Wadai ujana wao utawapeleka pabaya. Wakae watulie, na wajifunze kwa wazee.
Ni kweli huku akijua kuwa nguzo kubwa ya CDM ni vijana amewaponda wabunge vijana kuwa wawe na busara na kuwa wazee ni hazina, yaani hata nimeshindwa kuwa specific ya yale aliongea lakini kwa tuliomuona amefuka Moshi sana.Baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa Katibu wa wabunge wa CDM John Mnyika aliomba wabunge wote wakutane.Nadhani suala la Shibuda litakuwa linajadiliwa.To me Shibuda ni wa kusimamishwa ubunge na kama ikiwezekana Kamati Kuu ya CDM imtimue mara moja.Kwa kilichojitokeza leo bungeni ni fedheha kubwa.Shibuda ni makapi na hafai kuwa ndani ya CDM
Wadai ujana wao utawapeleka pabaya. Wakae watulie, na wajifunze kwa wazee.
Mkuu yalikuwa mashairi huku akishangiliwa kwa nguvu sana na watu wa CCM hata kupata flow yake na kuipresent ni ngumu kidogo lakini ukweli hakuongea vyema.Alimesema maneno gani mbona hamumquote? na sisi tuchangie?
Wamfukuze tu, wasingekuwa vijana wala asingepata ushindi,na angegombea kupitia chama tofauti na CHADEMA leo hii hasingekuwa bungeni. Wamuondoe haraka la sivyo atakiua chama.maneno ya shibuda ni machafu mno,imenishtua mno kuwa mtu kama huyu imekuwaje cdm hawakumjua mapema,wasipomfukuza mara moja ni hatari sana,shibuda jina la cdm limembeba sana,inashangaza maneno yale bungeni.jamani hiyo nidhamu anayosema shibuda kuwa vijana hatuna ndio hiyo anayotufundisha kubwabwaja kimipasho bungeni ukikiponda chama chako! Cdm wasipomfukuza haraka sana itashangaza sana,hakuna cha kutaka radhi wala maelezo wacha cdm wapoteze jimbo lakini walinde heshima yao na misimamo yao.