Taa za Namanga, mke wa Balozi Mahiga na tamko la rais

From Sir With Love

JF-Expert Member
Sep 13, 2010
2,076
3,804
Poleni na Majukumu.

Sina nia ya kuendeleza mjadala unaohusisha tuhuma za Mke wa Balozi Mahiga kumtukana askari na baadaye Rais Magufuli kutoa agizo huyo askari apandishwe cheo, lakini natoa angalizo kwa yale yaliyonikuta pale taa za Namanga kama unaelekea kulia kwenda msasani.

ANGALIZO 1: Sijafatilia kujua kama mtafaruku tajwa hapo juu unahusiana na taa za Namanga, japo inaelezwa sehemu tajwa ni Namanga. Kama maelezo yangu yatakuwa hayarandani na eneo la tukio basi huu uzi utakuwa wa kuelimisha tu na sio vinginevyo.

ANGALIZO 2: Nina mwezi mmoja tangu nitoke Dar inawezakana hizo taa zimesharekebishwa.

Mwezi mmoja sasa umepita tangu askari anikamate. Nilikuwa natokea taa za St. Peters kuelekea taa za Namanga ili nikunje kulia kuelekea Msasani. Taa za Namanga zilikuwa zimeruhusu kuelekea kulia (Kuelekea msasani). Ghafla ule mshale unaoonyesha kwenda kulia ulizima na taa nyekundu zikawaka. Wakati hili linatokea nilikuwa tayari najiandaa kukata kona kuelekea msasani lakini kwa sababu mwendo wangu haukuwa mkubwa nilisimama. Nafikiri pana Zebra japo sina uhakika. Kwa maana hiyo nitakuwa lazima nilizikanyaga au nilikuwa mbele zaidi.

Nilisubiri taa ziniruhusu kuelekea Msasani. Kwa mbele kumbe askari alikuwa ananisubiri kwa hamu. Akanipiga mkono na nikasimama. Nikamsalimia kwa heshima zote na nikampa pole kwa majukumu. Akaniomba leseni nikampa.

Akaniuliza kama najua kosa langu au anipeleke nikalale ndani. Nikamwambia kwa mwonekano naonekana nimefanya kosa lakini kinadharia makosa sio yangu. Hapo ndipo alipoanza kunieleza kwamba unajua gari ni kaburi na pale uliposimama haparuhusiwi kusimama. Akaenda mbele kusema labda nilikuwa natafuta sifa kwa mke wangu. (Wife alikua pembeni) Dah nikacheka moyoni na kusema huyu hanipati japo nilimwambia kwamba gari langu sio kaburi ni gari.

Nikatumia utashi na wala sikugombana naye. Sikumpa sababu ya kugombana. Nikamuuliza kama anajua Taa za njano haziwaki pale taa za Namanga. Akaniambia zinawaka ila labda zimefifia na hilo ni tatizo la TANROADS. Nikamwambia hizo taa haziwaki na ni muhimu ziwake ili kama dereva ameisha kunja kuingia kulia na taa za kijani zikazima basi taa za njano zinamruhusu Dereva kumalizia kwenda lakini kwa tahadhari. Lakini kwa taa za njano kutokuwaka lazima tu kuna dereva atamalizia kuvuka na taa nyekundu au atasimama niliposimama mimi.

Yule askari hakuelewa lakini tuliyamaliza.

SOMO:

1. Askari siku hizi wanakaa pale namanga kusubiria taa za kwenda msasani zizime ghafla bila njano kuwaka na hivyo kusema umepita wakati taa nyekundu zinawaka.

2. Kama upo kwenye mwendo wa taratibu na ukawa unaelekea kulia (Msasani) na ukagundua taa za kukuruhusu zimezima, asilimia kubwa sana lazima utasimama mbele au katikati ya Zebra.

3. Kama Mfano wangu unarandana na wa Mama Mahiga basi yule traffic ana makosa kwa sababu tatizo ni taa za njano kutokuwaka na askari anakiri hilo sio tatizo lao bali la TANROADS.

