Sheria ziwaongoze vijana katika kufanya maamuzi

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
277
1,000
SHERIA ZIWAONGOZE VIJANA KUFANYA MAAMZI YA NAFASI ZAO.

Vijana wengi wamekuwa wakiaminiwa kwenye serikali na vyama vyao vya siasa tangu nchi hii ilipopata uhuru. Imani hii kwao inatokana na ukweli kwamba hata msingi wa uhuru wa nchi hii ni matokeo ya Umoja wa Vijana walioamua kuungana na kupigania uhuru.

Wapo Vijana ambao umekuwa mfano bora kwenye jamii pindi wanapopewa madaraka na Wapo ambao umekuwa mfano mfu kwenye jamii na kuua kabisa ndoto za Vijana wengine. Hii ni kwa kuwa Vijana wengine pindi wanapopewa madaraka wamekuwa wanaomgoza kwa mihemko na si kufuata sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya kikazi.

Mantiki yangu si kwamba wazee hawakosei rahashaa! Wapo wazee wanaokosea sawa sawa na Vijana. Lakini wakati Mwingine hatuhitaji sana kuyajadili makosa ya wazee kwa kuwa kwa mkudha wa kisayansi tunaamini wanakuwa wameshalitumikia Taifa kwa muda mrefu na akili nayo inakuwa umechoka.

Kijana unapopewa nafasi ya kuongoza na kwa muda mfupi unagubikwa na tuhuma za utawala wa hovyo ni fedheha kwa jamii na kwa Vijana wote ambao walidhani wewe utakuwa taa yao. Ninazungumzia tuhuma kwa kuwa tuhumu ni dhahania inayoweza kukuleta kwenye makosa au kukuokoa kwenye makosa. Lakini kwa nini utuhumiwe?

Mhe Rais Samia wiki iliyopita akiwaapisha Makatibu tawala wa mikoa aliwasistiza kuzingatia sheria kwenye uongozi wao. Alisistiza kuwa kwenye utawala wowote kiongozi anapaswa kutumia maamzi yake sheria kwa 70% na maarifa binafsi ambayo msingi wake ni hekima 30%. Lakini Vijana wengine kwenye utawala wao wamekuwa wakifanya kinyume 30% sheria na 70% hekima( Maarifa binafsi).

Msingi wa makosa haya kwa Baadhi ya Vijana wetu waliopata nafasi ya kuongoza ni tamaa. Tamaa ndiyo inayowatawala na kuwafanya Vijana wengi kuingia kwenye migogoro na jamii wanazoziongoza. Vijana wenye aina hii ya utawala ni wale ambao wanataka kutumia madaraka yao kuwanyonya wale wanaowaongoza. Hawa wanapora mali za Wananchi kwa nguvu na kutumia nguvu kuongoza ili kuwatisha Wananchi.

Mimi ninajiuliza je, kila kiongozi akiamua kutumia nguvu kutawala, yaani kutawala bila kuzingatia sheria. Kila mtu akatumia nguvu kukwapua fedha za Wananchi, Maendeleo ya Taifa yatakuwaje? Kwa nini Vijana wengi hawaridhiki na mishahara wanayopata? Nimesema leo ninazungumza na Vijana ambao ndio wenye hati na hili Taifa.

Kijana anapojigeuza kuwa malaika kwenye Ofisi za umma huku akiongoza kama Shetani anakuwa anatafsiri nini katika uongozi wake? Anakuwa anapeleka ujumbe gani kwa waliomteua?

Ulimbukeni wa madaraka ndio unaowafanya Vijana waliowengi kuonyesha hawafai kuendelea kuwa kwenye nafasi zao kwani wameshindwa kuonyesha kile ambacho waliowateua wangetarajia. Unapokuta kijana kageuza Ofisi yake imekuwa Mahakama ya kutolea haki na kutolea adhabu unajiuliza huyu anaongoza taasisi au Wananchi kwa kutumia sheria ipi? Je huyu kiongozi anayeweza kutoa amri na maelekezo batili anatoa wapi mamlaka?

