Shibuda ajichimbia kaburi lake

Shibuda ajichimbia kaburi lake

Mkuu Zitto mwenyewe kathibitisha hilo na kuelezea mbinu anazotumia kukataa posho. Wengine wote wanapokea tena kwa moyo uliokunjuka na mikono miwili. Anayeweza kusema against posho ndani ya CHADEMA ni Zitto tu wengine wote kimya. Regia yupo humu pamoja na Mbunge wangu Ndugu Mnyika mbona hawajatoa kauli kama hawachukui posho za vikao?[/QUOTE<font size="4">]ILE SIO POSHO NI UJIRA WA MWIHA</font>
<br />
<br /> Kumbuka kuwa Zitto anaonekana kwa vile ni waziri Kivuli wa Fedha na hiyo ndio sera ya CDM lazima aishikilie hivyo kumbuka hii ni sera ya CDM ni ya chama c ya Zitto,na c kila mbunge atoe kauli yake humu au bungeni, cha msingi SHIBUDA aliingia CDM kwa bahati mbaya hivo kama hafahamu mlango wa kutokea aoneshwe,bora tujue ya kwamba moyo na fikra za SHIBUDA ni za CCM na yeye ni CCM mwenye kadi ya CHADEMA.
 
Zaidi ya yote yanayosemwa kuhusu Mhe. Shibuda, kwa kuongezea tuu, Mhe. huyu Shibuda ni mtu asiye na shukrani kabisa katika madogo, wala hakumbuki fadhila!.

Aliposhikiliwa kwa kubambikiwa kesi ya mauaji wakati wa kampeni, alisambaza ujumbe mfupi wa sms za kuomba msaada wa fedha kwa marafiki zake na hata kwa wasio marafiki lakini wanaojuana kisiasa. Japo aliwekwa chini ya ulinzi, lakini aliwekwa ki VIP fulani akiwa na simu yake ya mkononi.

Kwenye sms hiyo, alieleza jinsi anavyoteseka mahabusu ya polisi, na kumalizia kuwa amenyanga'nywa kila kitu mpaka kadi zake za ATM, hivyo anaomba msaada kidogo wa tulaki tuwili tutatu kusaidia familia yake kwa chakula. Ujumbe huu, ulimfikia mshirika wangu wa karibu na ikatokea bahati mbaya mshirika huyu naye ujumbe ulimkuta akiwa katika hali mbaya, ndipo akaweka wazi kwa watu wake wa karibu.

Ikapitishwa harambee ya papo kwa papo, kikapatikana kiasi kuliko kilichoombwa, akapigiwa simu kuulizwa zitamfikiaje, hata bila kujibu ile simu au japo kusema asante, alimkatia jamaa sumu sikioni na mara jamaa ilipigwa simu na mtu aliyejhitambulisha katumwa na mheshimiwa kukusanya hicho chochote kitu, na mara alielekezwa zilipo akazipitia.

Yule mjumbe akarudisha ujumbe, mzigo umemeshamfikia mlengwa kwa kuutuma kwa mtu, ambaye amemfikishia rasmi mheshimiwa wetu, jamaa yangu akitegemea japo sms nyingine toka kwa mhishimiwa ya kushukuru, japo aliomba kidogo, amepewa mara dufu ya alichoomba, akitegemea jamaa ange appreciate kwa hilo lililofanyika ndani ya muda wa lisaa limoja tuu, lakini no!. Hakuna cha shukrani, wala asante!.

Hata baadaye walipokutana na Shibuda viwanja vya bunge, alianza kwa kumpongeza kwa ushindi wa ubunge, na kuulizia vipi maendeleo ya kesi, na jee kale kamzigo kalifika na kama kalisaidia kitu, jibu likawa kalifika, akitegemea basi japo kaasante kangetoka, lakini wapi!.