4. Rais Magufuli angemuagiza IGP afatilie ilivyokuwa ili apate tabia au uadilifu wa yule askari na vigezo vya askari kupandishwa cheo. ( Hii inasaidia kujua kama yule askari ana skendo zozote au labda ana barua za onyo kuhusu vitu fulani ambazo zingeleta picha tofauti kwa askari wengine waadailifu ambao hawajawahi kupandiswa cheo.)

5. Kwa madereva. Kuna askari waaminifu na waadilifu sana, na kunao baadhi tabia zao zinaharibu jina la askari wote wa barabarani. Muhimu ni kutokulipuka wanapo kuudhi lakini simamia haki wa ueledi na utashi.

ANGALIZO TENA:

1. Sitetei mtu kuvunja sheria wala kutukana kwa sababu ya cheo chake wala familia yake

2. Recorded clip kati ya askari wa barabarani, Mama Mahiga na RTO haina tukano lolote kwenda kwa yule askari, unless kama askari alichelewa kurekodi.

3. Kazi ya askari barabarani inaelekea kwenye kukusanya mapato zaidi siku hizi badala ya kuelemisha na kusimamia sheria. (Kipimo cha kufanya kazi sana kwao ni kiasi cha mapato kitakachoingia)

Unazunguuuuka lkn lengo lako ni lile lile tu la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki jambo ambalo limeshajadiliwa kwa kina na mapana na hakuna kilichobakia tena kujadili! sasa si ungehifadhi muda na akili yako kwa mambo mengine na kuandika tu moja kwa moja kuhusu Mke wa Waziri Mahiga na trafiki?? au uliogopa labda uzi wako kuunganishwa???
 
Mkuu. Issue yangu kubwa ni ubovu wa taa za Namanga ili haya ya Mke wa Balozi yasijirudie. Kama issue ni kama yangu basi hata huo mtafuruku usingekuwepo.
 
Siyo kweli, kwani ungeweza pia kuandika uliyoaandika bila ya kuhusisha na Mahiga na trafiki, ukisoma ulichoandika kila kinajitosheleza na hakuna sababu hata ya kutaja Mahiga na trafiki!
 
ANGALIZO TENA:

1. Sitetei mtu kuvunja sheria wala kutukana kwa sababu ya cheo chake wala familia yake

2. Recorded clip kati ya askari wa barabarani, Mama Mahiga na RTO haina tukano lolote kwenda kwa yule askari, unless kama askari alichelewa kurekodi.

3. Kazi ya askari barabarani inaelekea kwenye kukusanya mapato zaidi siku hizi badala ya kuelemisha na kusimamia sheria. (Kipimo cha kufanya kazi sana kwao ni kiasi cha mapato kitakachoingia)

Hili la mwisho nadhani ndiyo jipu sahihi!
Hatujengi jamii sahihi kwa staili hii na hata magereza yako kwa ajili ya kurekebisha wahalifu! Mtindo huu wakugeuza Jeshi la Polisi kuwa kama TRA siyo afya kitaasisi- na mbaya zaidi hakuna kitengo cha dharua cha kuwalinda walaji ambao ndiyo Madereva!
 
Poleni na Majukumu.

Sina nia ya kuendeleza mjadala unaohusisha tuhuma za Mke wa Balozi Mahiga kumtukana askari na baadaye Rais Magufuli kutoa agizo huyo askari apandishwe cheo, lakini natoa angalizo kwa yale yaliyonikuta pale taa za Namanga kama unaelekea kulia kwenda msasani.

ANGALIZO 1: Sijafatilia kujua kama mtafaruku tajwa hapo juu unahusiana na taa za Namanga, japo inaelezwa sehemu tajwa ni Namanga. Kama maelezo yangu yatakuwa hayarandani na eneo la tukio basi huu uzi utakuwa wa kuelimisha tu na sio vinginevyo.

ANGALIZO 2: Nina mwezi mmoja tangu nitoke Dar inawezakana hizo taa zimesharekebishwa.

