Sheria inasemaje ukigonga gari kwa nyuma?

dereva anaendesha magari 3
1. la kwake
2. mbele yake
3. la nyuma yake
hapo sasa ukigonga gari kwa nyuma ww ndo mwenye makosa chakufanya ita wahusika wapime alafu bima ya gari itamalizana mbele kwa mbele na alieumia
Kuendesha matatu nayo ni sheria au ni porojo za driving school
 
Point yako ni nini? Unafikiri sijui mita 20 ni nini? Haya nashukuru kwa kunipa elimu sasa najua mita sio km wala mile.
RRONDO huyu jamaa naona kama alichanganya masuala ya umbali gari na gari. Sasa kuna mtu kasema mita 4 umbali wake sijui kigambni na wapi...... Nadhani labda ni writing errors au uelewa wa vipimo.
 
Kuna nafasi imewekwa kisheria kati ya gari moja na lingine. Sikumbuki ni mita ngapi, ila nadhani ni mita 20. Sina uhakika.

Kwa maana hiyo ukiligonga gari la mbele yako, ina maana hukuzingatia taratibu na sheria za ile nafasi. Kwa maana hiyo unakuwa una kosa.
distance kati ya gari na gari inategemea aina ya barabara "LEVEL OF SERVICE(LOS)" LOS A,B,C,D,E na F distance ya gari na gari ktika LOS "A" ni kubwa mfano free way ila kwny LOS "E" ni ndogo Mfano Mandera road
 
Hiyo ya kulipa ni kama watu tu wameihalalisha lakini ukigongwa kwa nyuma yule aliekugonga ndio mwenye makosa na bima yake ndio inalipa uharibifu uliotokea kwenye gari lakini imekuwa kama sheria mtu akikugonga anakulipa wakati sio
Mkuu, hata hizi bima za kawaida zinaweza kuCover hayo matengenezo uliyogonga au mpaka bima kubwa?
 
Yes nafahamu hilo LA kuendesha magari ma3 mkuu,ila kibinaadamu tu huwa kuna wakati viajali vidogo vidogo vinatokea,....nimeuliza maana kuna mshikaji wangu aliigonga BMW X5 ya mtu, akavunja taa zote za BMW na kuiharibu sura yote ya BMW,jamaa alikubali kosa na hv sasa anadaiwa madeni mtaani karibu 3m aliyokopa kutengeneza BMW,ndo maana nikaona niulize,na ile BMW ilikuwa na comprehensive insurance lkn jamaa alikataa katukatu na kutaka gari yake itengenezwe.
Huyo mshkaji wako alifanya kosa kubwa sana. Kama alikuwa na bima (iwe third party au comprehensive) asingetakiwa kutoa hata senti moja.

Sheria ndiyo inatamka hivyo na ndiyo maana ana bima. Yeye alifuata maelekezo ya aliyemgonga badala ya sheria.

Angekataa kutoa fedha. Kesi ingeenda mahakamani baada ya hukumu unamkabidhi uliyemgonga nyaraka zako za bima, registration card, driving licence copies yeye anaenda kudai bima
 
Ukimgonga mtu kwa nyuma wewe ndio una makosa. Kama una insurance hata third party subiri trafiki aje apime mfuate taratibu insurance yako imtengenezee au kama ana comp insurance itamtengenezea.

Ukimgonga mtu ukiona matengenezo gharama sana subiri trafiki aje insurance italipa.
Nakumbuka mara moja
Kulikuwa na gari aina ya Land rover disc na ndani yake walikuwa wazungu kama wanne hivi
Mbele yao kulikuwa na basi la kampuni ya Dar Exp, wakiwa wameongozana na wote wakiwa kwenye mwendo kidogo punde basi linapunguza mwendo ghafla na kutaka kutoka barabara kuu na kuingia hotel bila kuonesha ishara yoyote. Wale wazungu waliligonga basi kwa nyuma, kilichotokea washwahili wakataka basi lilipwe, wazungu wakavimba kuwa kwanini hajaonesha hata ishara? Mzozo ukawa mkubwa lakini baadae wala jamaa wahakulipwa
 
Watu wengi ukiwagonga wanageuza mtaji ndio maana anang'ang'ania umlipe, au kukwambia lazima ukamtengenezee garage anayoitaka yeye. Hawa dawa yao mwambie tusubiri trafiki aje.
 
dereva anaendesha magari 3
1. la kwake
2. mbele yake
3. la nyuma yake
hapo sasa ukigonga gari kwa nyuma ww ndo mwenye makosa chakufanya ita wahusika wapime alafu bima ya gari itamalizana mbele kwa mbele na alieumia
Hivi ni kweli ...? na je inawezekana kweli dereva 1 kuendesha magari 3 au ni kiki tu za driving skulz...?
 
Sio lazima mpaka mahakamani. Kama una comp insurance kuna form sikumbuki namba ngapi ukiipata tu hio unaanza kutengenezewa gari. Nafikiri third part ndio hadi hukumu itoke.

Pakitokea mgogoro ndio wataenda mahakamani, zaidi ya hapo watafatilia taratibu za kawaida za kujaza form za bima na kufatilia police report.
 
Mkuu, hata hizi bima za kawaida zinaweza kuCover hayo matengenezo uliyogonga au mpaka bima kubwa?
Yes zina-cover ndio maana zikaitwa third party yaani ukimgonga mtu na ikaonekana wewe ndio mwenye makosa, bima yako inatumika kulipia uharibifu kwa gari lingine au umegonga mpitia njia hali kadhalika hivyo hivyo
 
Angalau umefungua njia kidogo mkuu,je hio ipo kisheria kabisa?...I mean akienda bima atalipwa hata km ana third part?
Lakini kumbuka kuna kwenda mahakamani, na ukapigwa faini sasa watu wengi hatupendi usumbufu ndiyo maana mtu unaamua ulipe tu kama ni ela ndogo kuepuka usumbufu.
 
Yes nafahamu hilo LA kuendesha magari ma3 mkuu,ila kibinaadamu tu huwa kuna wakati viajali vidogo vidogo vinatokea,....nimeuliza maana kuna mshikaji wangu aliigonga BMW X5 ya mtu, akavunja taa zote za BMW na kuiharibu sura yote ya BMW,jamaa alikubali kosa na hv sasa anadaiwa madeni mtaani karibu 3m aliyokopa kutengeneza BMW,ndo maana nikaona niulize,na ile BMW ilikuwa na comprehensive insurance lkn jamaa alikataa katukatu na kutaka gari yake itengenezwe.

Huyo jamaa alikuwa boya, mimi kama gharama inazidi Laki na nusu asee hapo hata selo nitaenda, lakini bima lazima ihusike. 3M kumtengenezea gari mtu wakati gari yangu na yake zote zina bima, sasa bima ina kazi gani hapo?
Ukute huyo jamaa wa bmw aliipeleka complaint bima pia akapiga mpunga.
 
Back
Top Bottom