Sheria ya Manunuzi yaua ‘upigaji dili’

Sheria ya Manunuzi yaua ‘upigaji dili’

Kuna UOTE="MURUSI, post: 16541678, member: 153125"]Ya kawaida sana hii, wajaribu kucheki na NGOs haza za kimataifa zinazo fanya kazi Tanzania wana sheria kari sana za manunuzi, wakizifuata zile basi watakuwa wamemaliza kila kitu[/QUOTE]
Kuna NGO moja niluhudhuria seminar zao unaambiwa washiriki wote tulilipwa posho zetu kwa M-PESA, hakuna cash payment.
 
Mkuu hizo dead lines zipo na ndio maana unasikia serikali inadaiwa fidia kwa kuchelewa kulipwa, mara nyingi hizi serikali haziwi fair kwa supplier
Mkuu hizo unazosema labda ni kwa ile mikataba mikubwa ya kimataifa, lakini kwa hawa wazabuni wa ndani wanaofanya kazi na hizi Halmashauri hakuna kitu kama hicho, yaani pesa hata ikae miaka 5 unalipwa ile ile
 
Mkuu mimi ni victim, sheria zipo ila watu/wazabuni hawadai kutokana na wahusika kutojua haki za wazabuni, mzabuni ukidai au kuwaandikia barua ya kudai watakupiga mkwara kuwa ukiendelea kudai tutakublack list hapa kwetu usipate kazi. Serikali na kandamizi sana kwa suppliers na nadhani hiyo yaweza kuwa sababu ya kusupply substandard service kama ule usemi " Aliyetoa dhahabu bandia alilipwa fedha bandia". Swala la muhimu ni kurudisha maadili kutoka kwa kitengo cha manunuzi na wasimamizi kwa ujumla.
 
Sheria hiyo on the surface inaonekana watertight kubana walarushwa namafisadi lakini haikutilia maanani hulka ya watanzania wengi.Ili sheria hii iwe very effective inatakiwa pawepo marekebisho katika utendaji kazi wa BRELA. Mtu anayejifahamu ana doa la rushwa halafu kuna zabuni nono mahali, atafanya ujanja wa kuandikisha kampuni mpya harakaharaka na kuiingiza kwenye uombaji tenda - kitu kama hicho!

Tanzania tumefika mahali pabaya sana.
..kuongezea, watu wapo tayari kutoa rushwa pia mahakamani ili ashinde kesi, au kukata rufaa ili asafishwa na mahakama kuwa hukumu ilikosewa. Nawashangaa sana wanaombeza Dr. Magufuli. Hii nchi iko njia panda sana, na bila Magufuli nadhani in 5 years tulikuwa tunawapita Mexico (mexico ni rushwa kila kitu, mpaka wapiga kura wanapewa tv au kitu chochote ili wampigie kura mgombea dhaifu, watu wa madawa ya kulevya, gangs wanafadhili wanasiasa, na wao ndiyo wanaamua inchi iendeshweje) na hali hii ilikuwa imetua bongo, maana kipindi fulani Said mwema aliwahi kusema eti mafisadi wa EPA wananguvu zaidi kuzidi serikali, na after those 10 years wauza madawa ya kulevya, mafisadi walikuwa wameshikilia nchi, na wananchi nao hawakuwa nyuma kuchukua rushwa ili wampigie mtu kura.
 
Hawamu = awamu
hacheni = achene
Kalili = kariri

Tukiachana na hayo makosa tuje kwenye hoja yako. Kwani watu wanamkosOa Rais au wanahoji ili kuboresha kusudi iwe makini?
Achene = Acheni
 
..kuongezea, watu wapo tayari kutoa rushwa pia mahakamani ili ashinde kesi, au kukata rufaa ili asafishwa na mahakama kuwa hukumu ilikosewa. Nawashangaa sana wanaombeza Dr. Magufuli. Hii nchi iko njia panda sana, na bila Magufuli nadhani in 5 years tulikuwa tunawapita Mexico (mexico ni rushwa kila kitu, mpaka wapiga kura wanapewa tv au kitu chochote ili wampigie kura mgombea dhaifu, watu wa madawa ya kulevya, gangs wanafadhili wanasiasa, na wao ndiyo wanaamua inchi iendeshweje) na hali hii ilikuwa imetua bongo, maana kipindi fulani Said mwema aliwahi kusema eti mafisadi wa EPA wananguvu zaidi kuzidi serikali, na after those 10 years wauza madawa ya kulevya, mafisadi walikuwa wameshikilia nchi, na wananchi nao hawakuwa nyuma kuchukua rushwa ili wampigie mtu kura.
Umesahau na hapa kwetu wanapewa kofia, Tshirts na pombe?
 
