaji wa serikali yake na hivyo kuzuia kuanguka kwa Labour.
ANGEMRUDISHA PALE PALE INGEKUWA NI KNEE JERK REACTION AMBAYO WANASIASA WA ULAYA WANA AVOID.Semilong,
Pia speech ya Milband na kurudi kwa Mandelson kulikuwa hakuna uhusiano. Hayo mambo mawili yalitokea wakati tofauti kabisa.
Mtu aliyempinga Brown kwenye serikali yake ni junior minister mmoja mwanamke na siku hiyo hiyo aliachishwa kazi tena akaambiwa na mtu wa TV kwamba umekuwa sacked.
Kwa UK ni wazi kama wewe ni waziri huwezi kumpinga PM wazi wazi, ukifanya hivyo inabidi uachie ngazi na kuomba uchaguzi na kama una wabunge wa kutosha kukuunga mkono basi uchaguzi unaitishwa, vinginevyo ukikosa wa kukuunga mkono unaishia kuwa backbencher na ndio sahau hurudi tena serikalini.
Kama sikosei, huyo Shibuda aligombea pia na MKapa. Jamaa anajiamini na kwenye siasa tunataka watu kama hao hata kama ni wachache lakini kuna principles wanaziamini.
Chaguzi za CCM zilivyo sio rahisi kumwondoa rais aliye madarakani. Maamuzi mengi yanafanywa na CC ambayo wajumbe wake wengi wanachaguliwa na huyo mwenyekiti wao ambaye pia ni rais. Hiyo ndio inachuja majina, wana uwezo wa kutupa majina kama walivyofanya kwa Malecela na huwezi kuwahoji.
Kama kuna nafasi ya kumwondoa JK ni kupitia upinzani, sahau hii ya CCM kumwondoa JK.
Tatizo la JF kuna watu ni vipofu na hawaoni kabisa ukweli mwingine wowote zaidi ya ule wanaouamini wao.
huyu atakuwa siyo shibuda tu.kuna watu wazito nyuma yake wanautaka urais 2010 baada ya kuona uwezekano wa kumuangusha kikwete upo kama watapata upenyo ndiyo mana hawa wazee wanajitahidi kwa nguvu zote kuwavunja nguvu maanake wakiacha italeta vurugu na hata kumuharibia kikwete na kumuweka katika wakati mgumu kama upinzani wataweka mgombea mzuri.
Mkuu Mtanzania labda utanipa elimu zaidi hapa manake ninavyojua CC ya ccm ina wajumbe 35 hivi au hawazidi 40 na wote ni vingunge wa juu kabisa wa ccm na wanapochuja majina ya wagombea basi mjumbe ambaye ni mwana CC haruhusiwi kuwapo.Kwa maana hiyo hata kama yeye Kikwete ni mwenyekiti lakini siku hiyo itabidi atoke nje.
sasa mkuu kwa nchi yetu ilipofikia hapa au niseme ccm ya sasa hii jinsi ilivyo na umaarufu wa kikwete ulivyoporomoka,mkuu huwezi kuweka guarantee kwamba kikwete atapitishwa tu hasa ukichukulia kwa mfano watokee wagombea wenye influence kubwa.ndiyo mana hawa wazee wa ccm vichwa vinawauma.mimi nadhani ingekuwa kama ni shibuda tu peke yake mwenye nia hiyo wala wasingepoteza muda wao na waandishi wa habari na kuanza kuweka mikwara mizitomizito.
Utakuwa unajidanganya ukifikiri wanasiasa wanapofanya mambo yao, lengo namba moja ni manufaa kwa taifa. Namba moja ni manufaa kwao labda mbili ndio taifa.
Ukiwa na watu kama Chenge si ajabu taifa iko namba kumi.
Maneno ya Malecela hayajabadili katiba ya CCM. Kama Shibuda anataka kugombea na atagombea tu. Lakini kweli kwa akili yako unaamini ile CC ya CCM inaweza kupita jina lingine zaidi ya JK?
Uteuzi wa mwanzo ungelikuwa unafanywa na halmashauri kuu, ningeweza japo kuamini kwamba labda inawezekana, lakini CC zaidi ya nusu ya wajumbe wanawekwa na rais/mwenyekiti, unategemea nini toka kwa watu kama hao?
Hii dunia ni muhimu mno kuelewa the reality, vinginevyo utaishia kugonga ukuta. Kwa TZ kama mnataka kumwondoa JK nafasi pekee ni kupitia upinzani na uchaguzi mkuu. Haya mambo ndani ya CCM kwa mimi naona nafasi hakuna.
Mkuu,
Hawa watu hapa chini ndio unategemea wamgeuke JK? Labda kama tunaota ndoto.
2. Msekwa - Makamu Mwenyekiti
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Edward Ngoyai Lowassa - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23.Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30 . Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31 . Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32 . Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34 . Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37 . Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe
mimi sio msomaji wa sun, MIMI NASOMA FT, hehehehe...