Sheria ya taa za sportlight kwenye magari

KIBUKUSA

Member
Dec 13, 2013
84
29
Juzi nililazimishwa na askari wa barabarani kufunika taa za ukungu baada ya mabishano ya muda mrefu. Alitaka kunilima notification lakini nikamuwahi kwa hela ya kubrashi viatu.

Sasa kwenye hili jukwaa lazima kutakuwa na mdau wa hili. Hii sheria inahusu taa za mwanga mkali ama hata hizi za rangi zinazotumika kama kuna ukungu. Nauliza kwa vile wenyewe hawa traffic wanatofautiana wengine hawaoni kwamba ni tatizo wengine kama wa jana ameona sehemu ya kupatia chochote. Hii imekaaje?
 
Back
Top Bottom