Sheria ya kutoa notice kwa mpangaji wa nyumba inasemaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya kutoa notice kwa mpangaji wa nyumba inasemaje?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MZALAMO, Jul 10, 2011.

 1. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #1
  Jul 10, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Wana JF naomba mnifahamishe kuhusu sheria ya upangaji kama mpangaji anataka kuhama. Je anatakiwa amjulishe mwenye nyumba muda gani kabla ya kuhama? Au mwenye nyumba akitaka kuchukua nyumba yake anatakiwe ampe mpangaji notice ya muda gani kabla ya mkataba kuisha?
   
 2. mbasajohn

  mbasajohn JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kwa mujb wa sheria ya ardhi ambayo ria inaongelea mambo ya lease, notice ya weza kuwa ya mda wowote kulingana na mda wa pango husika yaan monthly au weekly au yearly au zaid na kulingana na mkataba wa pango husika.
  Kama hakuna mkataba au mkataba haujatoa mda wa notice muda wa siku thelathin mara nying hutumika lakn kulingana na urefu wa muda pango kama nilivyoonyesha hapo juu.
  Lakn ikumbukwe kuwa ukikatsha mkataba pasipo sababu za msing pamoja na notice utatakiwa kulipa fidia isipokuwa tu pale ambapo mkataba umetoa uhuru wa kukatsha mkataba wakat wowote kwa sababu yeyote ile.
   
 3. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #3
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako.
   
 4. M

  MZALAMO JF-Expert Member

  #4
  Jul 19, 2011
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 471
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 60
  Nashukuru mkuu kwa maelezo.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa kuongezea hapo. Suala la kuvunja mkataba au kuongeza mkataba huwa linakuwa linabainishwa katika Mkataba wa kupangisha nyumba. Mara nyingi sana taarifa inatakiwa itolewe kwa mpangaji au mpangishaji kama utasitisha mkataba au utaongeza mkataba miezi mitatu kabla kumalizika kwa mkataba.

  Hicho ni kipengele muhimu sana katika mkataba
   
 6. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2013
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ni ndani ya masaa 24 awe amehama lakini mwenye nyumba atatakiwa kumlipa mpangaji wake kodo ya miezi mitatu au kulingana na mkataba wa mwenye nyumba
   
 7. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2013
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  Suala la mpangaji na mwenye nyumba(landlord and tenant) linaongozwa na sheria mbili, ya kwanza ni sheria ya ardhi namba nne ya mwaka 1999, na sheria ya mikataba (law of contract). Kimsingi sheria ya ardhi upande wa upangaji imeweka minimum or principle issues ambazo zitaongoza suala lolote linalohusu upangaji katika mainland tanzania. Hivyo, hata kama mmeingia kwenye mkataba na ukawa na mapungufu, sheria ya ardhi upande wa lease huyajazia mapungufu hayo. Hivyo basi, kwa suala tajwa hapo juu, kama mkataba wenu haukuongelea notisi, kwa mujibu wa sheria, notisi ni siku 30, japo kwa sasa sikumbuki kifungu halisi. Hata hivyo, kama nlivyosema,suala la upangaji pia linaongozwa na sheria ya mkataba ndio maana wahusika husaini MKATABA WA UPANGAJI. Ni nini maana yake? Maana yake wahusika kwa kutumia sheria ya mkataba wanaweza kuweka vipengele vyao vya kuwaongoza na vipengele hivyo vinakuwa na nguvu baina yao. Kwa mfano, kama eneo ni la biashara, haiwezekani kutoa notisi ya siku thelasini kwa kuwa mpangaji lazima apewe muda wa kutafuta eneo la kibiashara kama analohama. Kama mpangaji alikodishwa eneo la hoteli ghorofa tano, lazima ajikinge dhidi ya notisi fupifupi kwa kuweka kipengele katika mkataba. Hivyo ni muhimu sana kutafakari kila kipengele kwa kina na kwa kuangalia mbele. Lastly, kwa wapangaji na wenye nyumba, .notisi inatolewa ndani ya muda wa mkataba, mfano kama mkataba unasema notisi ni mwezi mmoja, .notisi hiyo itolewe kabla mkataba haujaisha, si baada ya mkataba kuisha kwa kuwa utamruhusu mpangaji kukaa bure one more month after the expiry of the contract
   
 8. U

  Upiversity JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2016
  Joined: Jun 19, 2015
  Messages: 3,389
  Likes Received: 2,009
  Trophy Points: 280
  .....mkuu naomba nisaidie nini cha kufanya kwenye hizi cases mbili:
  ..mosi.,mpangaji aliemaliza mkataba wake na akaomba na kulipia mwezi mmoja ili ahame;mwezi umeisha ila hapokei simu wala kujibu meseji na kuhama hajahama!
  ...pili,mpangaji mkataba wake umeisha ila anapiga kalenda kwa zaidi ya mwezi na nusu kulipa tena ili kuingia mkataba mpya.
  .natanguliza shukrani
   
 9. GOKILI

  GOKILI JF-Expert Member

  #9
  Dec 17, 2016
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Kuna mpangaji ambae mwenye nyumba anataka kumtoa katika nyumba yake kutokana na sababu zifuatazo;1.Halipi kodi ya pango ya kila mwezi katika muda uliopangwa.2.Hana maelewano mazuri na wapangaji wenzeka na mwenye nyumba .Na katika mkataba wa kupanga imeelezwa mpangaji atakapokiuka mojawapo mwenyenyumba ana haki ya kumpa notisi ya kuhama.Swali langu jee ni sawa kumpa notisi ya mwezi mmoja ili kuhama mpangaji huyo?na jee atalipa kodi ya mwezi anaotumikia notisi au hapana?
   
 10. merengo90

  merengo90 JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2016
  Joined: Nov 5, 2013
  Messages: 6,465
  Likes Received: 2,251
  Trophy Points: 280
  Notisi ikitolewa ndani ya mkataba maana yake ile pesa bado inatumika, ila kama ikitolewa wakati mkataba umeisha basi mhusika atakaaa bure mwezi wote, so watu huwa wanatoa notisi wakati mkataba bado upo valid
   
 11. GOKILI

  GOKILI JF-Expert Member

  #11
  Dec 20, 2016
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 422
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Asante mkuu.
   
Loading...