Jamaa alipoturudishia feedback kumbe jamaa hata shukrani hana, sisi tulisisitiza kuwa lengo letu lilikuwa ni kutenda wema tuu na kuendelea na maisha yetu na sio kusubiria shukrani.

Mtu asiyekumbuka fadhila na kushukuru kwa madogo kama Mhe. Shibuda, Chadema isitarajie hisani, fadhila wala shukrani yoyote kutoka kwake, sana sana, isubiri kuambulia matusi ya haja, mara atakaporejea nyumbani CCM baada ya ziara ya kutembelea Chadema!.

Mh. Shibuda, hivi kweli wewe unasema mbele za watu na unajidai kwamba wana-Maswa ni wako! Umesahau vijana tuliokusaidia kwa hali na mali maana ulikuwa huna uwezo wa kushinda. Kwanza Shibuda ulikuwa na doa la kumchezea mchezo mchafu JIDULA MABAMBASE ambaye alikufa mda si mrefu wakati wa kura za maoni za CCM. Sisi vijana wa Maswa tunafahamu hata waganga wako (kamati ya ufundi), ulikuwa na waganga saba, ulienda siku moja kwa mganga wako wa Malampaka na alikutabiria mambo yako kuwa hayakuwa mazuri, vijana wa Kizungu, Dodoma, Kadoto, shishiyu,Mwabayanda wote kwa sasa tunakushangaa na tunakuona huna fadhila. Wananchi wa Maswa tunataka mageuzi na mageuzi yataletwa na CHADEMA hakuna chama mbadala kwa sasa zaidi ya CDM. Kama unajidanganya unamtaji Maswa, sahau wananchi wameshakutoa maana.
Pamoja na kasoro za Shibuda Haya mengine ni majungu na fitna tu, jengeni hoja bana
 
SHIBUDA.



shibuda.jpg




GAZETI la Chama Cha Mapinduzi (CCM) lilipoandika wiki iliyopita kwamba Mbunge wa Maswa Mashariki, John Shibuda "amejilipua" lilijua linachokifanya.

Ilikuwa baada ya mbunge huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwashutumu viongozi wake kwa mafumbo, na hata kuwafananisha na Nduli Idi Amin wa Uganda.



Inashangaza Shibuda amekuwa anatumia fursa ya kuchangia bungeni kukishutumu chama chake hadharani. Kumbukumbu zinaonyesha tangu amechaguliwa kuwa mbunge wa CHADEMA mwaka jana, Shibuda ametofautiana hadharani na viongozi wake mara tatu.


Mara ya kwanza ilikuwa katika kikao cha kwanza cha Bunge, pale wenzake waliposusia hotuba ya Rais Jakaya Kikwete bungeni, na kukataa kushiriki shughuli zake hadi hapo atakapojibu hoja za msingi, ikiwamo umuhimu wa mabadiliko ya katiba.

Wabunge wa CHADEMA waliokuwa bungeni, walinyanyuka na kuondoka mara tu Rais Kikwete alipoanza kuhutubia. Wachache kwa udhuru waliotoa, hawakuingia hata bungeni. Sidhani kama Shibuda alitoa udhuru wowote, lakini hakuonekana bungeni. Jioni alionekana akisamiliana na Rais Kikwete katika hafla iliyoandaliwa na rais kwa wabunge hao, Ikulu Chamwino.


Baadaye alipopata fursa ya kuchangia bungeni, badala ya kujielekeza kwenye hoja iliyokuwa mbele yake, aliwashambulia viongozi wa CHADEMA, akisema wenzake ni wanaharakati, na kwamba yeye ndiye mwanasiasa mahiri.



Mara ya pili ilikuwa katika kikao hiki cha Bunge, alipotofautiana na wabunge wenzake katika msimamo wa kususia posho. CHADEMA kimekuwa kinasisitiza kwamba posho za vikao kwa watumishi wa umma, wakiwamo wabunge, ni matumizi mabaya ya fedha za umma; na kwamba pesa hizo zingefaa zielekezwe kwenye kuinua kipato cha watumishi wa chini.

