Sheria Mkononi!

Nimeshakutana na vibaka ktk anga zao mara kibao lakini sijawahi hata kufikiria kuchukua jiwe na kumrushia kibaka.
Hii biashara ya kushabikia MAUAJI itatupeleka pabaya WATANZANIA. siyo ufahari kuua vibaka. kuna mzembe fulani (inawezekana unahusika) nyuma ya meza ofisini anakwapua kwa maandishi fweza za kusomeshea vijana halafu anasahau tatizo la mbeleni la vibaka watakaojitokeza baada ya kuwa jobless na hopless

je huyu ana tofauti gani na wale walioiba fwedha za Richmond, anatofauti gani na wale wa EPA, anatofauti gani na mtu anayechukua safari imprest halafu haendi safari anatofauti gani na anyeingia mkataba hewa wa kujenga barabara.

Wote tuko sawa ila maskini huyu atapigwa mpaka kufa lakini wale wa mahela mengi hawaishi kusifiwa mpaka maredioni.

Tumelogwa!!!!!!!!
 
Jamani kama simu au sufuria la ugali unaua mtu. Hebu tujiulize anayeibiwa ni mmoja lakini mwizi anauwawa je, wanaoibia watu millioni 40 mbona wanaachwa wakishangilia?
 
hujakutana na wezi wewe unaongea tu mimi nimeshaibiwa gari pale Millenium Tower tena la mkopo nimekatwa miaka mitatu sina hamu pia kuna siku nilipigwa roba jamaa wakala kila kitu mitaa ya nje ya DUCE kuelekea taifa walikuwa na visu, mapanga na marungu sema tu mimi nikatii kila walichosema wakaniibia simu 2, wallet, viatu, mkanda na pesa

Tokea hapo kila nikiona mwizi nahakikisha napiga vya kutosha na akifa ndio nasikia raha kwani nakuwa nimepunguza kibaka mmoja duniani

Huyo aliyeiba hapo mchikichini ni mwehu maana kupona kifo hapo ni asilimia 1 kati ya 100 ila siku hiyo aliamka na zali hiyo hiyo moja imemwokoa

sasa hivi nimenunua (kihalali) cha moto yaani nikisikia mbwa wangu wanabweka tu nje najiaandaa kumfumua mtu ubongo sina mzaha na mtu anayeitwa mwizi
Bado hujanishawishi kuua kibaka
Katika sheria kuna mahala wanazungumzia reasonable force yaani huwezi kumtwanga risasi kibaka aliyekuja kwako bila silaha ya mto (only in tanzania labda)
Pia mie huwa nina mbinu ya kupambana na hawa jamaa bila ya kuwaumiza.

Kama unapenda kuishi ujue hata shetani anapenda kuishi naye sembuse mtu mbaya!
 
Jamani kama simu au sufuria la ugali unaua mtu. Hebu tujiulize anayeibiwa ni mmoja lakini mwizi anauwawa je, wanaoibia watu millioni 40 mbona wanaachwa wakishangilia?
Ndo maana tunawashauri watu wampigie kura SLAA maana inaonesha watu wameshachoka na maisha ila hawajui hilo
 
Bado hujanishawishi kuua kibaka
Katika sheria kuna mahala wanazungumzia reasonable force yaani huwezi kumtwanga risasi kibaka aliyekuja kwako bila silaha ya mto (only in tanzania labda)
Pia mie huwa nina mbinu ya kupambana na hawa jamaa bila ya kuwaumiza.

Kama unapenda kuishi ujue hata shetani anapenda kuishi naye sembuse mtu mbaya!
najua kuwa kuna sheria hata siku niliyouziwa nilielezwa yote hayo ila naua na jela siendi labda bongo iwe marekani ndio nitaenda jela
 
kwani unaua peke yako si mnakuwa wengi kila mtu anapiga kwa hiyo mnashea dhambi

ila mimi binafsi hata peke yangu naua kwa sababu ukizubaa wanakuwahi wewe mie nakaa sehemu ambayo kuna ule wizi wa kumtaimu mtu getini yaani nikikaribia home naweka cha moto mkononi kabisa mtu akijimiksi tu namfumua ubongo


nilikuwa cna mpango wa kucheka kabisa leo, khaa!....pics zinackitisha sana tena huyo wa mawe ndio bac tena, lakini binadamu tuna roho ngumu sana,huyo alieshika kisu utadhani anakimbiza kuku achinje, na hapo hapo hawa watu mie wananilizaga sana jamani.
 