Umesahau na hapa kwetu wanapewa kofia, Tshirts na pombe?
Hahaha, shabiki wa chadema utamjua tu. Kibaya zaidi chadema wanatoa T-shirt, viroba, kofia na wanakusanya michango kwenye kapu kuubwaa
 
Hahaha, shabiki wa chadema utamjua tu. Kibaya zaidi chadema wanatoa T-shirt, viroba, kofia na wanakusanya michango kwenye kapu kuubwaa
hahaha tofauti ni vitu vinavyotolewa tu ila wote wanatoa au? ila sina uhakika wa hao uliowataja
 
Katika kukidhi haja ya kuondoa malalamiko ya sheria iliyopo kutumika kuibia nchi, marekebisho hayo yamesisitiza bei za huduma na bidhaa zitakazotolewa ziwe za soko, ununuzi ufanyike moja kwa moja kiwandani badala ya kupitia kwa mtu wa kati na mkataba wa manunuzi, lazima usainiwe mbele ya mashuhuda.

Hapa pana shida kidogo mbona kama aya hizi zinapingana au mimi ndie niliyeshindwa kuelewa ,naona watu wa kati juu wanakatazwa huku chini wanakubaliwa, which is which?

(Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma, ofisi husika kwa nia ya kupata thamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoa huduma.)
Kwahiyo hawataki mtu wa kati, yaani kwa mfano mimi nanunua bidhaa kutoka China ambazo hazitengenezwi nchini kama Electronics hawataniruhusu kuwa supplier wao sababu tu sina kiwanda?? Au kwamfano hizi tenda za stationeries mpaka huko mawilayani atakuwa anasambaza MASUMIN peke yake?? Kama ndivyo basi tujiandae na pengo la umaskini kuongezeka..
 
Ndo maana umewekwa wazi ili tuweke mawazo yetu pamoja
Doubt yangu, hawa maCEO wa sasa wengi wao hawana skills za manunuzi, na wahakuwa wajumbe wa bodi za manunuzi/tender kazi yao ilikuwa kusaini tu, je watatakiwa kusoma kwanza?

Aidha, kwa sasa inatakiwa soma la manunuzi "walau basics za manunuzi" viingizwe kwenye mitaala katika masomo ya vyuo vikuu.
 
Sheria hiyo on the surface inaonekana watertight kubana walarushwa namafisadi lakini haikutilia maanani hulka ya watanzania wengi.Ili sheria hii iwe very effective inatakiwa pawepo marekebisho katika utendaji kazi wa BRELA. Mtu anayejifahamu ana doa la rushwa halafu kuna zabuni nono mahali, atafanya ujanja wa kuandikisha kampuni mpya harakaharaka na kuiingiza kwenye uombaji tenda - kitu kama hicho!

Tanzania tumefika mahali pabaya sana.

Sio rahisi kihivo labda kuwepo rushwa kwani kwenye evaluation masala ya supplier appraisal yanatiliwa mkazo experience, previous financial perfomance about 3to5yrs nk...
 
imebana nini?..Nilikua naisubilia hii coz asilimia 70+ ya shughuli za selikal ni manunuzi....still kuna mianya tu ya sheria hii maana hapo kikubwa naona neno rushwa wakati sheria yenyewe ni rushwa...Mfano

1. Procurement of used items, haijasemwa used item inapaswa iwe katika hali gani in term of making, year, condition yake etc,,ndo maana yale mabehewa, kivuko kigoma kule if not mistaken tulipigwa na hakuna angle ya kumshika mtuhumiwa.

2. Misuse of forced account method of procurement, hapa napo sheria yetu haijabainisha qualifications za mpewa zabuni, ndo maana madaja etc ni mabovu, anachukuliwa low profile individual anapewa kidogo na anjenga upuuz mpunga mwingine unapigwa.

na mengine pia...
 