Alipopata fursa ya kuchangia hotuba ya waziri mkuu, Shibuda aliwashutumu wenzake, akidai hata posho yenyewe wanayopewa haitoshi. Akataka Bunge liwaongezee posho hiyo hadi Sh 500,000 (laki tano).

Alidai wanaokataa posho hizo wana pesa, na kwamba wabunge maskini kama yeye wanazihitaji kwa ajili ya misiba, harusi na kadhalika. Akawaita wenzake "wabunge maslahi binafsi," na kwamba yeye ni "mbunge maslahi ya jamii."



Mara ya tatu ni wiki iliyopita, alipowashambuliwa kwa mafumbo na kuwafananisha viongozi wake na Idi Amini.

Zipo habari pia kwamba wabunge wa CHADEMA walipokuwa kwenye vikao vya ndani vya kuwekana sawa na kupanga mikakati ya kazi, mwanzoni mwa mwaka, Shibuda aliwarukia kwa maneno makali na kuwashambulia kwamba hawajui siasa, ni watoto wachanga na wanaharakati.

Wabunge walimjia juu mmoja baada ya mwingine. Mbunge mmoja kijana akamwambia Shibuda, "kama umetumwa na CCM kuvuruga chama chetu, mlango ule pale. Rudi ulikotoka."


Ndani ya chama na mbele ya umma, Shibuda amekuwa anapenda kujionyesha kama mwanasiasa mahiri, mzee wa busara, mkongwe mwenye busara za kisiasa ambazo "watoto wa CHADEMA wanapaswa kuvuna."


Amekuwa akisema kwa rafiki zake kadhaa, ndani na nje ya vyombo vya habari, kwamba CHADEMA hawamheshimu wakati yeye ni mzee, na kwa makuzi aliyopewa, uzee ni dawa.

Lakini anasahau kwamba kama suala ni uzee, CHADEMA kinao wazee wengi, na hatuwasikii wakilalamikia uongozi wa vijana walionao. Hata pale yanapotokea matatizo ya kiutendaji au ya kinidhamu, wamekuwa wakihusika kutoa ushauri na kuchukua hatua bila kelele wala lawama hadharani.

Sana sana, wazee wa CHADEMA wamekuwa wanajivuna kuwa na timu ya vijana wachapakazi wanaokipa chama sura ya matumaini na uhai usioonekana katika vyama vingi tulivyo navyo.


Mbele ya macho ya wengi, Shibuda si mwana CHADEMA. Ni mwana CCM aliyevaa u-CHADEMA kupata ubunge. Na sasa anatumia ubunge wake kufyatua makombora dhidi ya CHADEMA.


Kinachoshangaza wengi pia ni upole wa Spika wa Bunge, linapofika suala la mbunge kuacha kujadili hoja iliyo mbele ya Bunge, akaanza ama kujitetea binafsi au kushambulia viongozi wa chama chake.


Hii inaongeza tetesi kwamba Shibuda anafanya kazi aliyotumwa. Lakini sasa kwa kasi hii atawafanya hata hao "waliomtuma" waone aibu kujihusisha naye, maana haifanyi kwa akili.


Wanaofuatilia mwenendo wa Shibuda wanasema kuwa makundi mengi ya watu anaoshinda nao, anaokunywa nao, anaobadilishana nao mawazo, na wanakiri kwamba haonekani kupenda kukaa na wana CHADEMA wenzake. Sana sana anatumia muda mrefu kuwasema vibaya na kuwapiga vijembe.

Tabia yake hiyo ndiyo ilimfanya Katibu wa Wabunge wa CHADEMA, John Mnyika kumshitaki kwenye chama, katika shauri ambalo hatujajua limefika hatua gani.

Lakini ni wazi kuwa Shibuda hana moyo wa kujisuta. Hatambui kasoro zake. Anatumia muda mrefu kujisifu, jinsi alivyo jabali la kisiasa, na jinsi alivyoshinda ubunge bila kampeni kubwa.