Hasikitishi hiyo dada Binafsi nakuwa na petroli katika galoni nimeweka ndani ya gari siku nikija kukumbana na watu kama hao simpi muda na mwagia petrol na kumuwasha utakuja shuhudia humu kwenye Jf sitanii hiyo ndio dhamira yangu ,pongezi za zati nawatumia wananchi wenye uchungu katika kuhangaika na maisha mnapokumbana na watu kama hao msiwapi nafasi ya pili katika maisha.
Iko siku nawewe utachomwa tu.
 
Kuna makala inayozungumzia mambo ya kijichukulia sheria mkononi -- Source: Tukemee ufedhuli! (Makala kamili yenye picha, video clips etc, inapatikana kwenye link iliyotolewa...)

______________________________________

Kelele za "mwizi, mwizi!" zinapopigwa, unyama na ukatili usio wa kawaida huamshwa ndani ya roho za baadhi yetu. Huu ni ukweli usiopingika kutokana na maovu tunayowatendea binadamu wenzetu, wanaoitwa wezi. Tunawapiga na hata kuwachoma moto bila kujua kama wana hatia au la; kama wameiba fedha za umma au wamekwepua tu cheni bandia. Kuendelea kwa matendo haya ya kinyama, kikatili na kutisha, ni kosa letu wote. Na ni lazima tugawane lawama sisi sote kama wanajamii.

Inatubidi tujiulize: Huu ukatili uliojengeka na kuwa sehemu ya utamaduni umetoka wapi? Ni kwanini bado tunakubali uendelee katika jamii yetu?

Hoja za majibu hayo ni nyingi, lakini pia nyingi ni za kijinga na kipumbavu, tena hutoka kwa watu wanaojidai kuwa na akili timamu - kumbe ni makunyata tu! Hili suala la kuongezeka kwa hali ngumu ya maisha, huja na ongezeko la hasira, ngeni, hasa pale mtu anapoibiwa kile alichokihangaikia kwa jasho na damu yake, tena kihalali. Hilo linaeleweka, lakini halitoi idhini kwa mwananchi kujichukulia sheria mkononi. Watu wote wanaojichukulia sheria mkononi, wao pia wamevunja sheria sawa sawa na yule muhalifu wanayempiga. Tena uhalifu wao ni mkubwa zaidi kwasababu wao wameua! Wameiba uhai wa mtu ambae aliiba simu, ambayo inayoweza kununuliwa tena. Inaonekana ukatili ukitupanda, basi unatupanda kweli na tunatupa pembeni mawazo na maamuzi ya busara, na kuanza kumcheka nyani na makalio yake bila kujua kuwa yetu ni mekundu pia. Tena yetu ni mekundu zaidi kwani yanatiririka damu ya huyo tunayempiga na kumchoma moto.

Lakini, je, ni sahihi ‘kutetea' ukatili wa baadhi yetu na kudai unatokana na ukata wa maisha na umasikini unaotusumbua? Labda hasira na misongo yetu binafsi huishia kutolewa kupitia ukatili kwa tunayemtendea unyama mtu anayeiitwa mwizi. Hapa ndipo ninaanza kuona umuhimu wa madaktari wa kisaikolojia, au therapists. Baadhi yetu, ambao ni wehu na wakatili kupindukia, tunadhani kumpiga mwizi itapunguza kuchanganyikiwa au misongo ya maisha yetu. Kwani, kumbonda binadamu mwingine na jiwe kichwani ni kama therapy session… tiba mbadala.

Sasa ujuha na ukatili ndipo hapo huingiliana kwasababu kuna watu – tena tunaishi nao majumbani mwetu, tunafanya nao kazi, tunasalimiana nao mitaani, na hata kwenda kusali au kuswali pamoja – wanadiriki kutetea ukatili huu. Hoja zao za kikatili na kipuuzi hudai kuwa, kuwauwa wezi ni fundisho kwa wengine; tatizo la uhalifu litapungua.

Nasema fikra hizi ni za kikatili, kipumbavu na kipuuzi! Na watu wenye mawazo haya tuwaogope zaidi ya ukoma!

Kwasababu ifuatayo: Hali halisi ni hivi, hata tukiwachapa na kuwachoma moto vibaka kwa kasi mpya, nguvu mpya na ari mpya, kamwe hawatapungua. Hii ni kwasababu, mwisho wa siku, tumbo lenye njaa litakoroma tu; njaa itauma, na binadamu huna budi kukubali kulitumikia vile uwezavyo. Utake usitake. Na jinsi ajira zilivyokuwa finyu, kwa waliosoma na ambao hawakubahatika au kupata nafasi ya kusoma, hawawezi kuacha kuiba mpaka wapewe maisha mbadala. Sisemi kwamba kama hujasoma na huna kazi basi uibe. Hapana! Lakini ndio hali halisi ya vibaka wengi. Jambo la msingi hapa ni kwamba, kujaribu mabadiliko ya mazingira hubadilisha tabia za watu; kwani hata siku moja mkulima wa mahindi havuni mihogo.