Kuna Muhindi alikua ana Supply matairi kwenye taasisi moja hiv ua Serikali akishindwa kabisa akaona ni ujinga. Njoo kesho mara haina mafungu subiri tupate fungu la kukulipa. Matokeo yake anakuja kuandikiwa cheque baada ya miezi 4.

Pia kuna sehem nyingine wata shindwa kuagiza nje kuna mawakala wao wapo nchini na wao ni cash to hand no mkopo. Hiyo sheria bado kidogo kwakweli
 
MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA MANUNUZI YA UMMA.

Step nzuri.

MUSWADA wa Marekebisho ya Sheria ya Manunuzi wa Mwaka 2016, umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni jana na kuwekwa wazi kwa umma, na moja ya vifungu vinavyopendekezwa ni kuzuia mtu yeyote aliyewahi kuhukumiwa kwa rushwa, kufanya biashara na serikali.

Katika marekebisho hayo yanayopendekezwa na serikali, wizara, taasisi au shirika lolote la serikali wakati wa kufanya biashara na kampuni yoyote, ikibaini kampuni husika au mmoja wa wakurugenzi wake aliwahi kuhukumiwa kwa rushwa, biashara hiyo itasitishwa mara moja na taarifa kutolewa serikalini.

Mbali na watu waliohukumiwa kwa makosa ya rushwa, marekebisho hayo yamependekeza kuwa pamoja na sifa nyingine za viongozi wakuu wa serikali hasa maofisa watendaji wakuu, watapaswa kuwa na sifa ya ziada ya uzoefu katika masuala ya manunuzi.

Katika kukidhi haja ya kuondoa malalamiko ya sheria iliyopo kutumika kuibia nchi, marekebisho hayo yamesisitiza bei za huduma na bidhaa zitakazotolewa ziwe za soko, ununuzi ufanyike moja kwa moja kiwandani badala ya kupitia kwa mtu wa kati na mkataba wa manunuzi, lazima usainiwe mbele ya mashuhuda.

WATUHUMIWA WA RUSHWA

Katika Ibara ya 83 ya Sheria hiyo, imependekezwa ibara ndogo ya pili kwamba shirika au wizara itakaporidhika kwamba kampuni au mtu anayependekezwa kupewa zabuni, amewahi kutangazwa na Mahakama kuwa alishiriki katika vitendo vya rushwa, ufisadi, au ukiukwaji wa taratibu wakati wa kushindania zabuni. Ofisi hiyo ya umma itapaswa kukataa pendekezo la kumpa mhusika zabuni hiyo.

Ofisi hiyo ya umma, pia itapaswa kumtangaza mtu huyo au mzabuni ikiwa ni pamoja na wakurugenzi wake, kuwa hawapaswi kupewa zabuni yoyote inayogharimiwa na fedha za umma.

Pia ofisi hiyo ya umma, itapaswa kumtaka huyo mtu au mzabuni, kurejesha sehemu ya fedha aliyopewa kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa au huduma au kuzuia sehemu ya fedha iliyopaswa kwenda kwa mzabuni kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa au huduma.

Pamoja na hayo hapo juu, ofisi husika ya umma ndani ya siku saba baada ya kutangaza kuwa mzabuni huyo hafai kupewa zabuni inayogharimiwa na fedha za umma, itapaswa kuwasilisha jina la mzabuni na wakurugenzi wake kwa mamlaka inayotajwa na sheria husika.

Mamlaka hiyo nayo imetakiwa na mapendekezo hayo ya sheria, kwamba baada ya kupata taarifa hiyo, kumfungia mtu au mzabuni husika asipate zabuni yoyote inayogharimiwa kwa fedha za umma, kwa muda usiopungua miaka 10.

SIFA ZA CEO

Katika mapendekezo kwenye Kifungu cha 23 cha Sheria hiyo, Kifungu Kidogo cha II, kimezungumzia uteuzi wa maofisa watendaji wakuu wa ofisi hizo za serikali.

Kifungu hicho kinaeleza kuwa ofisa mtendaji mkuu, atateuliwa kutoka kati ya wataalamu wenye uzoefu wa angalau miaka 10 katika fani za uhandisi, usanifu wa majengo, sheria, menejimenti ya ununuzi na usambazaji na ukadiriaji majengo.

Fani nyingine zilizotajwa ni pamoja na uongozi wa biashara, mipango ya kiuchumi na maendeleo au katika fani nyingine yoyote, lakini awe na uzoefu usio na shaka katika masuala ya ununuzi wa umma.

