Sheria mbovu za Uchaguzi Tanzania: Wapiga kura na wapigiwa kura

Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mimi nimekuwa nikijiuliza sababu gani Mbunge anayeishi Kinondoni Dar, anaweza vipi kugombea Ubunge jimbo la Babati au Rorya wakati mwananchi asiyeishi jimbo hilo haruhusiwi kupiga kura jimbo lolote.

Kuna sababu gani haswa zilizopelekea sheria hii kutungwa na kuna faida gani? Je, sheria hii haizai Ukabila kiasi kwamba mkazi wa Dar ataenda kwao kugombea Ubunge wakati si mkazi wa huko na kishahama yeye na familia yake?.

Nijuavyo, kwa taratibu za Kugombea Ubunge, mgombea hatakiwi kugombea nje ya jimbo analoishi maana wananchi wa huko hawamfahamu vizuri uwezo wake, sii mkazi hawezi kuyajua ama kuyafuatilia matatizo yao na pili kuhusiana na wakazi wanalazimika kupiga kura katika majimbo yao kwa sababu wanayataka maendeleo ya jimbo wanaloishi na kiongozi watakayemchagua ndiye anayefaa kukuwakilisha jimboni.

Mpango huu una mantiki na unaeleweka sehemu zote duniani lakini mfumo wa Tanzania kusema kweli siuelewi maana yake wala sababu za kwa nini mbunge anaruhusiwe kugombea sehemu yoyote asiyoishi? Kwanini? Halafu upande wa pili mpiga kura haruhusiwi kupiga kura sehemu asiyoishi.

Wanabodi nawaomba darasa maana nijuavyo gharama za Ubunge zinazidi kuwa kubwa kutokana na mifumo vibovu kama hii.
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Bila tume hii kutoka. Tume ya magogoni, sheria mbovu za uchaguzi nyingi tu zitaendelea kuwepo hata ukiingia upinzani!
Lakini hilo la Ubunge lipo katika katiba na sidhani kama hata rasimu ya Warioba wameliondoa kulazimisha wakazi tu ndio wagombee sehemu zao. Hizi gharama za mafuta kila mwezi zinatuumiza majimbo hayana ukubwa huo isipokuwa wanasafiri safari ndefu sana kurudi majimboni kwa gharamia sisi.
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,341

Hii ni hoja ya maana kabisa. Lakini kumbuka kuanzia kuandika katiba, kutunga sheria za uchaguzi na kuendesha nchi wanasiasa ndio kila kitu.

Hii sheria iko kwa ajili ya maslahi yao kwasababu wanajua kabisa vijijini hakukaliki na maisha ni magumu hivyo dawa ni kuishi mjini na kurudi vijijini wakati wa uchaguzi tu. Katu hawatakubali kabisa ibadilishwe kwani itawaondolea huu uhuru.

Kumbuka hata kwenye hii katiba mpya ilikuwa imesema wabunge wasiwe mawaziri (kitu ambacho ni muhimu sana) lakini wanasiasa wakaona hapa wataumbuka wakabadilisha.

Afrika inaangamizwa na wanasiasa (soma matapeli)
 
Ndio maana sisi kama wananchi na wanaharakati tusikumbwe na hizil fikra za Uchama wakati tuliomba Katiba yetu na itokane na sisi wenyewe. Uchaguzi huu hautaweza kufanikisha lolotee zaidi ya kurudia na kuendeleza mfumo ule ule unaotajirisha viongozi.

Mimi nasema hata kama UKAWA wakishinda uchaguzi hawawezi kubadilisha mfumo huu kwa sababu hakuna kati yao yupo tayari kurudi Kijijini kwake wakati nyumba na Shamba lake lipo Mbezi au Mkulanga. Hakuna mbunge atakaye kubali kupoteza nafasi ya Uwaziri pale kisha kamata madaraka. Utapeli huu hauna mwisho wala chama ni gonjwa ambalo linahitaji sisi wananchi wenyewe kusimama dhidi ya mfumo mzima.
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,695
2,000
Sheria za uchaguzi ni mbovu sana sana. Jiulize kwa nini kupiga kura si lazima uwe mwanachama wa chama chochote lakini kupigiwa kura lazima uwe na chama! Mantiki iko wapi?