Anachosahau ni kwamba kama si CHADEMA, asingepata ubunge. CCM walishamtupa kwenye kura za maoni. Walishamchoka.

CHADEMA walimwokota kwenye jalala. Wakamteua. Wakampatia jukwaa, baadhi yao wakamchangia pesa, wengine wakaenda kumnusuru wakati alipokamatwa na kuwekwa ndani kwa kesi ya mauaji ya kubambikiwa siku chache kabla ya kupiga kura.

Mbunge wa Maswa Magharibi, Sylvester Kasulumbayi, ambaye wana Maswa walikuwa wakimwita Yesu, alifanya kampeni katika majimbo mawili &#8211; kwake na kwa Shibuda &#8211; wakati Shibuda akiwa katika matatizo.


Wana CCM wenyewe wanasema kwamba anachokifanya CHADEMA leo ndicho alikuwa akifanya kwenye CCM, lakini kwa kuwa kilikuwa chama tawala kulikuwa na uficho. Na wanasema ndiyo maana hata alipogombea vyeo ndani ya CCM hakupita.

Mara zote alilalama kwamba anaonewa, lakini wanachama wenzake wa zamani wanasema kuwa walishamjua kwamba ni tatizo, wakaamua kumnyima fursa za kuendelea kuwasumbua ndani ya vikao.

Ni dhahiri kwamba Shibuda anakihitaji CHADEMA kuliko chama hicho kinavyomhitaji. Anaweza kujitapa kwamba liwalo na liwe, lakini hawezi kuwa na uhakika kwamba akifukuzwa na CHADEMA leo, akahamia chama kingine, ataupata ubunge.


Shibuda ameshindwa kusoma alama za nyakati, hasa katika mazingira ambamo CHADEMA kimekuwa taasisi kubwa inayotikisha chama tawala, na inayoaminiwa na wananchi.


Tambo zake kuwa anapingana na viongozi maslahi ndani ya chama chake si kweli, kwani ameonyesha jinsi asivyo tayari kuacha posho ya kikao, ambayo chama chake kimesema ikiondolewa na kuhamishiwa kwengine itaboresha maisha ya watumishi wengine wasio na masilahi manono kama ya wabunge.

Baadhi ya wana CHADEMA na waandishi wa habari walio karibu na Shibuda wanasema kwamba uadui wa Shibuda na chama chake unatokana na ukweli kwamba alipohamia kwenye chama hicho mwaka jana, alidhani angepewa pesa ya kufanyia kampeni.


Mara kadhaa aliwaendea viongozi wa CHADEMA na kuwaomba wampe pesa, lakini majibu aliyopata yalimkatisha tamaa, kwani walimwambia yeye kama mbunge aliyemaliza ngwe yake, alipata kiinua mgongo.


Wakamweleza kuwa wabunge wote wa CHADEMA hawapewi pesa na chama; sana sana wao ndio wanapaswa kuchangia chama na kusaidia wagombea wasio na chochote. Baadhi ya viongozi aliowaomba pesa nao walikuwa wanagombea majimbo, wakamweleza kuwa nao wanazihitaji pesa hizo.


Kwa chuki na hasira alizotoka nazo hapo akajiapiza "kuwashughulikia" baadhi ya hao waliomnyima pesa. Wanasema Shibuda amekuwa pia anakerwa na kauli za viongozi za kuwataka wabunge wachangie chama kama njia ya kudumisha utamaduni wao uliokifikisha chama hapo kilipo.


"Anasema kama walikifikisha hapo kwa michango yao, ilikuwa ni uamuzi wao, wasijitape wala kuwalazimisha na wapya wachangie. Hii haikubaliki, na ni kielelezo kingine cha ubinafsi wa Shibuda," anasema mwanachama mmoja kijana ambaye Shibuda amekuwa anamsimulia mikakati yake ya kuwashughulikia viongozi wake.