Mwezi mmoja sasa umepita tangu askari anikamate. Nilikuwa natokea taa za St. Peters kuelekea taa za Namanga ili nikunje kulia kuelekea Msasani. Taa za Namanga zilikuwa zimeruhusu kuelekea kulia (Kuelekea msasani). Ghafla ule mshale unaoonyesha kwenda kulia ulizima na taa nyekundu zikawaka. Wakati hili linatokea nilikuwa tayari najiandaa kukata kona kuelekea msasani lakini kwa sababu mwendo wangu haukuwa mkubwa nilisimama. Nafikiri pana Zebra japo sina uhakika. Kwa maana hiyo nitakuwa lazima nilizikanyaga au nilikuwa mbele zaidi.

Nilisubiri taa ziniruhusu kuelekea Msasani. Kwa mbele kumbe askari alikuwa ananisubiri kwa hamu. Akanipiga mkono na nikasimama. Nikamsalimia kwa heshima zote na nikampa pole kwa majukumu. Akaniomba leseni nikampa.

Akaniuliza kama najua kosa langu au anipeleke nikalale ndani. Nikamwambia kwa mwonekano naonekana nimefanya kosa lakini kinadharia makosa sio yangu. Hapo ndipo alipoanza kunieleza kwamba unajua gari ni kaburi na pale uliposimama haparuhusiwi kusimama. Akaenda mbele kusema labda nilikuwa natafuta sifa kwa mke wangu. (Wife alikua pembeni) Dah nikacheka moyoni na kusema huyu hanipati japo nilimwambia kwamba gari langu sio kaburi ni gari.

Nikatumia utashi na wala sikugombana naye. Sikumpa sababu ya kugombana. Nikamuuliza kama anajua Taa za njano haziwaki pale taa za Namanga. Akaniambia zinawaka ila labda zimefifia na hilo ni tatizo la TANROADS. Nikamwambia hizo taa haziwaki na ni muhimu ziwake ili kama dereva ameisha kunja kuingia kulia na taa za kijani zikazima basi taa za njano zinamruhusu Dereva kumalizia kwenda lakini kwa tahadhari. Lakini kwa taa za njano kutokuwaka lazima tu kuna dereva atamalizia kuvuka na taa nyekundu au atasimama niliposimama mimi.

Yule askari hakuelewa lakini tuliyamaliza.

SOMO:

1. Askari siku hizi wanakaa pale namanga kusubiria taa za kwenda msasani zizime ghafla bila njano kuwaka na hivyo kusema umepita wakati taa nyekundu zinawaka.

2. Kama upo kwenye mwendo wa taratibu na ukawa unaelekea kulia (Msasani) na ukagundua taa za kukuruhusu zimezima, asilimia kubwa sana lazima utasimama mbele au katikati ya Zebra.

3. Kama Mfano wangu unarandana na wa Mama Mahiga basi yule traffic ana makosa kwa sababu tatizo ni taa za njano kutokuwaka na askari anakiri hilo sio tatizo lao bali la TANROADS.

4. Rais Magufuli angemuagiza IGP afatilie ilivyokuwa ili apate tabia au uadilifu wa yule askari na vigezo vya askari kupandishwa cheo. ( Hii inasaidia kujua kama yule askari ana skendo zozote au labda ana barua za onyo kuhusu vitu fulani ambazo zingeleta picha tofauti kwa askari wengine waadailifu ambao hawajawahi kupandiswa cheo.)

5. Kwa madereva. Kuna askari waaminifu na waadilifu sana, na kunao baadhi tabia zao zinaharibu jina la askari wote wa barabarani. Muhimu ni kutokulipuka wanapo kuudhi lakini simamia haki wa ueledi na utashi.

ANGALIZO TENA:

1. Sitetei mtu kuvunja sheria wala kutukana kwa sababu ya cheo chake wala familia yake

2. Recorded clip kati ya askari wa barabarani, Mama Mahiga na RTO haina tukano lolote kwenda kwa yule askari, unless kama askari alichelewa kurekodi.

