Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Hakika hili ndio jambo la msingi sana tunahangaika sana lakini kumbe kuna mahala kuna dawa ya watawala kama hii tukiiweka kuwa ndio ajenda yetu kuu hakika kuna mwanga mwisho wa shimo kama sio mwezi basi jua tuna mengi ya kupigania ikiwa na hili kama tutalifanya ajenda yetu na hakika wenye kuona mbali watakua wameliona na hili ni jambo muhimu sana kwa wakati huu na ujao
 
Kama tumeweza kuwa na wabunge wa kuteuliwa, na tatizo letu ni gharama za uchaguzi, na wananchi walishakikubali chama fulani kutoa mbunge kwa miaka mitano, kwa nini tusikipe chama hicho kilichoshinda uchaguzi nafasi ya kuteua mbunge atakayeshika ubunge huo mpaka uchaguzi mkuu ujao?
mkuu hiii hoja nayo inamashiko, tena itakomesha mzizi wa fitina, mtu hataweza kuhama chama A halafu tena akagombee nafasi ile ile chama B, kikubwa hapa chama kitapewa haki ya kumchagua mbadala wake mpaka mda utapoisha, lakini je nani yuko tayari kukubali hili wakati mfumo uliopo unakibeba chama tawala?
 
Amdiko limejitosheleza na mapendekezo kuhusu way forward ni mazuri lakini kikwazo ni strategy gani itatumika kutekeleza hayo mapendekezo tatizo wengi wetu wasio wanachama hawana platform ya kuongelea mawazo yao inahitajika platform ya wanaharakati wakuongoza kufikia hayo malengo, hili ni jambo kubwa limahitaji uungwaji mkono na watu wengi siyo la watu wachache kwakuwa kutakuwa na nguvu kubwa ya kubeza mabasiliko yanayopendekezwa. Ila mimi mapendekezo kuwa badala ya kuchukuwa aliyekuwa mshimdi wa pili wa Tatu na kuendelea pale jimbo linapokuwa wazi uwekwe utaratibu kuwa chama kilichokuwa na huyo mbunge kiruhusiwe kuchagua mbunge wa muda kumalizia muda uliobaki hadi uchaguzi mwengine, ila endapo mbunge alikuwa mgombea binafsi basi hapo ufanyike uchaguzi .
 
Hutakiwi kulinganisha nchi ambayo mgombea huru anaruhusiwa lakini hafanikiwi, na mgombea huru nchi ambayo haruhusiwi kabisa.

Labda kwenye urais tu lakini kwenye ugavana, useneta, ubunge wa wawakilishi, umeya, na kadhalika, independent candidates Marekani huwa wanashinda.

Sijui jamaa hapo alikuwa analinganisha nini hasa....lakini mtu hawezi tu kusema kijumla jumla kuwa Marekani independent candidates hawashindi.

Huwa wanashinda kwenye ngazi zote za serikali kuanzia local, state, na federal.
 
Boss Pascal Mayalla Umeongea vizuri sana sana na mno. Ushauri na Mapendekezo yako yote matano aka 5 ninayaunga Mkono Hoja. Pendekezo lako la 3 aka tatu, Mimi Binafsi niliweka uzi humu nikimshauri Rais wetu afute hizi Chaguzi. Labda Chaguzi za Kiongozi kufariki. Hiyo haina neno. Otherwise hizi chaguzi ni kupoteza pesa ya Mlalahoi na mlipa kodi.
 
Well said paskali, lakini unazani hayo uliyosema hawayajui, they know everything lakini wanafanya ujinga kama ulivyosema ili kukizi personal interest kwa gharama za walalahoi.
 
Nimesearch hata hao USA waliona independent candidate ni failing way ndiyo maana toka mwaka 1922 hajawahi tokea akashinda huyo mgombea huru rejea

Ni ujinga kuadvocate mgombea huru sababu hakutakua na kitu cha kumcontrol maamuzi yake specially kwa katiba zetu za unga mwana!..

Kuwepo mgombea binafsi ni jambo moja, kushinda ni jambo jingine. Kumcontrol ni kuwa na taasisi zenye nguvu. Kwani hapa kwetu huyu aliyepo anatokana na chama ni chombo kipi kinamcontrol maamuzi yake?
 
Pascal Mayalla naunga mkono hoja yako, huu upuuzi unaoendelea nchini hivi sasa na huyu anayejidai anabana matumuzi upigwe vita kwa nguvu zote.

Kwanza kuna gharama hizi za kutoa rushwa ili wachumia tumbo wahamie kwenye chama cha wahuni. Inawezekana kabisa huyu kwa tabia yake ya kuchota pesa hazina bila idhini ya Bunge hizi ni pesa zilizochotwa hazina.

Bila shaka wanahongwa kuanzia milioni 100 kwenda juu. Gharama za uchaguzi wa jimbo moja ni zaidi ya bilioni 2. Mwanzoni mwa mwaka huu jimbo lenye watu wachache la dimani gharama zilikuwa ni 1.7 bilioni.

