Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Wakuu,
Kichwa cha habari hapo juu chahusika.

Kufuatana na hali ya sintofahamu ya wabunge wa upinzani kununuliwa na maccm, ninapendekeza kwa viongozi wa ukawa per se waitishe mkutano wa wabunge wote wa upinzani na waambiwe kuwa kama kuna yoyote katika hao wabunge anataka kujiuzulu, basi wajiuzulu wote kwa pamoja ili serikali yetu tukufu sana ipate kupanga bajeti ya uchaguzi wa marudio iliyonyooka. Sio leo huyu kajiuzuru j3 yule ijumaa. Inaipa tume yetu tukufu shida. Wajiuzuru kwa umoja wao ili serikali ipange bajeti yake ya uchaguzi vizuri.

Hongereni Watanzania kwa demokrasia!
 
Walimjaribu , wameonja majaribu yao. Kwisha kama barafu ya mlima Kilimanjaro. Sasa hivi ni kupiga Magoti kama wamekula mlenda. Acha kumdharau raisi Msukuma utalamba ya Kafulila.
 
Uchaguzi wa Mbunge ni gharama kubwa sana hasa ikitokea nafasi ya Mbunge kuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali. Mimi naishauri Bunge letu litunge sheria kuwa:- Iwapo nafasi ya Mbunge itabaki wazi kutokana sababu mbali mbali basi nafasi hiyo ichukuliwe na mgombea aliyeshika namba mbili kwa kile Chama kilichoshinda na kuweza kumpata Mbunge mpya. Kwa wastani marudio ya uchaguzi wa Mbunge unachukua takriban Tshs.400 millioni. Fedha hizi ni nyingi sana na zingeweza kununua ambulace tatu kwa ajili ya Vituo vyetu vya Afya au kujenga Zahanati katika mojawapo ya Vijiji vyetu. Tuepuke matumizi mabaya ya rasilmali zetu. Nawasilisha.
 
Mkuu Paskali,
Umeleta furahiday ya majonzi kwa huu uzi wako. NMungu akubariki sana kwa huruma unayoipata juu ya taifa lako. HUU NDIO UZALENDO. BAABEJA SANA.
 
US wana mgombea binafsi.
Nimesearch hata hao USA waliona independent candidate ni failing way ndiyo maana toka mwaka 1922 hajawahi tokea akashinda huyo mgombea huru rejea
The first president, George Washington , was elected as an independent. Since the election of his successor, John Adams , in 1796, all winners of U.S. presidential elections have represented one of two major parties. Third parties have taken second place only twice, in
1860 and 1912.
The last time a third (independent candidate) achieved significant success (although still finishing in third place) was in 1992 , and the last time a third-party candidate received any electoral votes not from faithless electors was in 1968 .
Ni ujinga kuadvocate mgombea huru sababu hakutakua na kitu cha kumcontrol maamuzi yake specially kwa katiba zetu za unga mwana!..
 
Shida yako mayalla wewe ni kigeugeu,hata ikitokea siku umeandika kitu cha maana bado tutaona unafanya ukigeu geu.Mwanaume lazima uwe na msimamo katika maisha sio unakuwa wa uvugu vugu.
Mabandiko ya Mayalla karibu yote nayasoma. Hata mimi kuna wakati nilianza kumuona kama kigeugeu na MTU asiyekuwa na msimamo. Kadri nilivyoendelea kusoma, objectively nikashawishika kwa kiasi kikubwa sana (siyo asilimia 100) kuwa Mayalla independent and objective thinker (zingatia kuwa, kando ya kumuona kwa runinga na kumsoma mitandaoni, simfahamu kabisa huyu mtu).

Sasa basi kama wewe si mvivu wa kusoma article ndefu, ukisoma kwa makini with an objective mind utagundua kwamba kuna watu kama Mayalla wengi tu ambao watasifia pa kusifia na kukosoa pa kukosoa na hiyo ni sahihi kabisa. Kwanini tuwaite vigeugeu?

Upembuzi alioufanya Mayalla leo unapaswa kuungwa mkono na kila aliye timamu bila kujali itikadi za kisiasa.

Kudos, Mayalla!
 
Kuna matatizo ya msingi kadhaa. Nitajaribu kuweka summary in point form.

1.Uongozi bora ni haki ya taifa na haupimwi kwa fedha. This is an intangible.Ndiyo maana hatujawahi kuahirisha uchaguzikwa sababu ya kukosa fedha. Kenya wamerudia uchaguzi wa rais bila kujali gharama.

2. Kukataza mtu kujiuzulu chama ni kumkatalia haki yake ya kuamua mambo yake kisiasa, hii ni haki ya kikatiba.

3. Hata ukiruhusu wagombea binafsi, hilo halitazuia watu kuhama vyama. In fact halitazuia hata wasio na chama kujiuzulu ubunge.