BEI YA SOKO

Katika Kifungu cha Tisa cha Sheria hiyo imeitaka ofisi ya umma, wizara au taasisi ya umma kuwa na taarifa ya bei ya soko ya bidhaa na huduma inayotumika mara kwa mara na ofisi husika kutoka katika ofisi husika ya umma ili kuhakikisha bei ya bidhaa na huduma zitakazonunuliwa, zinalingana na za soko.

Katika kuhakikisha ofisi za umma zinanunua bidhaa bora kwa bei ya soko, ununuzi wa umma umetakiwa kwa mujibu wa muswada huo, kufanyika kwa kuzingatia uaminifu wa hali ya juu, ushindani, uwajibikaji, kuzingatia kupunguza gharama, ufanisi, uwazi na kupata thamani ya fedha iliyotumika.

Aidha, ili kupata bei iliyo chini ya soko bila kuathiri ubora wa bidhaa au huduma. Ofisi husika kwa nia ya kupata thamani ya fedha na ubora wa juu, imetakiwa kufanya ununuzi wa bidhaa na huduma mahususi moja kwa moja kutoka kwa mtengenezaji, au kiwandani, mwakilishi wa mtengenezaji au wa kiwanda, muuzaji wa jumla au mtoa huduma.

WAWEKEZAJI WA NDANI

Mapendekezo ya muswada huo, pia yametaka pale kampuni au taasisi ya umma inapolazimika kufanya ununuzi kutoka nje ya nchi hasa kama ni suala la ushauri linafanywa na kampuni ya nje ya nchi. Ofisi hiyo ya serikali inalazimika kuhakikisha kuna wataalamu wa ndani ya nchi.

Ushiriki huo wa wataalamu na kampuni za ndani katika shughuli za ushauri kutoka nje ya nchi. Sheria hiyo imependekeza kuwa, kampuni yoyote ya ushauri ya nje ya nchi, inapoomba kazi katika kazi zinazogharimiwa na fedha za umma lazima ishirikiane na kampuni, mshauri wa Kitanzania kwa asilimia mpaka 15.

Aidha, kampuni au mshauri huyo wa nje ili apewe zabuni katika shughuli ambazo zinagharimiwa na fedha za umma kuna kigezo cha kuhakikisha wafanyakazi wa kampuni yake zaidi ya asilimia 60 ni Watanzania.

Mbali na kuwa na asilimia 60 ya wafanyakazi Watanzania kampuni husika lazima ieleze kiwango cha bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi, ambazo itazinunua katika utekelezaji wa shughuli zake.

Muswada huo unatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa katika Bunge hili ili kuzuia matumizi mabaya ya fedha za umma . Katika bajeti ya 2016/17 40% ya trilioni 29.53, imepelekwa katika miradi ya maendeleo.

Nini maoni yako katika marekebisho hayo?
 
Serikli imependekeza bei za sokoni ziendane na soko badala ya bei elekezi. Serikali yataka ununuzi serikalini uendane na bei ya sokoendekezo hili ni miongoni mwa mapendekezo sita katika maboresho ya sheria ya manunuzi sura 410, yanayolenga kuongeza ufanisi katika manunuzi ya Umma.
 
SERIKLI IMEPENDEKEZA BEI ZA SOKONI ZIENDANE NA SOKO BADALA YA BEI ELEKEZI
Serikali yataka ununuzi serikalini uendane na bei ya sokoENDEKEZO HILI NI MIONGONI MWA MAPENDEKEZO SITA KATIKA MABORESHO YA SHERIA YA MANUNUZI SURA 410, YANAYOLENGA KUONGEZA UFANISI KATIKA MANUNUZI YA UMMA,
Fafanua kidogo hii ni taaluma (ya manunuzi) wengine hatujui. Tafadhali
 
hili nalo litakuwa jipya! watakuwa wanatangaxa tenda au watakua wanaenda kariakoo wenyewe?

nchi hii haiishi vituko!
 
Fafanua kidogo hii ni taaluma (ya manunuzi) wengine hatujui. Tafadhali
Mkuu, ni kazi rahisi tu. Kalamu ya kuandikia inaweza kuuzwa Shs mia tano mitaani. Lakini utakuta kwenye manunuzi ya serikali bei yake ni Shs elfu mbili!
 
Back
Top Bottom