Upande wa pili wa sarafu ni hivi vyombo vyetu vya habari. Waandishi wa habari wanazidi kutuangusha katika kupinga huu ukatili. Vyombo vya habari vimekuwa vikichochea badala ya kukemea, na hata wale ambao wanakemea, wanafanya hivyo kinafiki! Sio wote, ila kuna wale ambao wanakemea huku wakitumia lugha ya uchochezi.

Vyombo vya habari vina nafasi nyeti sana katika jamii, kama tulivyoona katika mauaji ya halaiki Rwanda mwaka 1994. Vyombo hivi vilitumika kujaza watu uhasama na kuchochea mauaji, huku wakiita upande mmoja "mende." Hiyo ilisaidia kufanya upande huo kuonekana sio binadamu tena, hivyo thamani yao kupotea na utu wao kuyeyuka. Matokeo yake tunayatambua vizuri.
Kwani, si ni vigumu kumuua kuku? Ujue, pindi utakapomuona binadamu mwenzako kama kiumbe tofauti na binadamu, basi kumuua inakuwa sio vigumu tena! Leo hii vyombo vya habari wanadiriki kutumia lugha kama mwizi "akibanikwa."

Hebu tuangalie matumizi ya lugha hapo. Kuku hubanikwa, mbavu za mbuzi hubanikwa, hao wote ni wanyama! Lakini utumiapo neno hilo kwa binadamu mwenzako, ina maana umemvua utu wake. Thamani ya uhai wake haizidi ya mnyama mwingine yoyote tunayemchinja kama kitoweo. Hivyo, pamoja na kuwa tunaweza tukawa tunapinga mauaji hayo, lakini matumizi ya lugha yetu yanahamasisha na kuchochea.

Halafu vyombo vingi hupenda kutumia maneno "wananchi wenye hasira kali."
Kuna chembe za kuhalalisha dhana ya ukatili. Eti kwasababu walikuwa na hasira, na tena ni haki yao kuwa na hasira… Huu ni ujinga mtupu ulio tukuka! Kwani mara nyingi hao wananchi wenye ‘hasira kali' ukiangalia picha kwa ukaribu, utagundua wengi wao wana nyuso za kushangilia, kuchekelea na kushabikia. Hivyo hiyo dhana ya kuwa na hasira ni potofu.

Vyombo vya habari na waandishi wamekuwa wakipotosha jamii kwa kuchapisha na kuongelea mambo ya uongo. Hapo hapo, vikizidi kuwachochea wakatili hawa badala ya kukemea moja kwa moja kwa lugha sahihi - kali. Hivi kwani, tukiwaita wananchi hao wakatili, wauaji, kuwapiga picha na kuwaanika mbele ya jamii, si litakuwa jambo la busara? Mbona wezi wa mali ya umma, mapapa wa nchi hii, tunawaita mafisadi? Kwanini wao tusiwaite wajasiriamali?

Inabidi baadhi ya vyombo vya habari viache unafiki na ushabiki. Mimi na wewe hatuna budi kupinga na kukumea vikali unyama huu! Na kuacha kuwaita hao wauaji ‘wananchi wenye hasira kali', kwani (nadhani) tunawapa kichwa kwa uwenda wazimu wao.

Tuwapige picha, na tuanze kuwatafuta. Tukianza na huyu aliyebeba tofali na huyu anayemvisha tairi mwizi!
Jeshi la polisi nalo libebeshwe lawama kwa kushindwa kukomesha huu unyama. Tabia ya kuwaachia wahalifu kutokana na sababu wanazozijua wao wenyewe linachangia ukatili huu kuendelea. Wakuu wa Jeshi la Polisi nawashangaa kwani hawaoni aibu kwa kufanyiwa kazi yao na wananchi. Kwani hii imekuwa hadithi ya mkia kuongoza kichwa? Jeshi la Polisi liwatie nguvuni wahalifu na mkondo wa sheria uchukue nafasi yake. Pia, iwatie nguvuni wananchi wanaoshiriki katika haya mauaji ya kutisha. Hata kama atakamatwa mmoja, huo ndio utakuwa mwanzo. Jeshi likikaa na kushangalia haya mauaji, na sisi raia wa kawaida tufanyeje? Mheshimiwa IGP Mwema, hili ni tatizo ambalo nadhani linahitaji suluhisho, au haya maradhi yatazidi kuendelea kwenye jamii, na kidonda kuishia kuwa ndugu.