4. Kiongozi anayechaguliwa kwa tiketi ya chama, anachaguliwa kwa tiketi ya chama, si kama mtu binafsi. Kuna watu wengi sana wanapiga kura kwa kuangalia chama kwa matumaini ya kwamba sera za chama hicho zitaongozahuyo mtu,bila kujali mtu ninani. Huu ndio msingi wa habari ya kumtaka mtu anayejiuzulu uanachama, kamaalipata ubunge kwa tiketi ya chama, awe amejiuzulu ubunge hapohapo.

5. Inawezekana kabisa ikawa mtu aruhusiwe kujiuzulu uanachama 9na hivyo ubunge) halafu kama kuna concern za gharama, uchaguzi usifanyike mpaka baadaye,hata uchaguzi mkuu ujao. Hapa Marekani kuna Senator Al Franken wa Minnessota anajiuzulu muda si mrefu ujao. Badala ya kufanya uchaguzi mara moja, gavana wa Minessota anamteua "Liutenant Governor" wa Minnessota aende kuwakilisha jimbo hilo katika Senate.

Hili lina faida kadhaa.
a) Senata anaachiwa haki yake ya kujiuzulu bila matata
b) Wananchi wanapewa haki yao ya kuwa na muwakilishi kwa vile mtu mwingine anateuliwa kuwawakilisha.
c) Nchi haipewi gharama za kufanya uchaguzi mara moja

Kama tumeweza kuwa na wabunge wa kuteuliwa, na tatizo letu ni gharama za uchaguzi, na wananchi walishakikubali chama fulani kutoa mbunge kwa miaka mitano, kwa nini tusikipe chama hicho kilichoshinda uchaguzi nafasi ya kuteua mbunge atakayeshika ubunge huo mpaka uchaguzi mkuu ujao?

Ingawa uongozi mzuri hauna bajeti,naelewa pia nchi yetu haina rasilimali zisizo mwisho, na hivyo naelewa watu wanaoongelea suala la gharama.

Suluhisho hilo hapo juuni compromise katiya kutafuta uongozimzuri kabisa lakini pia kujali kutokuwa na gharamaza ajabu za chaguzi zinazojirudia rudia.
 
Nimesearch hata hao USA waliona independent candidate ni failing way ndiyo maana toka mwaka 1922 hajawahi tokea akashinda huyo mgombea huru rejea

Ni ujinga kuadvocate mgombea huru sababu hakutakua na kitu cha kumcontrol maamuzi yake specially kwa katiba zetu za unga mwana!..
Hutakiwi kulinganisha nchi ambayo mgombea huru anaruhusiwa lakini hafanikiwi, na mgombea huru nchi ambayo haruhusiwi kabisa.
 
Hutakiwi kulinganisha nchi ambayo mgombea huru anaruhusiwa lakini hafanikiwi, na mgombea huru nchi ambayo haruhusiwi kabisa.
Tutengeneze mazingira ya kumbana mgombea huru kabla ya kumruhusu kugombea tu!..
Haruhusiwi sio sababu haruhusiwi tu ni sababu mazingira hayaruhusu!..
 
Mabandiko ya Mayalla karibu yote nayasoma. Hata mimi kuna wakati nilianza kumuona kama kigeugeu na MTU asiyekuwa na msimamo. Kadri nilivyoendelea kusoma, objectively nikashawishika kwa kiasi kikubwa sana (siyo asilimia 100) kuwa Mayalla independent and objective thinker (zingatia kuwa, kando ya kumuona kwa runinga na kumsoma mitandaoni, simfahamu kabisa huyu mtu).

Sasa basi kama wewe si mvivu wa kusoma article ndefu, ukisoma kwa makini with an objective mind utagundua kwamba kuna watu kama Mayalla wengi tu ambao watasifia pa kusifia na kukosoa pa kukosoa na hiyo ni sahihi kabisa. Kwanini tuwaite vigeugeu?

Upembuzi alioufanya Mayalla leo unapaswa kuungwa mkono na kila aliye timamu bila kujali itikadi za kisiasa.

Kudos, Mayalla!
anacho kisema ni kweli ndio maana nilisema hata siku akiandika vitu vya maana vinaweza visiwe na wachangiaji kwa kuwa wengi wanamuona kama kigeu geu,mfano post ya leo ameandika vyema sana ukisoma lakini haina wachangiaji wengi kutokana na mitazamo ya watu juu yake kutokana na huko nyuma alivyokuwa ana present hoja zake
 
Paskali waweza kuwa si mwanachama wa chama chochote lakini unakereketwa na "sera, itikadi na imani " ya chama moja wapo hapa Tz.
Magufuli aliwahi kumwambia huyu jamaa pale ikulu kuwa Mayalla kwa kisukuma maana yake ni njaa. Mimi navyoju Ni Njaa tena nyingi. Unawezaje kupinga katiba na wkat huo unataka rais afuate hiyohiyo katiba ? Wanayo haki ya kuhama
 
Back
Top Bottom