Kwa nini wananchi wamchague mbunge na baadae wagundue kuwa aliwatapeli wasimuondoe? lakini mwenyekiti wa kijiji/kitongoji/mtaa wananchi wanaweza kumuondoa wakiona hatimizi malengo yao na kuchagua mwingine!?

Sheria mbovu zimezaliwa na katiba mbovu. Katiba mbovu imetungwa na wanasiasa wabovu! Hilo ndilo jibu la ukweli!

Kila mwanasiasa anakoona ana maslahi atapitisha sheria mbovu ilimradi tu yeye anufaike!
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,341
2,000
Ndio maana sisi kama wananchi na wanaharakati tusikumbwe na hizil fikra za Uchama wakati tuliomba Katiba yetu na itokane na sisi wenyewe. Uchaguzi huu hautaweza kufanikisha lolotee zaidi ya kurudia na kuendeleza mfumo ule ule unaotajirisha viongozi.

Mimi nasema hata kama UKAWA wakishinda uchaguzi hawawezi kubadilisha mfumo huu kwa sababu hakuna kati yao yupo tayari kurudi Kijijini kwake wakati nyumba na Shamba lake lipo Mbezi au Mkulanga. Hakuna mbunge atakaye kubali kupoteza nafasi ya Uwaziri pale kisha kamata madaraka. Utapeli huu hauna mwisho wala chama ni gonjwa ambalo linahitaji sisi wananchi wenyewe kusimama dhidi ya mfumo mzima.

Ni kweli. Lakini sisi waafrika tuko kama tumelogwa. Vyama na dini vinafanya watu wasione makosa ya wanaotuongoza. U
 
Janjaweed

JF-Expert Member
Jan 20, 2010
11,036
2,000
Hoja nzuri, labda tujiulize nchi zenye mfumo wa kisiasa ka wetu zimehandle vipi hii issue ya makazi ya wabunge?? kwasbabu tuna wabunge wengi sana wana nyumba vijijini where they spend less than 20% of time na nyumba mijini... in some extreme cases tuna mbunge wa chadema "vitu maalum" yeye yuko USA kabisa

I general mfumo wetu wa siasa ni mfumo changanyishi, na umewekwa hivyo on purpose ili waendelee kutuzuga
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,691
2,000
Lakini hilo la Ubunge lipo katika katiba na sidhani kama hata rasimu ya Warioba wameliondoa kulazimisha wakazi tu ndio wagombee sehemu zao. Hizi gharama za mafuta kila mwezi zinatuumiza majimbo hayana ukubwa huo isipokuwa wanasafiri safari ndefu sana kurudi majimboni kwa gharamia sisi.

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa tume ya jaji Warioba lipendekeza/wananchi walio wengi walipendekeza Mbunge awe ni mkazi wa eneo husika na hasihurusiwe kukaa nje ya jimbo lake kwa kipindi kisicho zidi miezi 6 bila sababu ya msingi(ila sina uhakika) Kwa hiyo basi swala la wabunge wengi kama sio wote kwenda kujirundika Dar na kusahau majimbo yao linawaumiza wananchi na ndo maana wakapendekeza kitu kama hicho.

Lakini Katiba ya Sitta na Chenge ilikitupilia mbali kifungu hiki.

Tukirudi kwenye hoja yako. Ukiangalia wabunge wengi kama si wote wakishachaguliwa tu basi wanaamisha hata makazi yao na kuyapeleka Dar. Katika majimbo yao wanakwenda tu kama likizo au kutembea lakini si wakazi wa hayo jimbo na kitu hiki kinarudisha maendeleo ya wananchi nyuma maana Mbunge ambaye ni mtetezi wao, mtu ambaye anawawakilisha matatizo yao serikalini, mtu ambaye alitakiwa kuwa katika jimbo lake masaa 24 akifanya kazi na wananchi wake, leo unamkuta yuko Dar anaongelea habari za foleni na mafuriko hali katika jimbo lake kuna matatizo zaidi ya hayo.

Napenda kumpongea Mh. Nassary mbunge wa Arumeru angalau anaonyesha mfano wa jinsi mbunge anavyotakiwa kuwa.

Na hivi ndo vitu vya muhimu ambavyo sheria zetu za uchanguzi vilitakiwa kufanyiwa marekebisho ili twende na wakati. Lakini kiyume chake tume hiko busy na kungeza majibo/ulaji kwa wanasiasa.
 
hata pendekezo la rasimu ya Warioba bado lilikuwa na makosa juu ya hili kwa sababu hivi leo wabunge wote wameisha rudi majimboni kuanza kampeni za kimya kimya waonekane wapo, lakini ukweli unabaia kuwa sii WAKAZI wa hapo. Toka kikao cha bunge lilopita wote wameisha rudi majimboni na wana sababu leo ya kutokuwepo kutokana na kikao hiki cha Bunge, hivyo tusikubali mbinu hizi za ujanja ujanja.

Mbunge anaweza kuishi Dar miaka minne yote akienda jimboni mara moja kwa mwaka na kukaa wiki, lakini inapokaribia uchaguzi hurudi jimboni kuanza kujipendekeza, tumewazoea hawa kilichotakiwa ni lazima Mbunge awe mkazi wa hapo, ana nyumba, kama shamba liwe jimboni awe mfano wa kutumikia sio kuwatumikisha watu wakati yeye yupo Dar. Watoto wake wasome shule za hapo sii ndio kazi yake? kama anataka kulijenga taifa la wote sio njia za kuchuma.

Na Sisi wananchi, Uraia wako wenye kuonyesha siku ulozaliwa ndio kitambulisho chako hakuna sababu ya kadi za kupigia kura. Kama una uthibitisho wowote wa kuonyesha Ukazi wako na umri wako hakuna sababu ya kujiandikisha, tena inatakiwa serikali iwe na rekord ya watu wote wanaozaliwa wakifika miaka 18 tu anapewa namba na ifanyike mashuleni zaidi ya ofisi za serikali.

Inasikitisha sana kuwasoma viongozi wa vyama na serikali wakizungumzia sana matukio badala ya kutazama wataweza vipi kuubomoa mfumo huu ili tujenge Taifa la kesho maana nina hakika tumeliwa tena na tena kila kukicha ni hadith za Utapeli mtupu.Leo kweli watu wenye uchungu na nchi hii mkajirithishe millioni 200 kila mmoja kwa utumishi wenu kama sio kuwaibia wananchi nini zaidi!
 
Alinda

Platinum Member
Jun 26, 2008
1,691
2,000
hata pendekezo la rasimu ya Warioba bado lilikuwa na makosa juu ya hili kwa sababu hivi leo wabunge wote wameisha rudi majimboni kuanza kampeni za kimya kimya waonekane wapo, lakini ukweli unabaia kuwa sii WAKAZI wa hapo. Toka kikao cha bunge lilopita wote wameisha rudi majimboni na wana sababu leo ya kutokuwepo kutokana na kikao hiki cha Bunge, hivyo tusikubali mbinu hizi za ujanja ujanja.

Mbunge anaweza kuishi Dar miaka minne yote akienda jimboni mara moja kwa mwaka na kukaa wiki, lakini inapokaribia uchaguzi hurudi jimboni kuanza kujipendekeza, tumewazoea hawa kilichotakiwa ni lazima Mbunge awe mkazi wa hapo, ana nyumba, kama shamba liwe jimboni awe mfano wa kutumikia sio kuwatumikisha watu wakati yeye yupo Dar. Watoto wake wasome shule za hapo sii ndio kazi yake? kama anataka kulijenga taifa la wote sio njia za kuchuma.

Na Sisi wananchi, Uraia wako wenye kuonyesha siku ulozaliwa ndio kitambulisho chako kahuna sanbabu ya kazi za kupigia kura. Kama una uthibitisho wowote wa kuonyesha Ukazi wako na umri wako hakuna sababu ya kujiandikisha, tena inatakiwa serikali iwe na rekord ya watu wote wanaozaliwa wakifika miaka 18 tu anapewa namba na ifanyike mashuleni zaidi ya ofisi za serikali.