Mimi ninaamini kunaweza patikana njia mbadala ya kuadhibu wahalifu tunanapowakamata mitaani. Kwanini tusifanye kama nchi nyingine, mwizi akikamatwa, achapwe mijeledi kadhaa, kisha apelekwe polisi? Hili linaweza kusimamiwa na balozi wa nyumba kumi kumi wa mtaa aliokamatiwa mwizi huyo, au hata kiongozi yoyote wa mtaa huo. Lakini utekelezaji wa adhabu hii utafanywa ndani ya vipengele vya sheria na si kienyejienyeji tu.

Hoja ya pili ni hii ya kukata viungo pindi mwizi akamatwapo. Hilo lisipewa hata nafasi, kwani haliwezi kuwa adhabu mbadala. Najua baadhi yetu hapa ambao wanadhani hilo ni jambo la maana katika kukomesha wahalifu. Hilo ni jambo la kikatili sana, kwani ukishamkata mtu mkono umezidi kumrudisha nyuma kimaisha. Kivipi? Wezi wengi ambao tunawakamata mitaani ni watu ambao hufanya kazi za kutumia nguvu "blue collar jobs," kama zikipatikana. Hivyo basi, pale tunapoamua kumkata mkono, tunamfanya ashindwe kuweza kujitegemea. Kazi gani atapata akishakuwa na mkono mmoja, na hana elimu? Hivi kweli atapata kazi ya kubeba mizigo Kariakoo, au ataishia kuwa omba-omba, halafu aanze kufukuzana na wana-mgambo? Hilo la kukomeshana kwa kukatana viungo halina mantiki, tena ni ukatili mwingine ambao utaongezea watu shida za kimaisha badala ya kuwasaidia.

Kuna mambo mengi sana ambayo yanaweza kufaidisha Taifa letu pindi wezi wanapopatikana na kufungwa jela. Tanzania ina ardhi kubwa tu, kwanini wasilimishwe? Au hata kwenda kusaidia wanavijiji kuvuna na kulima, na kushughulishwa na kazi nyingine za kijamii? Serikali haitakuwa na haja tena ya kuajiri watu wengi kufanya baadhi ya kazi zinazohitaji nguvu nyingi kwani zitashughulikuwa na wafungwa. Tayari, si wanalishwa na kodi zetu? Basi watumiwe ipasavyo katika jamii ambayo inawalisha. Moja, watajifunza mbinu mbadala za kuendesha maisha yao. Pili, watasaidia kujenga jamii badala ya kuendelea kuiharibu kwa matendo yao maovu.

Mwisho, tusikae hapa na kujazana ujinga. Eti jicho kwa jicho, jino kwa jino ndio suluhisho la uhalifu. Sote tutaishia kuwa chongo au vibogoyo. Sasa sijui nani atamwongoza nani baada ya hapo. Wadau wa kwenye vyombo vya habari wajue kwamba wao wana nafasi kubwa sana katika kukemea na kusaidia kutokomeza huu unyama wa baadhi ya manduli wachache katika jamii yetu.

Pia tusisahau kuwa, hata tukichomana moto kila siku, kama hali ya maisha ni ngumu, ni ngumu tu. Na watu watafanya vyovyote kukidhi mahitaji yao; hapo ndipo viongozi wa maisha bora kwa kila Mtanzania inabidi waulizwe, kulikoni? Hivyo, wachochezi wote wa huu unyama, wananchi wenye roho za kikatili za namna hii na viongozi mafisadi wanao sababisha hali ya Mtanzania kuzidi kuwa ngumu, wote ni makunyata!

Vijana wenzangu, hatuwezi kuendelea kufanyiana ukatili kama huu sisi wenyewe kwa wenyewe. Tuelewe kuwa umasikini wetu unasababishwa na mafisadi wachache walio juu… Hao ndio maadui zetu wakubwa.



Tazama video hii kama tu una moyo mgumu.
 
Vijana FM (jina lako zuri sana) naona huyo mwandishi ameangalia upande mmoja tu wa shilingi na hajawahi kukutana na maswaibu ya wezi na majambazi wasio na huruma ambao wanatutoa uhai kila siku majumbani, kwenye biashara na maofisini, kuna matukio mengi yanatokea majambazi kuua na yakifika polisi yanaachiwa, kuna wezi wanacharanga watu na mapanga kila siku na kuwapa vilema vya maisha na kuua pia hayo huyaoni

Kwa nini wakienda polisi mchana jioni wanaachiwa wanazidi kuleta maafa tena, na wengine wakifika mahakamani wanatolea kwa njia za panya, vyombo vya dola vimepoteza mwelekeo ndio maana unaona watu wanachukua sheria mkononi wamechoka hakuna anayepanda kuua ila hali ni mbaya usipoua utauliwa wewe
 
Inasikitisha sana.. lakini wakikubana, Hawana huruma kama wewe unavyowaonea huruma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom