Sheria kandamizi kupelekwa Bungeni kuiminya TLS kufanya kazi na kutojihusisha na siasa ni marufuku

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
pic+tls.jpg



Kwa ufupi
Baadhi ya mawakili wasema sheria haiweki mipaka ya kujihusisha na siasa


Dar es Salaam. Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesema kitawatumia wabunge wao kupinga muswada wa marekebisho ya Sheria ya TLS, yaliyowasilishwa bungeni hivi karibuni na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Dk Aderladus Kilangi.

Katika kutekeleza azma hiyo rais wa TLS, wakili Fatma Karume kupitia barua yake aliyoiandika kwa wanachama wote akiwaelezea kuwapo kwa muswada huo ametoa wito kwa wanachama kuwatumia wabunge hao kupinga marekebisho hayo.

Fatma katika barua hiyo anasema muswada huo wa marekebisho ya sheria mbalimbali wa 2018 kifungu cha 108, kinalielekeza Baraza la Uongozi la TLS lililochaguliwa kuwasiliana na AG kwanza kabla ya kutengeneza kanuni mpya.

Anasema AG ambaye pia ni mwanachama wa chama hicho, kwake huo ni mfano wa mwanachama mmoja kutumia mamlaka ya Bunge kujipa haki na mamlaka ndani ya jumuiya ya kidemokrasia.

Katika kifungu cha 106(2)(a) cha muswada huo, wanachama wa TLS ambao si raia wa Tanzania wanazuiliwa kuchaguliwa katika Baraza la Uongozi. Vilevile katika kifungu cha 106(3) kinawazuia wanachama ambao ni watumishi wa umma, madiwani, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa kuchaguliwa katika Baraza la Uongozi.

Katika kifungu cha 107 cha muswada huo, wajumbe wa Baraza la Uongozi wanazuiwa kujihusisha na masuala ya kisiasa.

Fatma anasema mambo hayo yanayoweka zuio kwa wanachama wa chama hicho yanayopendekezwa na AG yaliyoingizwa katika kanuni za uchaguzi za TLS, ambayo sasa yameingizwa bungeni yalikataliwa na TLS katika mkutano wake mkuu.

“Mtizamo wangu wa awali kama rais wenu ni kwamba marekebisho ya Dk Kilangi ni ya kibaguzi hivyo yanakinzana na masharti ya Ibara ya 13(1) na 13(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Fatma anasema ataiomba Sekretarieti ya TLS kuitisha mkutano wa Baraza la Uongozi kujadili hatua za kuchukua kwa maslahi ya wanachama akiwamo AG.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Fatma alisema wana imani wabunge hawatakubali kupitisha sheria hiyo ambayo ni ya kibaguzi inayokiuka Katiba.

Alisema kushiriki masuala ya kisiasa ni haki yao ya msingi kwa mujibu wa Katiba na kwamba, haiwezi kuchukuliwa na mtu yeyote.

Akitoa maoni yake kuhusu marekebisho hayo, wakili Juma Nassoro alisema hana shida na wanachama kutokujihusisha na masuala ya siasa, lakini tatizo haijafafanuliwa au kutolewa tafsiri ya wazi ya kujihusisha na siasa.

Naye wakili Daimu Halfani alisema muda na namna ambavyo marekebisho hayo yanafanywa yanaondoa maana halisi, badala yake picha inayojengeka ni kwamba Serikali inalenga kuwabana wapinzani ambao ni wanasheria na kuwadhibiti wanasheria kwa ujumla.

Halfani alisema tatizo lingine katika marekebisho hayo ni kutokuwekwa mpaka katika kujihusisha na masuala ya kisiasa, kufanya shughuli za kisiasa na kutoshirikisha wanachama katika mapendekezo hayo.

Naye wakili Fulgence Massawe alisema kuna mikataba inayolinda mawakili inataka wawe huru, lakini inavyoonekana Serikali ni kama inataka kuidhibiti TLS.
 
Huu mswada bado hujamfikia rais tu atie saini? AG alikuwa anasubiria nini mda wote kuchelewa kupeleka huu mswada bungeni,
 
Ana onaje Ag akapeleka muswada wa sheria wa mabadiliko haya
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kutokuwa mwanasiasa, pia kutochaguliwa na rais.
Pili, wakuu wa mikoa kutokuwa wanasiasa.
Tatu, majaji kutochaguliwa na rais.
Nne, spika wa bunge baada ya kuchaguliwa avuliwe uwanachama ili awe huru.
Tano, wakuu wa jeshi la polisi na usalama kutochaguliwa na rais.

Nadhani haya ni muhimu zaidi kwa taifa letu
 
Back
Top Bottom