Kabla ya Mhe Rais Mama Samia kutolea mkazo kuwa kila mtu azingatie sheria tulikuwa tumeshuhudia Ofisi zingine kuadhibu watu na fimbo bila kibali Cha Mahakama. Tulishuhudia wakati Mwingine nguvu kubwa ikitumika kuhalalisha ubaya kuwa uzuri. Watu walifanya daraja la ubinadamu. Wapo waliokuwa wanaweza kumfanya binadamu chochote na asikemewe. Wapo ambao kwao sheria zilikuwa si stahiki kwao, bali waligeuza mawazo yao kuwa sheria na mwongozo.

Mhe Samia kwa muda mfupi tangu aapishwe amekuwa Mwalimu mzuri wa kutufundisha namna sheria inavyoweza kuleta furaha kwa watu wanaotofautiana. Kitendo chake Cha kusistiza kila anapowaapisha Wateule wake kusimamia sheria lakini na wakati Mwingine kutumia busara kufanya maamuzi ni ujumbe tosha kuwa watakaoshindwa kutii hayo maelekezo watakutana na rungu la udhibiti. Huu ni muda mwafaka wa wale walioteuliwa kumsaidia Mhe Rais kubadilisha mtazamo wao wa namna ya kuwaongeza Wananchi.

Benki ya Dunia, inakadiria ifikapo mwaka 2050 idadi ya vijana katika kundi hili hasa katika bara la Afrika pekee itaongezeka na kufikia asilimia 30 ya watu wote. Kwa takwimu za Tanzania vijana walio na umri wa miaka 15 hadi 24 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 wanafikia milioni 8.6 sawa na asilimia 20 ya watanzania wote milioni 44.9.

Nchini Tanzania vijana walio katika umri kati ya miaka 18 – 35 wanafikia milioni 15.6 sawa na asilimia 35 ya watanzania wote. Hili ni kundi mahsusi kwa sababu ndilo kundi pekee linaloonekana kuwa kubwa kuliko kundi jingine lolote kijamii hapa nchini. Ni kundi linalokabiliwa na changamoto nyingi, na ni kundi maalumu kisiasa Hivyo Vijana wanaopata nafasi katika uongozi wanapaswa kuwa mfano bora kwenye nafasi walizoaminiwa badala ya kuwa kikwazo Cha kuumiza watu wengine.

Takwimu hizi zinatoa picha moja muhimu siyo tu kwa waandaaji wa sera na serikali, lakini pia kwa jamii inayowajibika kuhakikisha ustawi na maendeleo kwa vijana kiuchumi, kisiasa, na kidemokrasia. Jambo hili si lingine bali ni idadi hii na ongezeko hili la vijana, huko tuendako dunia itakabiliwa na changamoto nyingi hasa zinazowahusu vijana kama hatua madhubuti hazitachukuliwa mapema. Ni wajibu wa wanaopata nafasi kuzitumia kwa weledi mkubwa na kuacha alama inayoongesha namna nchi itakavyokuwa na viongozi mahili mara baada ya wazee wetu kustaafu.

Lakini Vijana tunapokuwa mfano wa utawala unaojenga nyufa, basi tunakosa uhalali wa kuijenga Tanzania bora ambayo inawategemea Vijana ambalo ni kundi kubwa.

Ushauri wangu kwa Vijana ni kuwa tunapopata nafasi basi tuzitumie kwa kuacha uongozi uliotukuka ili tukiondoka Duniani tukumbukwe kwa mema na si kwa mabaya tuliyofanya. Tuzingatie ubinadamu kwenye kila maamzi tunayofanya hasa kwa kuvaa uhusika kwanza. Taifa hili ni letu wote, hakuna mwenye daraja la tofauti. Uongozi ni sehemu tu ya uaminifu wa muda mfupi. Tufanye mema ili tukumbukwe kwenye wema, ipo siku tutakufa. Tukifa lakini tukiwa tumefanya mema hata makaburi yetu yataombewa , lakini tukifa tukiwa tumewaumiza watu hata makaburi yetu yatanenewa mabaya.

Unapoaminiwa kuwa kiongozi si kwamba wewe unaakili kuliko wengine wote, bali wewe umepata bahati kwa kipindi hicho. Hiyo bahati usitumie kuwaumiza wenzako, bali kuwaunganisha. Pokea ushauri hata kwa ambao hawajapata bahati ya kuwa viongozi, kwani wapo wenye uwezo kukudhidi lakini hawajapata bahati ya kuwa hapo ulipo.Utawala bora msingi wake ni ushirikishwaji na si uongozi wa mabavu.

0768239284
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom