Nzwangendaba
JF-Expert Member
- Nov 9, 2019
- 501
- 710
Amani iwe kwenu wana JF
Kutokana na kile kinachoendelea kwa sasa almost kila kona ya nchi juu ya suala la uwekezaji ktk bandari zetu, Binafsi nimepata swali la kujiuliza na pengine tusaidiane kulidodosa;
Je katika uandishi wa draft hiyo ya Mkataba (IGA) ni nani aliyeshiriki kuandika mkataba huo in the first place na kisha kumkaribisha mwenzie kuusaini? Je kulikuwa na timu za watu toka pande zote (Dubai na Tanzania) ambao walikaa mahali wakauandika kwa pamoja kifungu kwa kifungu mwanzo mwisho ama ni upande mmoja tu ndio uliandika kisha mwengine akapewa ausome na kuusaini?
Kama ni timu sawia za watu ziliundwa kuudraft, je kwa upande wa Tz ni akina nani walituwakilisha ktk uandishi wa vifungu hivyo?
Kiujumla, DPW ni mpangaji na Tz ndio mwenye mali. Katika misingi tuliyoizoea ya upangishaji, mwenye mali ndio anayeandika mkataba na kuset masharti ya upangishaji anayoyataka mpangaji ayafuate.
Mnufaika mkubwa ktk suala la upangishaji ama ukodishaji anategemewa kuwa mwenye mali. Mfano, Mwenye nyumba anaandaa mkataba wa upangishaji na mpangaji ndio anapaswa kusoma masharti ya upangaji ili ajipime kama anaweza kuishi kwa kufuata masharti hayo, wala sio mpangaji aje na masharti yake mkononi ili mwenye nyumba asaini na kukubali. (Suala la nyumba hapa limetumika kama mfano tu).
Najua kuna wakati wa kukaa mezani kuweka sawa baadhi ya masharti ambayo yanaweza mbana mmoja wapo ili kuwe na win-win lakini awali ya yote mwenye mali ndio anaweka vigezo vikuu vya mtu kutaka kuja kuwekeza ktk mali yake hiyo.
Mara nyingi aliyepata fursa ya kuandika ama dominate mchakato huo ndiye hujiwekea vifungu vya kumnufaisha zaidi.
Nauliza haya kwa sababu malalamiko juu ya vifungu yanaletwa kila uchwao, tena wanaoleta ukosoaji wa vifungu ni wasomi wakubwa na kuonesha kuwa ni ukiukwaji wa sheria, katiba na kutoonekana kwa moja kwa moja kwa maslahi mapana kwetu kutokana na mkataba huo wa uwekezaji. Sisi wengine tunapenda kujifunza kutoka kwenye chanzo cha haya yote.
Sasa naomba wajuzi wa mambo watujuze, utaratibu kwenye huu mkataba ulikuwaje? Tunaweza wajua wenzetu waliotuwakilisha kwenye uandishi wa vifungu vya mkataba huu ili pengine tuje tuwahoji walikusudia nn? Huenda mawazo yao yalikuwa mazuri na plan nzr huko mbele ambazo hazijawekwa wazi bado. Au kwenye hili mwenye nyumba kaletewa masharti na mpangaji?
Wasalam!