Baadhi ya wanachadema wanadhani kwamba Shibuda hajajua hata sera ya chama chake. Wanaamini hajui hata katiba na kanuni za chama zinasemaje; vinginevyo mambo anayofanya sasa yangepaswa kufanywa na "mgonjwa wa akili."


Kwa hakika, hapa ambapo Shibuda amejifikisha, anaweza kuwa anajichimba kaburi lake mwenyewe.
 
hadi mwaka 2015 tutakuwa tumeongeza majimbo mengi tu, shibuda anatakiwa kupgwa chini kama wale madiwani wa arusha
 
CDM wanatakiwa wamfukuze uanachama Shibuda haraka kabla hajaleta madhara kwa chama,huyo ni pandikizi la CCM kaletwa kuivuruga chama,hizo ni baadhi ya mbinu za ccm kuua upiunzani nchini.Bado wapo wengine katika vyama vinavyoonekana vina nguvu kama CDM.
 
Ndani ya CDM ukiwa mkweli unajichimbia kaburi!! Wangwe alijichimbia kaburi baada ya kuhoji ruzuku zinatumikaje. Bado kuna wasaliti wengi tu ambao wanachukua posho za vikao ilihali CDM walishakubaliana kwamba posho za vikao ni haramu. Hawa nao wanatakiwa watendewe haki yao.
 
Huyu ndiye Shibuda ambaye Nape alsema cdm wakimwondoa wanavurugika, huyu mwanasiasa aliyepotoka kimaadili aivuruge cdm. Huyu ni mbunge anayeishia kisiasa na cdm wakimtema hana pa kwenda.
 
Ndani ya CDM ukiwa mkweli unajichimbia kaburi!! Wangwe alijichimbia kaburi baada ya kuhoji ruzuku zinatumikaje. Bado kuna wasaliti wengi tu ambao wanachukua posho za vikao ilihali CDM walishakubaliana kwamba posho za vikao ni haramu. Hawa nao wanatakiwa watendewe haki yao.
Kamtetee Mtatiro anasema CDM hawana nguvu Igunga, halafu anaanza kulalamika kuwa CDM watagawa kura za CUF.....sasa kama CDM hawana nguvu watagawaje kura za chama ngunguri??
 
Kamtetee Mtatiro anasema CDM hawana nguvu Igunga, halafu anaanza kulalamika kuwa CDM watagawa kura za CUF.....sasa kama CDM hawana nguvu watagawaje kura za chama ngunguri??

Mkuu nimtetee Mtatiro kwa nini? Hilo halihitaji utetezi ni suala la upinzani kukubaliana tu kwamba nani aachiwe baada ya kupima upepo. Lakini CDM walivyo na uroho wa madaraka hata kama hawakubaliki mahala wanaenda tu kugawa kura za wapinzani na matokeo yake: CDM 5, CUF 8, CCM 10!! CCM anatangazwa mshindi kwisha habari.
 
Sasa kama ccm wamemchoka basi tuseme hawakumtuma kuivuruga chadema, bali akili yake iliyojichanganya na mavi inamwongoza vibaya. Ngoja tuwaachi uongozi wa juu wa chama waamue.
 
Ndani ya CDM ukiwa mkweli unajichimbia kaburi!! Wangwe alijichimbia kaburi baada ya kuhoji ruzuku zinatumikaje. Bado kuna wasaliti wengi tu ambao wanachukua posho za vikao ilihali CDM walishakubaliana kwamba posho za vikao ni haramu. Hawa nao wanatakiwa watendewe haki yao.

