Sheria ndani ya dini ya Kikristo (Mahakama)

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi.kama zipo mnaweza kuziorodhesha mbili tatu hapa,ili tupate muongozo au ufunuo.Na je hapa duniani ipo mahakama yeyote ya kikiristo.

Naona kuna msukumo wa kujadili kisiasa ndani maamuzi ya dini ya kiislamu kutaka iwepo mahakama ya kadhi ,je na wenzetu ndugu zetu wa karibu kabisa wa dini ya kikristu ,nao iwapo wanazo sheria wanaweza kuanzisha mahakama ambayo itaweza kushughulikia misingi ya sheria za dini yao.
Naomba kuwakilisha hoja na natanguliza samahani ikiwa itaonekana nimemgusa mtu.
 
Naulizia tu ,je ndani ya dini ya kikristo zimo sheria ,mfano sheria za kumhukumu mwizi endapo atakamatwa,sheria za mwanamke iwapo atazini au ataonekana sio bikira siku ya mwanzo ya kukutana na mumewe ikiwa hajawahipo kuolewa,sheria za mavazi kwa wanawake na hata waume ,sheria zinazohusiana na urithi....
Hawana utaratibu wa kuingilia uhuru wa waumini wake kanisa halina mahakama hiyo ni kazi ya serikali
 
Nime google nikakumbana nazo ntaziweka kidogo-kidogo ili zifahamike au zifafanuliwe na wajuzi:

Don't let cattle graze with other kinds of Cattle (Leviticus 19:19)
 
Msingi wa sheria za nchi za mgaharibi,
ni biblia.
Kuna mambo mengi yaliyo ongezwa,
kutokana na maendeleo ya Science na Teknolojia,

Elimu aliyo itoa Yesu hatujaitumia hata robo,
tukiwa na dispute tunakwenda kwa Kaisari,
Mahakama za kikristo za nini?

Tunampa Kaisari vilivyo vyake na Mungu tunampa vilivyo vyake.
 
Kadhi courts are special for brain dead idiot religion.

Nia yangu si kukusaidia wewe kuonyesha tabia na malezi yako hapa, suali lipo wazi na wala hakuna dini nilioitukana au kuita wajinga ,hivyo kuwa mstaarabu ,ungeliweza kujibu kirahisi sana kama huna unalolifahamu ndani yake ,tatizo inaonyesha ni wale wacheza hakunaga ,huna elimu inayoweza kukusaidia ,basi upo upo tu.samahani sana .
 
Nime google nikakumbana nazo ntaziweka kidogo-kidogo ili zifahamike au zifafanuliwe na wajuzi:

Don't let cattle graze with other kinds of Cattle (Leviticus 19:19)

Ungetumia bible ya kiswahili iliyopo onlene ningefarijika sana.
 
Mwenye ruhusa ya kumhukumu mwanadamu ni Mwenyez MUNGU pekee,kwanini utake kumhukumu mtu kwa uzinzi wake mwenyewe.mwachie yeye na Mungu wake maana hakuna aliyekamilika
 
Mwiba mambo ya dini peleka jukwaa la dini, mods please hii thread wapelekeeni wapenda dini zao kwenye jukwaa lao la dini.
 
Last edited by a moderator:
Msingi wa sheria za nchi za mgaharibi,
ni biblia.
Kuna mambo mengi yaliyo ongezwa,
kutokana na maendeleo ya Science na Teknolojia,

Elimu aliyo itoa Yesu hatujaitumia hata robo,
tukiwa na dispute tunakwenda kwa Kaisari,
Mahakama za kikristo za nini?

Tunampa Kaisari vilivyo vyake na Mungu tunampa vilivyo vyake.
Kaisari ni nani ? Hili jina nimekuwa nikilisia sana ,,vya kaisari tumuachie kaisari ,something like that ,ila chimbuko lake bado sijalijua .

unasema sheria zipo nyingi sana au elimu aliioitoa Yesu haijatumiwa hata robo,unajua sijaona hizo sheria ndio nikaulizia ,na sikutaka kujua zote bali hizo au kwa hayo mambo niliyoyaainisha hapo mwanzo ,kuwepo kwa sheria ni kwa ajili ya kutumika katika maamuzi ,kuna wale wanaokwenda kutubia kanisani ,ambapo niliona katika filamu juzi inayoonyweshwa ITV..The woman with a steel heart kama sikosei hilo jina na hili la mkenya wa Ulimboka, bila ya shaka ni sheria ndio inatumika kumkubali anaetubu.

Ila mambo niliyoyahitaji nilikuwa na hamu nayo kuyajua.
 
Kazi kwelikweli...Ndiyo maana wengine tunasema hata kama ni Dini basi mjaribu kwenda na wakati. Kuna sehemu imeandikwa na mwanaume naye lazima awe bikira au ni wanawake tu? Mbona wanawake wanakandamizwa sana kwenye mfumo wenu? Hebu niambie, utajuaje mwanamke ni bikira mara ya kwanza ukifinya naye tendo la ndoa? Najua utasema ni lazima anatoke damu kidogo anapopoteza ubikra wake. Lakini ubikira maana yake ni mara ya kwanza kuanza kufanya kile kitendo. Wasichana wengine wanapoteza ubikira hata kwenye michezo na wengine wamezaliwa bila hata ya kuwa na hymen.
Lijitu linaweza kuoa halafu likampa talaka mke wake mpya kwa sababu siyo bikira kumbe ni bikira kweli.
Hii kitu imewafanya dada zenu wengi kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile kuilinda hiyo bikira.
Badilikeni bana!
 
Nime google nikakumbana nazo ntaziweka kidogo-kidogo ili zifahamike au zifafanuliwe na wajuzi:

Don't let cattle graze with other kinds of Cattle (Leviticus 19:19)

Mambo ya Walawi 19:19
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.
 
Na asie na dhambi awe wa kwanza kumtupia jiwe.....

mkuu naona unatuwacha ! Nani atupiwe jiwe kwa kosa gani ? Usione shida kumwaga ukweli ni dhahiri kuwa unajua mengi lakini unabania.
 
Mambo ya Walawi 19:27
Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
 
God wanted Israelite to maintain the best breed of animals they had.
My be because from the breed they were get more milk an meat.
crossing with the breed they dont know might have degenerated the best breeds of their animals.
Hapa si mahali pake thought.

Mambo ya Walawi 19:19
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.
 
Mambo ya Walawi 19:19
Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.

Mkuu Zomba habari za kuamka? Samahani unaweza kunifafanulia maana ya huo msitari uliokuja nao?
 
Back
Top Bottom