Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Ina maana unataka kusema tupitishe kipengele ambacho kinasema hata Bakhressa/mengi/manji/dewji akiamua anagombea uchguzi wa raisi kama mgombea binafsi?.
Tanzania ni changa sana kwenye suala zima la demokrasia!..labda naomba unipe mfano wa nchi ambayo inafanya huo uchaguzi wa mgombea binafsi!!..
 
Anajifanya anabana matumizi, wakati huohuo nyuma ya pazia anaruhusu wanachama waupinzani kununuliwa.....
Anayofanya kiongozi ni shaghalabaghala....akili mbovu
 
Watu wamepiga hesabu zao kwa kuangalia future zao halafu nyie mnaita upuuzi,mimi naona wapuuzi ni wale ambao waliweka imani na matumaini yao kwa hawa wanasiasa.

Hata hivyo hiyo ndiyo demokrasia.
 
wapinzani wengi wala hawakumuelewa Marehemu Mtikila na Watanzania wengi hawakumuelewa Mtikila na kesi yake ya Mgombea Binafsi,ila CCM na watawala walimuelewa vyema adhma yake ndo maana walitumia kila aina ya hila kuifinyangafinyanga kesi yake.
Marehemu Mchungaji Christopha Mtikila ambaye yeo amelala huko kwenye kaburi lililopo mkoa wa Njombe,wilaya ya Ludewa katika kijiji cha Milo aliliona hili tatizo Mapema mno, lakini yeye alichukua hatua kwa kwenda mahakamani kudai madaraka ya wananchi yarudishwe kwa wananchi kwa kupitia kesi yake ya mgombea binafsi, mara ya kwanza alishinda kesi mara ya pili tena mbele ya marafiki wa mahakama wasomi na manguli kabisa wa sheria wakina prof kabudi ukatolewa uamuzi wa kijinga kabisa na waajabu, yaani chombo ambacho kinahusuka na kutafsiri sheria kikaamua kesi hiyo ipelekwe bungeni..kituko hiki.
kwa mazingira ya sasa hawa wagombea si wawakilishi wa wananchi hawa ni wawakilishi wa vyama vyao,wakati wa uchaguzi wanapelekwa kwa wananchi wakapigiwe kura ila wakishashinda tu hana cha kufanya na mwanachi tena, hawezi kumuogopa mwanachi aliyempa kura kwasababu hawana cha kumfanya mpaka wakati wa uchaguzi tena, ila kinyume chake hawa wanakuwa mali ya chama cha siasa kilichomsimamisha. chama chake kinageuka kuwa ndio mtoa amri kwakwe na ndiyo kinampangia nini cha kufanya na nini asifanya,yaani kwa kifupi ndyiyo kinamdhibiti huyu mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge na raisi wa nchi, mhusika hata akitofautiana na wanachi cheo chake kipo salama kabisa ila siyo kutofautiana na chama chake, sa nyingine wanaweza hata wakawa na ugomvi na mwenyekiti wake au viongozi wake wa chama kwa visa vya kijinga kabisa ambavyo hata havihusiani na wanachi lakini ikawagharimu wanachi kumkosa na kupoteza muda kwa kuingia kwenye uchaguzi kumchagua mtu mwingine. mfano wakati ule wa Zito kabwe wanachi wake bado walikuwa na mahaba naye na bado walikuwa wanataka aendelee kuwa mbunge wao, lakini Zito alikuwa na ugomvi na chama chake, hivyo ugomvi ule ukasababisha Zito apoteze ubunge wake si kwa matakwa ya waliomchagua bali kwa matakwa ya Chama.
hili suala la sheria hii ya uchaguzi linatusumbua sana kiasi kwamba hata wabunge wanashindwa kufanya shughuli zao kwa utashi wao, maamuzi mengi wanayoyafanya bungeni ni maamuzi ya chama, kila ukiona wanaunga mkono jambo fulani basi jua chama chao kimeelekeza iwe hivyo, wabunge wa CCM wamekuwa wahanga sana kwenye hili mpaka imefika wakati hoja zao ambazo zinapingana na msimamo wa chama chao au zinakosoa serikali yao huwa wanawapenyezea wapinzani waziwasilishe, leo hii tunamshangaa Raisi wetu magufuli kuwa mbona anafanya mambo kana kwamba hakuwepo katika bunge, kila jambo anashangaa utafikiri kashushwa leo Tanzania, anafanya maamuzi kwa ukali anakishangaa Chama chake kwa kukumbatia uozo..anazishangaa serikali zilizopita kwa kukumbatioa ufisadi na ufujaji wa mali yauma na usainiji wa mikataba mibovu wakati ye mwenyewe alikuwa ni sehemu ya hizo hizo serikali na alikuwa ni sehemu ya wabunge waliopigia kura ya ndiyo mambo ya hovyo bungeni,HII YOTE NI KWASABABU YA SHERIA HII YA UCHAGUZI.
kwa kweli ifike mahala wananchi tupige kelele ili madaraka yarudishwe kwa wananchi, tuwamiliki hawa viongozi tunaowachagua kwa kura zetu, tumeviachia vyama vya siasa matokeo yake wanatumika kulinda maslahi ya watu fulani ndani ya vyama. leo hii taifa limekubwa na mambo ya kishamba kabisa ya kuhama hama kwa hawa wawakilishi wa uma, tunapoteza rasilimali fedha na tunapoteza rasilimali muda na saa nyingine tunawapoteza hata watu maana wengine hufariki kwa vurugu ya hizi chaguzi ndogo, damu humwagika na wengine hupata ama vilema au makovu ya kudumu kama alivyopata mama Rose kamili kwa kufanyiwa vitu vya ajabu huko Kalenga kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo.
kuongoza si lazima uwe ndani ya chama cha siasa, mwenyekiti wa mtaa anahitaji chama cha nini? Diwani anahitaji chama cha nini? mbunge anahitaji chama cha nini? raisi anahitaji chama cha nini? huu kweli ni mfumo wa kijinga kabisa. Eti tunamchagua raisi wa nchi ili aongozwe na utashi wa chama chake, leo hii tushukuru katiba ya CCM inampa uenyekiti wa chama mtu aliyechaguliwa kuwa raisi lakini hizo kofia kama zingekuwa mbili basi kuna hatari raisi angekuwa anapewa maagizo na mwenyekiti wa chama.
uraisi ni cheo ambacho kinatakiwa kiwe huru, mtu akiwa raisi aunde baraza lake la mawadhili na adhibitiwe na chombo cha wanachi ambacho ni bunge. hizi nafasi za kuchaguliwa basi yoyote mwenye sifa apewe nafasi ya kugombea na anadi sera zake kama mgombea huru na atayeona anataka kwenda kwenye chama basi aende, wengine sisi ni waumini wa ustawi na maendeleo ya jamii zetu ambao tunaona si lazima kupitia chama ili uwatumikie wanachi, vyama vyenyewe hivi havieleweki kwetu tunaona ni upumbavu tu, kwanini watu kama sisi tunabaguliwa na kunyimwa haki yetu ya kupigiwa kura kama hatuko kwenye vyama?...hapana tupaze sauti zetu
Mnyikungu.
 