Inasikitisha sana kuwasoma viongozi wa vyama na serikali wakizungumzia saana matukio badala ya kutazama wataweza vipi kuubomoa mfumo huu ili tujenge Taifa la kesho maana nina hakika tumeliwa tena na tena kila kukicha ni hadith za Utapeli mtupu..leo kweli watu wenye uchungu na nchi hii mkajirithishe millioni 200 kila mmoja kwa utumishi wenu kama sio kuwaibia wananchi nini zaidi!

Unachongea ni kweli.. Ila nikipata muda nitapekua pekua tume ya Jaji Warioba walipendekeza nini.. Lkn ilikuwa mbunge ni lazima awe ni mkaazi, awe na nyumba na awe ameishi hapo kipindi kisichopungua miaka 3 (??) sina uhakika nitapekua au hata wewe ukipata muda pekua pekua...
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Unachongea ni kweli.. Ila nikipata muda nitapekua pekua tume ya Jaji Warioba walipendekeza nini.. Lkn ilikuwa mbunge ni lazima awe ni mkaazi, awe na nyumba na awe ameishi hapo kipindi kisichopungua miaka 3 (??) sina uhakika nitapekua au hata wewe ukipata muda pekua pekua...
Mimi nimekuwa naipinga sana rasimu ya Warioba kwa sababu imepotosha sana wananchi, Katiba ile ni ya Serikali ya JMT haihusiani na katiba za nchi ambazo zingeundwa baada ya kuzaliwa Tanganyika haswa katika mambo mengi yasokuwa ya Muungano.

Kwa hiyo mwongozo wote mengi humo ni katika mambo yalokuwa ya Muungano. Bunge linalozungumziwa humu ni bunge la Muungano, hivyo kuacha wabunge wetu wangeendelea kutunga sheria za nchi zao na kujilipa wanavyotaka maana sii fungu la JMT. Leo hii Bunge la EAC haliwezi kuamua malipo ya wabunge wa Tanzania na wala hawana nguvu hiyo zaidi ya kutunga sheria za malipo yao wenyewe, kwa hiyo utaona kwamba tulipigwa bao toka dakika ya kwanza ya uandishi wa rasimu.

Kosa kubwa walolifanya Kina wariobani kujaribu kuepuka gharama za serikali 3 za Shrikisho ambazo zingelazimu kuwa na serikali kubwa ya Muungano halafu serikali ndogo za nchi ambapo mambo yote ni ya Muungano isipokuwa mamlaka ya usimamizi wa shughuli za serikali hiyo ndio hugawawia nchi husika. Kwa hiyo Tanganyika tungekuwa na mamlaka ya kusisimia mambo yetu sisi, Zanzibar nao vile vile, lakini sote tukiwa chini ya serikali ya JMT. Na isingewezekana hivyo pasipo kubadilisha kwanza Artical of Union kuonyesha ni Jamhuri za nchi mbili zilizoungana kuunda JMT na hivyo jina kubadilika kuwa The United Republics of Tanzania yaani tunaongeza s mwisho wa Republic.

Kwa hiyo kifupi, katiba hiyo na ukazi wa mgombea inazungumzia mgombea ubunge katika serikali ya JMT na kuacha wazi muundo wa serikali ya Tanganyika, bunge, na mahakama zake ktk kuendesha, kutunga sheria na kutafsiri zinazohusiana na mambo yasokuwa ya Muungano. Ni kama Bunge la EAC linatunga sheria zake ktk mambo tuloungana lakini hawaingilii sheria za kila nchi ambazo sii ktk maridhiano ya mambo ya Jumuiya.
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
41,859

