Selwa
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 573
- 578
Juzi nilikuwa maeneo ya selander bridge naelekea upanga. Kwa bahati mbaya kwenye mataaa taa ya njano ikanikuta nipo mbele ya zebra nikasita kuendelea maana nikajua nyekundu itanikuta mbele tu na nitakamatwa. Basi nikasimama na kurudi nyuma. Ikawa nyekundu taaa tukasimama. Ilivorudi kijani nikaendelea cha kushangaza traffic akaniandikia fine makosa mawili. Kusimama juu ya zebra kupita red light...baada ya kubishana kwamba kaka nimesimama kwenye njano tu ilivowaka akalitoa hilo kosa nikabaki na kosa la kusimama juu ya zebra nikamwambia kaka sasa pale nilipokuoepo ningesimama pale pale ningecause obstruction ningeendelea nimepita redlight kurudi nyuma zaidi kuna gari na taaa haijanizimikia imenikuta yellow light nilikuwa sipo speed..ningeeenda wapi ili usiniandikie fine...akasema huwezi uka tembea siku nzima hujatenda kosa akanikatia ticket...sasa nataka ushauri wenu wandugu hivi hii dheria imekaa sawa? Nataka kulipeleka hili suala mahakamani tuichallenge hii sheria maana ni fine yangu ya tatu