Leo Shemela umeongea kwa uchungu sana.Sitofautishi sana ulichoongea wewe na alichoongea Upendo Peneza,tofauti iliyokuwepo Peneza amulizwa CV yake baada tu ya kuongea.

Nadhani hata chama kitakachomfukuza Mbunge wake kipigwe fine kubw aili ujinga ujinga huo uachwe mara moja.

Ni kweli tunahitaji Uhuru wa kuchagua na kuchaguliwa kuwa viongozi bila kutokana na chama chochote cha siasa
 
Lakini wakati mwingine lzm nasi wananchi tufikiri vzr mtu anaamua yy mwenyewe binafsi kujiuzuru uanachama kwenye chama chake na ubunge sio kwamba amefukuzwa na chama hlf tena mtu huyo huyo anaenda kugombea kupitia chama kingine.Huu ni ujinga uliopitiliza watunga Sera wetu walione hili walifanyie marekebisho mapema. Maana hizo fedha zinazotumika kwenye uchaguzi mdogo zingeweza kusaidia Huduma za afya,elimu,miundombinu kuliko kupoteza kwenye uchaguzi mdogo ambao mtu kaamua kujiuzuru yy mwenyewe.Nakubaliana kwa namna moja na mapendekezo yako ndg.Pascal, hawa watu wanaojiuzuru wenyewe wasiruhusiwe kabisa kugombea nyadhifa hizo tena.
 
Ina maana unataka kusema tupitishe kipengele ambacho kinasema hata Bakhressa/mengi/manji/dewji akiamua anagombea uchguzi wa raisi kama mgombea binafsi?.
Tanzania ni changa sana kwenye suala zima la demokrasia!..labda naomba unipe mfano wa nchi ambayo inafanya huo uchaguzi wa mgombea binafsi!!..

US wana mgombea binafsi.
 
Pasco Mayala hata ukiwa na hoja nzuri, huwa hauna uwezo wa kutoa hoja. this is too bad for you ikizingatia ni mwanasaheria na mwandishi wa habari. pia kwa umri wako. usituaibishe.
 