Hapa kuna pande mbili ambazo zote zinabeba lawama kwa hali hii
  1. Mbunge/mfumo, hapa sisi kama taifa tumewaachia wabunge kuwa wachezaji na wakati huo huo kujitungia sheria za mchezo na kuwa marefariii kwa wakati mmoja. Katika mazingira haya unategemea nini ziadi ya watu kujipimia wa kushiba? Kwa mazingira haya ya watu kugeuza uongozi kama ajira ya kudumu ya sehemu ya kutokea kimaisha ni lazima wabunge wajitungie sheria zitakazowabeba. Kwa hiyo kwa upande huu inabidi sisi kama wananchi tuwe makini sana. Huko mbele ya safari inabidi bunge la katiba kwa mazingira ninayoyaona ni bora tuweke makundi yote tena kwa uwiano ama wale watakoingia kwenye bunge la katiba baada ya bunge hili wasiruhusiwe kugombea wangalau 5-10 years. Hapo tutaona katiba yenye meno na sio hii ya kuwapa wabunge waliopo lazima watalinda maslahi yao.
  2. Wananchi/ wapiga kura, mimi hapa huwa naona watu wenyewe kama wajinga fulani. Hivi inawezekanaje wewe leo unachagua mtu anayekuja jimboni mara moja moja tena akija kwenye msiba ama kusalimia wazazi wake huku ana maji ya chupa halafu msafi kama nini. Kisa eti unakuta ni kabila/dini yako, huku akiongea kiingereza cha kubabia!! Unakuta mtu kama huyo anaishia kuwanunulia watu pombe, chakula na kukaa mbele kwenye msiba karibia na uchaguzi, basi watu wanambabaikia balaa. Matokeo yake akishapata ubunge anahama kwani watu wanadhani ni mfadhili wa kudumu na yeye zile kero za kupigwa mizinga inabidi ahamie kwa watafutaji wenzake anawaacha na shida zenu. Ukimpigia simu hapokei wakati hayupo kwani anajua ni usumbufu wa kuombwa. Si unajua tena wa kijijini wanavyojua kuomba mpaka inakuwa kero. Yeye ukizingatia mlishamalizana kwenye pombe na chakula hapa hana muda wa kukaa jimboni kwani wapiga kura kwa wakati huo hawana nafasi bali biashara zake. Hapa wa kulaumiwa kwa kiwango kikubwa ni wananchi.

Suluhisho la mambo haya ni lazima wananchi wajiwekee utaratibu, kama hajawahi kukaa wangalau kipindi cha miaka 3 kati ya mitano iliyopita kabla ya uchaguzi hakuna haja ya kupewa kura. Na inabidi watu wajiridhishe kwamba wewe unapatia maisha yako kwenye eneo husika na sio kuja kama mtaliii na gari la bei mbaya huku ukibeba masimu na malaptop ya bei mbaya kukoga wananchi. Mtu wa aina hiyo awe ni wa kabila lako, dini yako ama nini wananchi inabidi wasimchekee.
 
Tusiwalaumu wananchi hata kidogo, kwa sababu wananchi wanaletewa majina tu, mgombea wa CCM huyu, Chadema Huyu, NCCR huyu wote wachumia tumbo wafanyeje? Mwaka 2010 wananchi wengi hawakupiga kura, walogoma lakini mfumo kandamizi ukapokea matokeo kama yalivyo na mengine kugushiwa pasipo kutazama kwanza kwa nini wananchi hawakupiga kura kwa wingi.

Mfumo kandamizi ndio huu unaoruhusu vyama kuchagua ama kuwachagulia wabunge wake wakagombee wapi na kuna uwezekano gani wa chama kushinda katika maeneo gani, kwa hiyo utaona vyama vinajinadi kupata wabunge wengi ili kuongeza pato lao na si kuhakikisha wananchi wanapata uwakilishi wanaoutaka kutokana na chama kukubalika kwa sera zake. Hivyo wananchi wanalazimika kuchagua sura..

Katiba inachangia sana mambo haya kwa sababu katiba ndio sheria mama ikisema hakuna mbunge kugombea Ubunge mahala popote kama sio Mkazi wa hapo, vyama vitalazimika kufanya hivyo na kizuri zaidi vyama vitalazimika kuwa na matawi ktk jimboni yote kupokea kero na malalamiko ya wananchi iwe chama tawala ama cha Upinzani. leo kuna vyama vitapeleka mgombea Ukerewe wakati hawana hata tawi wala ofisi kwa sababu wanadhani fulani anaweza pata nafasi pale.

Na umuhimu wa Katiba Mpya umepuuzwa kiasi kwamba watu wamejengwa Ujinga mkubwa kudhani Uchaguzi huu 2015 ni muhimu zaidi ya Katiba yenyewe. jamani CCM inajua wanafanya nini kila siku kuhakikisha mfumo Kandamizi hauondoki kirahisi na hasa kupitia sanduku la kura.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom