Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali

Pamoja na kumpenda, kwa hio ashakubari kumpa talaka na kuachana, Suala uliloleta hapa ni Mgawanyo wa mali tuu si ndio?

Hembu iweke hii ieleweke.
Kumpenda ni moja. Ni kuonesha kuwa jamaa bado hayupo willing kumuacha mkewe na hatuwezi kumlazimisha mke abaki kwa jamaa.(mnaelewa mapenzi yalivyo)

Mali ni swala la 2
Ikiwa hatuwezi kumlazimisha mke abaki,na makosa yote yapo kwa mwanamke na mwisho wa siku yeye ndo anataka talaka akiwa na mlengo mkuu wa kumuacha jamaa na wagawane mali.

Swali ni je,mke huyu atakuwa na haki ya kutaka mgawanyo wa mali?

Je hakuna sheria ya kumkinga mume?
 
Hafu unasikia mdada flani humu anapenda sana kuleta nyuzi za vifo vifo anakuja na habari:

"Mume amuua Mke wake kwa kumkata kichwa na Kuwapikia mbwa supu"

Ma keyboard warriors wanaanza popoma kwamba wanaume makatili. Hizi ndoa we sikiaga tu yasikukute.
 
Kumpenda ni moja.
Ni kuonesha kuwa jamaa bado hayupo willing kumuacha mkewe na hatuwezi kumlazimisha mke abaki kwa jamaa.(mnaelewa mapenzi yalivyo)

Mali ni swala la 2...
Mimi kwa hili sina uzoefu..
Ngoja wazoefu waje kwa msaada, Poleni.

Hizi mambo za sheria zinawekwa kwa kusaidia, ila wengine wanatumia kuumiza...

NAOMBA KUULIZA

Kwa mtu kama huyo, kuachana tuu na kutokubali kufanya nae mgawanyo wa hizo mali, Hivi ukigoma kabisa kumpa hio taraka anayodai mwenyewe(tunajua hadai sababu ya manyanyaso au shida yoyote), katika mazingira haya kuna sheria inakubana? na ina nguvu gani..?

Kinyume na hapo Mtu kama huyu, humpi talaka, Kama hataki kuishi na mimi aondoke mwenyewe.

Halafu haya mambo ya..
"..........bado anampenda"
ndio yataleta maafa zaidi baadae
 
Mimi kwa hili sina uzoefu..
Ngoja wazoefu waje kwa msaada, Poleni.

Hizi mambo za sheria zinawekwa kwa kusaidia, ila wengine wanatumia kuumiza...
Hili wazo lilinijia kuwa asimpe talaka.

Na kwa kuongezea hapa,huyo mke anamfata kwa shari mumewe na kumvaa amoe talaka ilimradi mume anyanyue mkono.

Mbaya mume ndo hali sio nzuri anaumwa so hata nguvu hana ila huyo mke anamfata kishari ie kumkunja n.k
 
Kisheria Mke Anayetaka Kupewa Talaka Bado ana Haki ya Kudai Mali Alizochuma akiwa na Mumewe, hata kama Yeye Ndio chanzo cha Tatizo Lililopelekea Kudai Talaka.

Sheria Haimlazimishi Mke Aendelee Kuishi na Mume Asiyemtaka Hata Kama Mume Huyo Bado Anampenda Mke Kwa Dhati. Maadamu Mmoja wao Hataki Tena Kuishi na Mwenza wake, Basi Linapokuja swala la Kugawana mali Kila Mmoja atapata Haki Yake Kulingana Na Walichokichuma Wakiwa Pamoja Katika Ndoa.

******
PAMOJA NA SHERIA KUMLINDA HUYO ANAYEDAI TALAKA LAKINI MKUMBUSHE HUYO MWANAMKE KUWA MUNGU HAELEWI KITU KINACHOITWA TALAKA, NA YEYOTE ANAYEFANYA HAYO ATAANGAMIZWA KATIKA ZIWA LA MOTO SIKU ILE ATAPOTOKA DUNIANI.
 
Wakuu,

Sheria ya ndoa inawataka watu wanaofungu ndoa wasiwe watu wenye uhusiano wa damu, na endapo watu wa namna hiyo wakifunga ndoa basi ndoa hiyo ni batili na haiwezi kuwa halali kisheria.

Usiku Mwema Wakuu
 
Wakuu,

Sheria ya ndoa inawataka watu wanaofungu ndoa wasiwe watu wenye uhusiano wa damu, na endapo watu wa namna hiyo wakifunga ndoa basi ndoa hiyo ni batili na haiwezi kuwa halali kisheria.

Usiku Mwema Wakuu
Sheria inasemaje katika ndoa hizi za kiislamu ambazo zinaruhusu ndoa ya wanandugu wenye uhusiano wa damu katika upande wa binamu au mtoto wa mjomba kuona..? Ipoje hii..
 
Kisheria Mke Anayetaka Kupewa Talaka Bado ana Haki ya Kudai Mali Alizochuma akiwa na Mumewe, hata kama Yeye Ndio chanzo cha Tatizo Lililopelekea Kudai Talaka.

Sheria Haimlazimishi Mke Aendelee Kuishi na Mume Asiyemtaka Hata Kama Mume Huyo Bado Anampenda Mke Kwa Dhati. Maadamu Mmoja wao Hataki Tena Kuishi na Mwenza wake, Basi Linapokuja swala la Kugawana mali Kila Mmoja atapata Haki Yake Kulingana Na Walichokichuma Wakiwa Pamoja Katika Ndoa...

Naomba unifahamishe kama unauelewa na hili.

Nikioa mwanamke kwa ndoa na akanikuta na kampuni yangu ambayo tayari inafanya vizuri, yeye ana ajira yake ya kumuingizia kipato ambacho ni chake binafsi hakihusiki hata kidogo kwenye kuendesha familia, Je nikimpa talaka na yeye atakuwa na haki ya kupewa sehemu ya kampuni yangu kisheria kama mgawanyo Wa Mali?

Swali LA pili ni same scenario sema mwanamke haujamuoa, unaishi nae tu, vipi atapata chochote.
 
Naomba unifahamishe kama unauelewa na hili.

Nikioa mwanamke kwa ndoa na akanikuta na kampuni yangu ambayo tayari inafanya vizuri, yeye ana ajira yake ya kumuingizia kipato ambacho ni chake binafsi hakihusiki hata kidogo kwenye kuendesha familia, Je nikimpa talaka na yeye atakuwa na haki ya kupewa sehemu ya kampuni yangu kisheria kama mgawanyo Wa Mali?

Swali LA pili ni same scenario sema mwanamke haujamuoa, unaishi nae tu, vipi atapata chochote.
Yes. Why not?
 
Wakuu nawasilimu.
Samahani na poleni kwa majukumu, naomba niende kwenye point. Kuna mzee wangu alikuwa na mwanamke aliyeishi naye kinyumba(Kama wapenzi) tangu 2009 bila ya kufunga ndoa (alitoa pesa ya barua tu) na wakadumu kwa muda wa miaka mitano wakiwa pamoja had mwaka 2014 yule mwanamke aliamua kuondoka mwenyew pale nyumbani kwa yule mzee akiwa hajaunda kitu chochote cha kudumu na yule mzee. Maisha yaliendelea na yule mzee akapata ustaafu mwaka 2016 baada ya kustaafu akaoa kisheria kabisa mwanamke mwingine ambye anaishi naye hadi sasa. Shida imetokea mwanzoni mwa mwaka huu yule mwanamke aliyeondoka 2014 ambaye hakumwoa kisheria amefungua kesi kuwa anahitaji huduma au fidia kwa muda aliokuwa anatumika kwake alipwe fidia. Ombi langu kwenu wakuu naomba kujua kifungu kipi kinamruhusu huyu mama kuomba fidia hali ya kuwa hakumwoa kisheria na huyu mzee hakumfukuza na hawakuunda mali yoyote ile na hawajazaa hata mototo mmoja? MSAADA WENU TAFADHALI.
 
Hawezi kudai fidia yoyote kwa kuwa aliondoka mwenyewe na imepita miaka mingi hawakai pamoja presumption of marriage haiwezi kuonekana hapo
 
Back
Top Bottom