mkuu wangwe ana ndugu zake na familia bado inaishi, sio ustaarabu kama familia imekaa kimya wewe kuongea mambo kama haya
unakua uitendei haki, kama kweli unaongea kwa utu, basi wapi ushahidi hiyo familia ya kwamba ndugu yao aliuawa kwa sababu ya kuoji posho,
ama la huku ni kukosa maadili na kuitukana familia yake, sio hivyo tu unawanyima uhuru wa wao kusonga mbele kwa kusahau yaliyopita,
wewe na mimi hatuna haki ya kuisemea familia ya wangwe, kwenye majukwaa bila ruhusa yao.

tujifunze kuheshimu familia za wafiwa, maneno mazito kama haya sio ya kuweka kwenye majukwaa tu kwa sababu una internet, futa kauli yako kama una utu, ama la peleka ushahidi kwenye hiyo familia, utakua umetenda haki
 
Kitu ambacho CHADEMA hawawezi kuthubutu ni kumuondoa Shibuda, wanajuwa wakifanya hivyo ndio kifo chao, kama wanabisha wamuondoe halafu waone nini kitafata.
 
kitu ambacho chadema hawawezi kuthubutu ni kumuondoa shibuda, wanajuwa wakifanya hivyo ndio kifo chao, kama wanabisha wamuondoe halafu waone nini kitafata.
hacha uhayawani wewe
lowasa ana fanya nini ccm?
Tena ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya ulinzi na usalama bungeni
kama chama chenu kina uthubutu inakuwaje gamba linashika hatamu
 
Mkuu nimtetee Mtatiro kwa nini? Hilo halihitaji utetezi ni suala la upinzani kukubaliana tu kwamba nani aachiwe baada ya kupima upepo. Lakini CDM walivyo na uroho wa madaraka hata kama hawakubaliki mahala wanaenda tu kugawa kura za wapinzani na matokeo yake: CDM 5, CUF 8, CCM 10!! CCM anatangazwa mshindi kwisha habari.

sio kila anayeichagua cuf ataichagua cdm kama cuf haipo inategemea na mapenzi ya mtu binafsi. kwa hiyo tuache kila chama chenye uwezo wa kusimamisha mgombea kisimamishe kwasababu lengo la msingi ni kushika hatamu.
 
Kimbunga kama unafuatili siasa vizuri utagundua kuwa katika kampeni suala siyo kushinda tu. Chama kinapofanya kampeni kinakuwa na malengo mapana ya kufanya publicity. Ndiyo maana vyama ambavyo havijitokezi kwenye kampeni havifahamiki kwenye maeneo hayo. Tena mfano wa wazi ni kwamba, ingawa CDM hawakupata dola 2010 lakini kampeni zao zimezaa matunda mzuri sana.

Hivyo, regardless kuwa chama kitashinda ama kushindwa ni vizuri kwa ustawi wa chama husika kufanya kampeni. Hii inawasadia kupata wanachama na kufungua matawi. Hivyo, inawawekea msingi wa baada. Hata hivyo, kwa Igunga si sahihi kusema wapinzani waachine. Kwani kila chama kina mikakati yake na mipango yake ya kushinda. Vinginevyo uwe unasema kwa ushabiki wa chama fulani.

Mkuu nimtetee Mtatiro kwa nini? Hilo halihitaji utetezi ni suala la upinzani kukubaliana tu kwamba nani aachiwe baada ya kupima upepo. Lakini CDM walivyo na uroho wa madaraka hata kama hawakubaliki mahala wanaenda tu kugawa kura za wapinzani na matokeo yake: CDM 5, CUF 8, CCM 10!! CCM anatangazwa mshindi kwisha habari.
 
Kila chama kina sera na itikadi zake, wacha vyama vyote viende kupambana
 
Bahati nzuri amekwisha gundulika, ni rahisi sana kumhandle!
 
Kitu ambacho CHADEMA hawawezi kuthubutu ni kumuondoa Shibuda, wanajuwa wakifanya hivyo ndio kifo chao, kama wanabisha wamuondoe halafu waone nini kitafata.

mwisho wao kivipi? cause they have been kabla hata hajajiunga nao
 
Back
Top Bottom