Wananchi wamechoka maana wanaona kila kitu ni usanii, la msingi wao wafanye wawezavyo. Kimsingi si sawa kuruhusu haya kutokea lakini hatuwezi kuyatibu kwa kuwanyima kufanya hivyo tuu, tunapaswa kujua vyanzo vya mambo haya na kuvishughulikia kwanza. Hapo tukiwasisitizia wananchi kuacha wataacha. Jeshi letu limeduwaa sana kwenye kuthibiti uhalifu, hata hivyo nao wao kwenye wakati mgumu maana maisha yao magumu, kipato chao kidogo na masikini kuliko wahalifu (obvious rushwa itachukua nafasi). Serikali yenyewe bado intakiwa kulaumiwa kwa yote, muundo mzima ni mbovu na kuna mambo mengi sana ya kurekebisha walau taratibu, kibaya ni kwamba juhudi kubwa za serikali ni kupambana na wananchi ili huu muundo mbovu uendelee kutumika.
Zamani ilikuwa ajabu sana kusikia kiongozi anasemwa semwa, wakaanza kusemwa lakini ilikuwa ajabu sana kuandikwa gazetini hata kwa tetesi za ubadhirifu. Lakini hayo yote yameendelea na sio ajabu sasa kutukana viongozi live kwenye internet, kuwatukana live kwenye magazeti, kusema habari zao za ubadhirifu live kwenye tv, kuwazomea viongozi wakubwa kama rais na mawaziri, kurushia misafara mawe n.k.., nina mashaka siku sio nyingi haitakuwa ajabu kuvunja-vunja na kuchoma moto magari ya viongozi wa serikali kisha baadaye kidogo itakuwa sio ajabu pia kuwakamata na hata kuwachoma moto viongozi wa serikali tulioona wazi ni wezi kama akina Chenge, Karamagi na wegineo kabla hatujaja kwa prezidaa ambaye atakuwa akilaza damu kuwashughulikia wezi wa nchi hii.
Maandamano na mashinikizo mengi ya kuwang'oa watawala yanayotokea katika nchi nyingi duniani hayakuanza siku moja, yalianza kwa wananchi kuminywa sana, kisha kupata habari na kujanjaruka kwamba wanaminywa. Kisha huendelea kwa wao kuanza kudai haki zao taratibu na wasipposikilizwa hufikia kutumia nguvu ikiwa ndio njia iliyobaki kwao kupata haki zao.
Watawala wanajifariji kwamba wanayofanya kwa sasa yatatupooza, mfano Kikwete anapopiga kelele na mambo ya mbolea anashawishika kwamba watu watapoa. Kimsingi itamsaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa hasira za wananchi, lakini sio kusafisha kutu zilowaingia watanzania kwa kugundua wanatapeliwa. Kikubwa hapa mfumo mzima ushughulikiwe tena "in-time" la sivyo ngoma iko pale maana tunaona wazi na tunazo data za kutosha kwamba wote huu ni usanii.
Watawala pia wanajitia moyo kwamba asilimia kubwa ya wananchi hawajui nini kinaendelea kwahiyo bado wanayo nguvu na muda wa kukaa, niwape tu wana-usalama tahadhari kwamba hii kampuni ya SEACOM inayoleta mkonga wa internet hapa kwetu italeta mabadiliko makubwa kwenye nchi hii ikiwemo wananchi wengi zaidi kupata taarifa haraka haraka zaidi na kwa urahisi zaidi. Sijafanya utafiti lakini naamini taarifa zitaenea over 10 times faster in few time to come. Tukumbuke kwamba kwa kipindi cha karibuni internet imechangia sana kulipua mabomu mengi yahusuyo ubadhirifu katika nchi hii, ina maana matumizi ya internet yakiongezeka pamoja na mambo mengine harakati za kupambana na mafisadi zitaongezeka maradufu. Kibaya ni kwamba wae wenye nguvu ndogo watakuwa wamepata msaada na kwa vyovyote nguvu ya umma kui-resist serikali itaongezeka kuliko uwezo wa serikali kuithibiti kwa njia ya demokrasia. Serikali itachagua vita ama ipoe ifanye itakachoelekezwa.
Naomba niishie hapa kwa leo maana naona simalizi wakuu, ni mengi sana na naomba tujifunze kutathmini mbeleni kutokana na historia zetu.