Sheria ya Manunuzi yaua ‘upigaji dili’

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria ya Manunuzi wa Mwaka 2016, umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni jana na kuwekwa wazi kwa umma, na moja ya vifungu vinavyopendekezwa ni kuzuia mtu yeyote aliyewahi kuhukumiwa kwa rushwa, kufanya biashara na serikali.

Katika marekebisho hayo yanayopendekezwa na serikali, wizara, taasisi au shirika lolote la serikali wakati wa kufanya biashara na kampuni yoyote, ikibaini kampuni husika au mmoja wa wakurugenzi wake aliwahi kuhukumiwa kwa rushwa, biashara hiyo itasitishwa mara moja na taarifa kutolewa serikalini.

Mbali na watu waliohukumiwa kwa makosa ya rushwa, marekebisho hayo yamependekeza kuwa pamoja na sifa nyingine za viongozi wakuu wa serikali hasa maofisa watendaji wakuu, watapaswa kuwa na sifa ya ziada ya uzoefu katika masuala ya manunuzi.

Katika kukidhi haja ya kuondoa malalamiko ya sheria iliyopo kutumika kuibia nchi, marekebisho hayo yamesisitiza bei za huduma na bidhaa zitakazotolewa ziwe za soko, ununuzi ufanyike moja kwa moja kiwandani badala ya kupitia kwa mtu wa kati na mkataba wa manunuzi, lazima usainiwe mbele ya mashuhuda.

Watuhumiwa wa rushwa

Katika Ibara ya 83 ya Sheria hiyo, imependekezwa ibara ndogo ya pili kwamba shirika au wizara itakaporidhika kwamba kampuni au mtu anayependekezwa kupewa zabuni, amewahi kutangazwa na Mahakama kuwa alishiriki katika vitendo vya rushwa, ufisadi, au ukiukwaji wa taratibu wakati wa kushindania zabuni, ofisi hiyo ya umma itapaswa kukataa pendekezo la kumpa mhusika zabuni hiyo.

Ofisi hiyo ya umma, pia itapaswa kumtangaza mtu huyo au mzabuni ikiwa ni pamoja na wakurugenzi wake, kuwa hawapaswi kupewa zabuni yoyote inayogharimiwa na fedha za umma.

Pia ofisi hiyo ya umma, itapaswa kumtaka huyo mtu au mzabuni, kurejesha sehemu ya fedha aliyopewa kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa au huduma au kuzuia sehemu ya fedha iliyopaswa kwenda kwa mzabuni kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa au huduma.

Mapendekezo hayo yameendelea kuitaka ofisi husika ya umma ndani ya siku saba baada ya kutangaza kuwa mzabuni huyo, hafai kupewa zabuni inayogharimiwa na fedha za umma, kuwasilisha jina la mzabuni na wakurugenzi wake kwa mamlaka inayotajwa na sheria husika.

Mamlaka hiyo nayo imetakiwa na mapendekezo hayo ya sheria, kwamba baada ya kupata taarifa hiyo, kumfungia mtu au mzabuni husika asipate zabuni yoyote inayogharimiwa kwa fedha za umma, kwa muda usiopungua miaka 10.

Sifa za CEO

Katika mapendekezo kwenye Kifungu cha 23 cha Sheria hiyo, Kifungu Kidogo cha II, kimezungumzia uteuzi wa maofisa watendaji wakuu wa ofisi hizo za serikali.

Kifungu hicho kinaeleza kuwa ofisa mtendaji mkuu, atateuliwa kutoka kati ya wataalamu wenye uzoefu wa angalau miaka 10 katika fani za uhandisi, usanifu wa majengo, sheria, menejimenti ya ununuzi na usambazaji na ukadiriaji majengo.

Fani nyingine zilizotajwa ni pamoja na uongozi wa biashara, mipango ya kiuchumi na maendeleo au katika fani nyingine yoyote, lakini awe na uzoefu usio na shaka katika masuala ya ununuzi wa umma.

Bei ya soko

Katika Kifungu cha Tisa cha Sheria hiyo sehemu (o) imeitaka ofisi ya umma, wizara au taasisi ya umma, kila taasisi imetakiwa kuwa na taarifa ya bei ya soko ya bidhaa na huduma inayotumika mara kwa mara na ofisi husika kutoka katika ofisi husika ya umma ili kuhakikisha bei ya bidhaa na huduma zitakazonunuliwa, zinalingana na za soko.

Katika kuhakikisha ofisi za umma zinanunua bidhaa bora kwa bei ya soko, ununuzi wa umma umetakiwa kwa mujibu wa muswada huo, kufanyika kwa kuzingatia uaminifu wa hali ya juu, ushindani, uwajibikaji, kuzingatia kupunguza gharama, ufanisi, uwazi na kupata thamani ya fedha iliyotumika.

Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya kupata thamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoa huduma.

Wawekezaji wa ndani

Mapendekezo ya muswada huo, pia yametaka pale kampuni au taasisi ya umma inapolazimika kufanya ununuzi kutoka nje ya nchi, hasa kama ni suala la ushauri linafanywa na kampuni ya nje ya nchi, ofisi hiyo ya serikali inalazimika kuhakikisha kuna wataalamu wa ndani ya nchi.

Ushiriki huo wa wataalamu na kampuni za ndani katika shughuli za ushauri kutoka nje ya nchi, sheria hiyo imependekeza kuwa, kampuni yoyote ya ushauri ya nje ya nchi, inapoomba kazi katika kazi zinazogharimiwa na fedha za umma, lazima ishirikiane na kampuni, mshauri wa Kitanzania kwa asilimia mpaka 15.

Aidha, kampuni au mshauri huyo wa nje ili apewe zabuni katika shughuli ambazo zinagharimiwa na fedha za umma, kuna kigezo cha kuhakikisha wafanyakazi wa kampuni yake, zaidi ya asilimia 60 ni Watanzania.

Mbali na kuwa na asilimia 60 ya wafanyakazi Watanzania, kampuni husika lazima ieleze kiwango cha bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi, ambazo itazinunua katika utekelezaji wa shughuli zake.

Muswada huo unatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa katika Bunge hili, ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma, ambazo katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wa 2016/2016, asilimia 40 ya trilioni 29.53, imepelekwa katika miradi ya maendeleo.


Chanzo: Habari Leo
 
Ofisi au mtumishi wa serikali atakaye kiuka kifungu chochote cha sheria atahukukiwa vipi na adhabu yake ni ipi?

Lazima hili nalo liwekwe wazi
 
"Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya kupatathamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoahuduma."

Ukisoma hiyo paragrafu kwa makini unabaini kuwa kilichofanyika ni danganya toto, na dili zitaendelea kupigwa kama kawaida!
 
Nina mashaka na kipengere cha kinachomtaka CEO kuwa na elimu ya manunuzi?
 
Sheria hiyo on the surface inaonekana watertight kubana walarushwa namafisadi lakini haikutilia maanani hulka ya watanzania wengi.Ili sheria hii iwe very effective inatakiwa pawepo marekebisho katika utendaji kazi wa BRELA. Mtu anayejifahamu ana doa la rushwa halafu kuna zabuni nono mahali, atafanya ujanja wa kuandikisha kampuni mpya harakaharaka na kuiingiza kwenye uombaji tenda - kitu kama hicho!

Tanzania tumefika mahali pabaya sana.
 
Huu mswada haujaeleweka, mfno wanaposema ofc ya summa itanunua kiwandani, au kwa


mwakilishi Wa Kampuni
au kwa muuzaji Wa jumla
Wanasahau Kuwa wauzaji Wa jumla hawapendi kufanya kazi na serikali kuepuka usumbufu Wa kudai, na hawako tayari kuijopesha serikali, na hawako tayari kuomba tender za hizo taasisi.na sio ofc zote za umma mahali zilipo kuna wauzaji Wa jumla au mwakilishi Wa kampuni, mfn ofc ya umma iko mtwara na inataka computer 2 , je muuzaji Wa jumla au mwakilishi anatoka wapi hapo mtwara ? hii sheria inamapungufu makubwa sana
 
"Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya kupatathamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoahuduma."

Ukisoma hiyo paragrafu kwa makini unabaini kuwa kilichofanyika ni danganya toto, na dili zitaendelea kupigwa kama kawaida!
Yes,hii paragraph ina ukakasi,ni danganya toto
 
Sasa unaposema bei ifanane na Soko nisawa lakani...wakumbuke huduma nyingi za Serikali ni Mkopo sasa kama na Supply Material then nalipwa baada ya Miezi au mwaka nitauzaje bei ya soko...Labda wangesema Bei isiende mbali sana iwe ya mazungumzo kati ya mtoa huduma na muhitaji huduma...nikweli Serikali imepigwa sana kwenye Eneo la Manunuzi lkn kumwambia MTU akukopeshe Mali kwa bei ya soko sidhani kama inafaa Labda nao Serikali wawe watu wa CASH
 
Hapa kinachoudhi kufanya biashara na serikali ni kuchelewesha malipo. Bei inaongezagwa sababu ya kusupply kitu then unakuja kulipwa baada ya miezi 3. Mpaka uwe na mtaji mkubwa sana ili kusubiri uliowauzia wale washibe kwanza ndo wakulipe tena kwa kushinikizwa utoe 10%
 