3. Kazi ya askari barabarani inaelekea kwenye kukusanya mapato zaidi siku hizi badala ya kuelemisha na kusimamia sheria. (Kipimo cha kufanya kazi sana kwao ni kiasi cha mapato kitakachoingia)

Mkuu kwenye angalizo namba 2 umezungumzia swala la trafic kuongea na rto kwann umewaza kusema alionhea na rto wake moja kwa moja kwani hakuna mdogo wa chini uliyemfikiria mpaka kumuongelea RTO
 
Inawezekana kabisa aliongea na mwenye cheo kingine zaidi ya hicho. Lakini ingekuwa vyema ungesema aliongea na nani kama sio RTO.
 
Mkuu. Issue yangu kubwa ni ubovu wa taa za Namanga ili haya ya Mke wa Balozi yasijirudie. Kama issue ni kama yangu basi hata huo mtafuruku usingekuwepo.

Lakini mama kosa lake halikuhusiana na taa kabisa, na hata maelezo yake hakuna sehemu kalalamika taa mbovu.
 
Ni ukweli usiojoficha traffic police majukumu yao siku hizi ni kukusanya hela, hawazongatii maadili ya kazi yao wanachofanya ni kukutafutia sababu ulipe hela wakiona unaijua sheria atakusemesha maneno ya karaha tu ili upandishe jazba, ukimjibu kisheria atakuambia unanifundisha kazi sio sasa wacha nikuonyeshe mimi ni nani yaani lazima utatoa hela tu akikuamulia.
 
Poleni na Majukumu.

Sina nia ya kuendeleza mjadala unaohusisha tuhuma za Mke wa Balozi Mahiga kumtukana askari na baadaye Rais Magufuli kutoa agizo huyo askari apandishwe cheo, lakini natoa angalizo kwa yale yaliyonikuta pale taa za Namanga kama unaelekea kulia kwenda msasani.

ANGALIZO 1: Sijafatilia kujua kama mtafaruku tajwa hapo juu unahusiana na taa za Namanga, japo inaelezwa sehemu tajwa ni Namanga. Kama maelezo yangu yatakuwa hayarandani na eneo la tukio basi huu uzi utakuwa wa kuelimisha tu na sio vinginevyo.

ANGALIZO 2: Nina mwezi mmoja tangu nitoke Dar inawezakana hizo taa zimesharekebishwa.

Mwezi mmoja sasa umepita tangu askari anikamate. Nilikuwa natokea taa za St. Peters kuelekea taa za Namanga ili nikunje kulia kuelekea Msasani. Taa za Namanga zilikuwa zimeruhusu kuelekea kulia (Kuelekea msasani). Ghafla ule mshale unaoonyesha kwenda kulia ulizima na taa nyekundu zikawaka. Wakati hili linatokea nilikuwa tayari najiandaa kukata kona kuelekea msasani lakini kwa sababu mwendo wangu haukuwa mkubwa nilisimama. Nafikiri pana Zebra japo sina uhakika. Kwa maana hiyo nitakuwa lazima nilizikanyaga au nilikuwa mbele zaidi.

Nilisubiri taa ziniruhusu kuelekea Msasani. Kwa mbele kumbe askari alikuwa ananisubiri kwa hamu. Akanipiga mkono na nikasimama. Nikamsalimia kwa heshima zote na nikampa pole kwa majukumu. Akaniomba leseni nikampa.

Akaniuliza kama najua kosa langu au anipeleke nikalale ndani. Nikamwambia kwa mwonekano naonekana nimefanya kosa lakini kinadharia makosa sio yangu. Hapo ndipo alipoanza kunieleza kwamba unajua gari ni kaburi na pale uliposimama haparuhusiwi kusimama. Akaenda mbele kusema labda nilikuwa natafuta sifa kwa mke wangu. (Wife alikua pembeni) Dah nikacheka moyoni na kusema huyu hanipati japo nilimwambia kwamba gari langu sio kaburi ni gari.