Mkuu Paskali nashukuru umeongea lakini ukiwa umechelewa. Watu kama nyie ambao hata hao viongozi wanafahamu kwa sura mnapokaa kimya kwa mambo ya kipumbavu wanaona sawa. Iko siku mtakuja kutoa ushauri watu wakiwa wameuwawa wa kutosha kwa kukaa kimya mpaka. Umetumia lugha nzuri ya ujinga ujinga hii ni lugha inayobeba ukweli bila kuremba. Mimi sasa hivi nasema kushiriki hizi chaguzi za kinyama na kikatili ni upuuzi na ushenzi wa hali ya juu.

Wakati wengine tukihoji wale wapinzani waliokuwa wanahama kwa sababu inayofanana tena wa sehemu na chama fulani mbona mlikaa kimya? Wakapokelewa mbele ya hafla ya kijeshi wakati jeshi na siasa vimetengwa kabisa kikatiba, akina Paskali mlikalia kimya kosa lile la kimaadili kisa anayefanya yale ni mkuu wa nchi. Hivi ni kweli mlikuwa hamuoni kwamba ule ni mchezo wa kipuuzi, umeona wapi watu wanahama pamoja, kwa sababu moja na wakati mwingine barua zikiwa zinafanana maneno na kukosewa majina. Ikasemekana muandishi wa barua ya kujiuzulu ni mmoja ila saini tu ndio za wahusika akina Paskali bado mkawa kimya.

Leo hii tunashindana na watu huku jukwaani kwamba kinachoendelea kwenye hii hamahama ni kutakatisha siasa chafu. Watetezi wa huu upuuzi wanasema tulete ushahidi, yaani wanatuona sisi ni watoto kwamba tunapaswa kuleta EFD receipt ndio iaminike kwamba kuna biashara. Hivi ni nani asiyejua kuna biashara ya ukahaba? Udhibitisho wa biashara hiyo ni receipt ya EFD? Haya basi huo ushenzi wa kuhama chama kwa muwakilishi unafanyika kisha uchaguzi unarudiwa, kwenye chaguzi hizo kuna chama kinaamini kinapendwa kinafanyia wengine ukatili wa kutisha na sheria za uchaguzi zinakiukwa mchana kweupe. Toka lini sheria zeti za uchaguzi zikamtambua Rc na Dc kuratibu upigaji kura? Akina Paskali bado mchezo huu mlikuwa kimya, nalo hili hamkuliona? Kibaya zaidi viongozi wa dini nao wako kimya wanasubiri kuombea nchi amani. Seriously Paskali? Bora umeongea ila ukiwa umechelewa.
 
1. Ile falsasafa ya CHAMA KUSHIKA HATAMU imetuachia madhara mpaka kesho.
2. Kuna watu walipoteza ndugu zao, walihatarisha maisha yao ili fulani ashinde uchaguzi. Miaka miwili baadaye amejivua uongozi. Dhambi mbaya sana!
3. Wazo hili haliwezi kuungwa mkono na kipitishwa na wale 'political middlemen ' kwenye vikao vyao
 
Paskali umeandika vizuri, hakuna sababu ya rais kila siku kuimba juu ya kusimamia vizuri mapato ya serekali huku kukiwa na matumizi ya hovyo na yanayoepukika. Mahospitali hayana dawa, barabara nyingi zina mashimo ya kutisha, lakini tunabebeshwa mzigo wa by election zisizokuwa na kichwa wala miguu. Tuliamriwa siasa zisimame hadi 2020 ili tujikite kwenye shughuli za maendeleo, je hizi by election ndiyo shughuli za maendeleo?
 
Mtikila alikuwa na mapungufu yake lakini kwenye kudai haki sijaona mtu aliyeweza kuziba pengo lake, mimi nimebaki shabiki tangia mfumo wa vyama vingi kwani wanasiasa wote na vyama vyote vinadanganya wanamchi kuwa wanawatetea ukweli wanatetea matumbo yao.Kwanini watu wanashindwa kupigania haki ya mgombea binafsi na hali hukumu ilishatolewa na mahakama ya Afrika.Ukweli wanaogopa kwani mgombea binafsi akiruhusiwa vyama vingi vitakufa au vitabaki majina kwani si wote wanaogombea kupitia vyama hivyo wanavikubali bali ni kutimiza masharti ua tume kuwa mgombea lazima adhaminiwe na vyama ndio maana hakuna anayeona uchungu wa kodi zetu
 
Paskali hongera,hilo neno wenye masikio na wasikie! Huu ujinga ulaleta kichefux2;Aibu yao wajinga wote.Eti kuna watu wanakaa kupanga mikakati ya kijima kupata umaarufu kisiasa!Wapumbafu sana (Kwa sauti ya mzee Nkapa)
 
Mkuu umenena serikali haiwezi ikadai ni watanzania masikini halafu tunaingia kwenye gharama za uchaguzi pasipo sababu yeyote. Demokrasia ya Tanzania imegeuka kuwa usajili wa Manchester United ama Real Madrid.
 
Back
Top Bottom