Hapa kinachoudhi kufanya biashara na serikali ni kuchelewesha malipo. Bei inaongezagwa sababu ya kusupply kitu then unakuja kulipwa baada ya miezi 3. Mpaka uwe na mtaji mkubwa sana ili kusubiri uliowauzia wale washibe kwanza ndo wakulipe tena kwa kushinikizwa utoe 10%
Ndio maana nami nimewashauri wakitaka bei za soko nawao Serikali wawe wa CASH vinginevyo nikutaabishana tu
 
"Ushiriki huo wa wataalamu na kampuni za ndani katika shughuli za ushauri kutoka nje ya nchi, sheria hiyo imependekeza kuwa, kampuni yoyote ya ushauri ya nje ya nchi, inapoomba kazi katika kazi zinazogharimiwa na fedha za umma, lazima ishirikiane na kampuni, mshauri wa Kitanzania kwa asilimia mpaka 15."

Hi wangesema kwa kampuni yeyote ya nje inayokuja fanya biashara na serikali kwenye zile (ICB) - International Competative Bidding, waungane na mtanzania kwa 15% ingekuwa bomba sio kwenye consultancy tu.
 
Ya kawaida sana hii, wajaribu kucheki na NGOs haza za kimataifa zinazo fanya kazi Tanzania wana sheria kari sana za manunuzi, wakizifuata zile basi watakuwa wamemaliza kila kitu
 
Madalali watakufa kifo cha kawaida kabisa.
Laiti kama jambo hili la kunyonga madalali lingeshuka chini hadi kwa wapangaji wa nyumba.
 
Hata hivyo kwa hii sheria itahitaji kwa kila manunuzi wawe na cash money.
Maana unafuu serikali iliyokua ikiupata ni pale supplies walipokua wanatumia pesa zao kufanya manunuzi kisha serikali inawalipa kwa installment.
 
tatizo la nchi yetu sio kutokuwepo kwa sheria bali ni utii wa sheria hasa kwa big bosses
 
Hapa kinachoudhi kufanya biashara na serikali ni kuchelewesha malipo. Bei inaongezagwa sababu ya kusupply kitu then unakuja kulipwa baada ya miezi 3. Mpaka uwe na mtaji mkubwa sana ili kusubiri uliowauzia wale washibe kwanza ndo wakulipe tena kwa kushinikizwa utoe 10%

Point nzuri na muhimu kuweka muda wa kulipa katika sheria kwa mfano USAID ni siku 45 kwa miaka ile kwa hiyo unajua inadvance after 45days baada ya kupeleka invoice, ndio pesa unapata hata kama ni installment payment kuliko kuacha ikielea. wangeongeza na kipande cha kuwabana CEO wakichelewa kulipa wachukuliwe hatua pamoja na kulipa riba manake hii ndio mianya ya figisu figisu. CEO atakayelipa fine kwa kuchelewa kulipa kwa wakati atafute kazi ingine.
 
Nina mashaka na kipengere cha kinachomtaka CEO kuwa na elimu ya manunuzi?

Ili kuitekeleza lazima accounting officer (CEO) awe na elimu kidogo hata kozi ya wiki mbili manake atashindwa kutekeleza sheria.
 
hata itungwe sheria mpya ya manunuzi bila ya sheria mama ya nchi(katiba) kurekebishwa watu wataendelea kupiga dili tu sheria ya manunuzi iliyopo ni nzuri vipengele vichache ndo vinahitaji marekebisho. Swali la kujiuliza ni kina nani wanahusika na wizi kwenye manunuzi jibu ni wakuu wa idara, mawaziri, na makatibu wakuu pamoja na raisi ndo wahusika wakuu bila kuwa na katiba yenye kuwabana viongozi wa umma hata itungwe sheria mpaya kutoka mbinguni wataendelea kuiba tu mikataba mingi ni ya siri na huko ndo wizi unafanyika kirahisi katiba mpya ndo dawa ya kila kitu itatupunguzia kero nyingi, kilio chetu watanzania kiwe katiba mpya ikipatikana kutakua na uwoga wa uongozi wa umma.
 
"Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya kupatathamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoahuduma."

Ukisoma hiyo paragrafu kwa makini unabaini kuwa kilichofanyika ni danganya toto, na dili zitaendelea kupigwa kama kawaida!
Uko sahihi kabisa hapa iko shallow sana na imejikita kwenye service Zaidi mfano ujenzi wa barabara kama bei ya soko inataka km ya lami ijengwe kwa milioni 800 akaja mzabuni akatenda kwa milioni 600 sasa huo ubora utapatikanaje? au huyo muuzaji wa jumla au kiwanda vinauhusiana vipi na ujenzi wa barabara?
 
Back
Top Bottom