Kwa hiyo kwa huu upuuzi anaofanya huyu aliyesukumiziwa Ikulu kwa majimbo mawili aliyonunua Wabunge tayari kishawabebesha walipa kodi gharama za kipuuzi ambazo zingeweza kabisa kuepukwa za zaidi ya bilioni 4 kwenye majimbo hayo mawili na gharama za uchaguzi wa Madiwani si chini ya 250 milioni.

Hichi anachokifanya huyu ni cha kipuuzi sana na ni lazima tukemee kwa nguvu zote.

^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^^

Tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) itatumia Sh bilioni 3.9 kama gharama za uchaguzi katika Jimbo la Dimani, Zanzibar na kata 22 ambazo zitafanya uchaguzi wa madiwani. Uchaguzi wa Jimbo la Dimani utagharimu Sh bilioni 1.7 na ule wa kata 22 unatarajia kugharimu Sh bilioni 2.2.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo, Ramadhani Kailima wakati akizungumza na vyombo vya habari kuhusiana na chaguzi ndogo zinazotarajiwa kufanyika januari 22, 2017 katika jimbo la dimani na kata ishirini za Tanzania bara.

The post Uchaguzi Dimani kutumia Bilioni 1.7 appeared first on Zanzibar24.
 
Labda kwenye urais tu lakini kwenye ugavana, useneta, ubunge wa wawakilishi, umeya, na kadhalika, independent candidates Marekani huwa wanashinda.

Sijui jamaa hapo alikuwa analinganisha nini hasa....lakini mtu hawezi tu kusema kijumla jumla kuwa Marekani independent candidates hawashindi.

Huwa wanashinda kwenye ngazi zote za serikali kuanzia local, state, na federal.
Nafikiri alikuwa anaongelea urais kwamba tangu Perot hajasikia independent candidates
mkuu hiii hoja nayo inamashiko, tena itakomesha mzizi wa fitina, mtu hataweza kuhama chama A halafu tena akagombee nafasi ile ile chama B, kikubwa hapa chama kitapewa haki ya kumchagua mbadala wake mpaka mda utapoisha, lakini je nani yuko tayari kukubali hili wakati mfumo uliopo unakibeba chama tawala?
Watawala hawawezi kukubali.
 
Tutengeneze mazingira ya kumbana mgombea huru kabla ya kumruhusu kugombea tu!..
Haruhusiwi sio sababu haruhusiwi tu ni sababu mazingira hayaruhusu!..
Mazingira gani hayo?

Na kuna kipi kinachomzuia mtu kugombea kwa tiketi ya chama, halafu akifika kwenye urais awe rais anayekitupa chama kama Magufuli?

Hivi sasa kuna mtu katika CCM anaweza kumfunga kengele Magufuli?
 
Wasomi wa Tanzania ni majinga majinga na ndiyo yamejaa huko kunakofanywa uamuzi.Kila mtu anaona pesa hizi ni za umma hivyo hazina uchungu!Kama una viongozi wanaona hivyo,basi ujue safari yetu baado sana ukilinganisha na wenzetu kama Kenya.Ndio maana naona mfumo wa elimu hapa kwetu,unaambukiza upumbavu zaidi kuliko werevu
 
Mkuu Mayalla, I beg to differ.

You started on the wrong premises and ended on the wrong solutions.

Tatizo Ni katiba hasa ibara ya 74 inayounda tume hiyo. Uteuzi wa mwenyekiti na makamu wake kwa ukweli hauko open transparent and competitive hivyo mwenye mamlaka ya uteuzi anaweza kuteua mtu yoyote kukidhi mahitaji yake na Wala isipingwe popote.

Tume ya uchaguzi kiutawala nayo kimfumo haiko vizuri, uteuzi wa mkurugenzi wake Ni kama hao viongozi waandamizi.

Kumbuka tume Ni kama refa kwenye mashindano yenye ukinzani wa wazi. Mgombea kwenye kinyang'anyiro hicho ndio mteuzi wa watendaji wakuu kwenye tume ya uchaguzi.

Huhitaji kukumbushwa kuhusu principle za natural justice, hasa rule against bias. Tulipopuuzia na au kusahau rule ya bias kwenye muundo wa tume ndipo tuliipokosea big time to the detriment of the electorate.

Kisheria pia, wasimamizi wa uchaguzi wamewekwa kuwa ni wakurugenzi wa manispaa, ambao wote pia huteuliwa mtu mwenye maslahi yake binafsi kama mgombea na kitaasisi kama kiongizi wa chama. Hii nayo ni kinyume cha rule of bias.

Katiba hairuhusu kupinga uchaguzi wa Urais, je bado Ni muhimu kutopinga matokeo ya uchaguzi wa urais mahakamani? Huoni kama katiba ilikosea kwenye hili?

Turekebishe Kwanza hapa, mengine uliyoyaweka Ni madogo sana.
 
Back
Top Bottom