Nikatumia utashi na wala sikugombana naye. Sikumpa sababu ya kugombana. Nikamuuliza kama anajua Taa za njano haziwaki pale taa za Namanga. Akaniambia zinawaka ila labda zimefifia na hilo ni tatizo la TANROADS. Nikamwambia hizo taa haziwaki na ni muhimu ziwake ili kama dereva ameisha kunja kuingia kulia na taa za kijani zikazima basi taa za njano zinamruhusu Dereva kumalizia kwenda lakini kwa tahadhari. Lakini kwa taa za njano kutokuwaka lazima tu kuna dereva atamalizia kuvuka na taa nyekundu au atasimama niliposimama mimi.

Yule askari hakuelewa lakini tuliyamaliza.

SOMO:

1. Askari siku hizi wanakaa pale namanga kusubiria taa za kwenda msasani zizime ghafla bila njano kuwaka na hivyo kusema umepita wakati taa nyekundu zinawaka.

2. Kama upo kwenye mwendo wa taratibu na ukawa unaelekea kulia (Msasani) na ukagundua taa za kukuruhusu zimezima, asilimia kubwa sana lazima utasimama mbele au katikati ya Zebra.

3. Kama Mfano wangu unarandana na wa Mama Mahiga basi yule traffic ana makosa kwa sababu tatizo ni taa za njano kutokuwaka na askari anakiri hilo sio tatizo lao bali la TANROADS.

4. Rais Magufuli angemuagiza IGP afatilie ilivyokuwa ili apate tabia au uadilifu wa yule askari na vigezo vya askari kupandishwa cheo. ( Hii inasaidia kujua kama yule askari ana skendo zozote au labda ana barua za onyo kuhusu vitu fulani ambazo zingeleta picha tofauti kwa askari wengine waadailifu ambao hawajawahi kupandiswa cheo.)

5. Kwa madereva. Kuna askari waaminifu na waadilifu sana, na kunao baadhi tabia zao zinaharibu jina la askari wote wa barabarani. Muhimu ni kutokulipuka wanapo kuudhi lakini simamia haki wa ueledi na utashi.

ANGALIZO TENA:

1. Sitetei mtu kuvunja sheria wala kutukana kwa sababu ya cheo chake wala familia yake

2. Recorded clip kati ya askari wa barabarani, Mama Mahiga na RTO haina tukano lolote kwenda kwa yule askari, unless kama askari alichelewa kurekodi.

3. Kazi ya askari barabarani inaelekea kwenye kukusanya mapato zaidi siku hizi badala ya kuelemisha na kusimamia sheria. (Kipimo cha kufanya kazi sana kwao ni kiasi cha mapato kitakachoingia)

Hivi bado huyu mama anawatuma tu! Atamuharibia mumewe sasa! Ye si anyamaze tu yaishe!
 
Unazunguuuuka lkn lengo lako ni lile lile tu la Mke wa Waziri Mahiga na Trafiki jambo ambalo limeshajadiliwa kwa kina na mapana na hakuna kilichobakia tena kujadili! sasa si ungehifadhi muda na akili yako kwa mambo mengine na kuandika tu moja kwa moja kuhusu Mke wa Waziri Mahiga na trafiki?? au uliogopa labda uzi wako kuunganishwa???
 
Kuna Askari wa kaki za kijani wanakaa pale Taa za Upanga KEMPISK au Peugeot House kuelekea Mnazi mmoja. Mbele yao ni askari wa treffic.
Ukipita ghafla ilawaka taa ya njano wanakukimbilia kukustop kwa Mkono. Mbele hatua 30 tayari wapo traffike wanakumalizia.
Sasa sijui hiyo njano imewekewa timing ya namna gani na kabla kuvuka kuna rubber humps/ matuta ya mpira ambayo yatakuchelewesha kidogo. Imenikuta weekendwakati magari sio mengi. This could be a tricky booby trap for something fishy.
 
Unatoaje angalizo halafu unasema hujafuatilia !!
Makala yanamna hiyo hata sisomi. Fuatilia kwanza ndo uje!!!
 
Back
Top Bottom