Sheria inasemaje ukigonga gari kwa nyuma?

mmash

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2013
Posts
832
Reaction score
1,240
Habari za leo wanajamvi,kuna utata naupataga kwenye hili swala,labda wajuzi wa sheria za usalama barabarani watatusaidia,....
Mara nyingi inajulikana kuwa ukigonga gari lingine kwa nyuma inakuwa kwamba ww mgongaji ndio una kosa,je ni sheria ww ngongaji ndio utengeneze gari la mwenzako?,i mean sheria hasa za usalama zinasemaje?,maana wengine wanasema kuwa bima ndio zinatengeneza gari zote mbili,je unaweza kukomaa na mwenye gari ili ulipe faini ya polisi then kila mmoja akatengenezewe gari lake na kampuni ya bima?,...hapo naongelea Third part insurance.Naomba wataalam wa sheria za barabarani watusaidie.
 
Mkuu mimi japo sijui sheria yaani ugonge gari langu halafu ulipe faini polisi halafu upite hivi..aaah haiwezekani..utanilipa japo kidogo...

Ngoja wajuzi waje zaidi
 
Ukimgonga mtu kwa nyuma wewe ndio una makosa. Kama una insurance hata third party subiri trafiki aje apime mfuate taratibu insurance yako imtengenezee au kama ana comp insurance itamtengenezea.

Ukimgonga mtu ukiona matengenezo gharama sana subiri trafiki aje insurance italipa.
 
dereva anaendesha magari 3
1. la kwake
2. mbele yake
3. la nyuma yake
hapo sasa ukigonga gari kwa nyuma ww ndo mwenye makosa chakufanya ita wahusika wapime alafu bima ya gari itamalizana mbele kwa mbele na alieumia
 
Kuna nafasi imewekwa kisheria kati ya gari moja na lingine. Sikumbuki ni mita ngapi, ila nadhani ni mita 20. Sina uhakika.

Kwa maana hiyo ukiligonga gari la mbele yako, ina maana hukuzingatia taratibu na sheria za ile nafasi. Kwa maana hiyo unakuwa una kosa.
 
Mita 20..!!! Ingekuwa balaa.
Ni mita nne tu
 
Ukimgonga mtu kwa nyuma wewe ndio una makosa. Kama una insurance hata third party subiri trafiki aje apime mfuate taratibu insurance yako imtengenezee au kama ana comp insurance itamtengenezea.

Ukimgonga mtu ukiona matengenezo gharama sana subiri trafiki aje insurance italipa.
name umenifumbua masikio,asante kaka kwa maelezo yako mazuri. kwenye masuala ya magari wewe ni king
 
Habari za leo wanajamvi,kuna utata naupataga kwenye hili swala,labda wajuzi wa sheria za usalama barabarani watatusaidia,....
Mara nyingi inajulikana kuwa ukigonga gari lingine kwa nyuma inakuwa kwamba ww mgongaji ndio una kosa,je ni sheria ww ngongaji ndio utengeneze gari la mwenzako?,i mean sheria hasa za usalama zinasemaje?,maana wengine wanasema kuwa bima ndio zinatengeneza gari zote mbili,je unaweza kukomaa na mwenye gari ili ulipe faini ya polisi then kila mmoja akatengenezewe gari lake na kampuni ya bima?,...hapo naongelea Third part insurance.Naomba wataalam wa sheria za barabarani watusaidie.
Kama ulivyosema wa nyuma ndie mwenye kosa. Hivyo bima ya wa nyuma ndio itagharamia matengenezo ya gari zote.
 
Ajali itapimwa na askari mwadilifu kisha mpelekwa mahakamani, aliegonga gari kwa nyuma atapigawa faini ya uzembe na uharibifu kisha bima yake itahusika na matengenezo ya gari
 
Inategemea na scenario ya ajali kama wa mbele yako ameingia barabara kuu ndio ukamgonga....kama umbali toka alipoingilia hadi ajali ilipotokea ni chini ya mita 25(kama sijakosea) hapo gari ya mbele ina makosa...ila kama zipo zaidi ya hzo gar ya nyuma ina makosa,kama wote mpo njia moja wa nyuma ana makosa.Swala la malipo inatakiwa kulipwa na bima ila mlolongo ni mrefu unahusisha kwenda mahakamani ndio maana wengi tunaona bora kumalizana tu ili kupusha kupoteza muda.(nisahihishwe nilipokosea).
 
Mkuu mimi japo sijui sheria yaani ugonge gari langu halafu ulipe faini polisi halafu upite hivi..aaah haiwezekani..utanilipa japo kidogo...

Ngoja wajuzi waje zaidi
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Usiondoke eneo la tukio mpaka polisi waje wapime atalipwa na bima.
Angalau umefungua njia kidogo mkuu,je hio ipo kisheria kabisa?...I mean akienda bima atalipwa hata km ana third part?
 
Ukimgonga mtu kwa nyuma wewe ndio una makosa. Kama una insurance hata third party subiri trafiki aje apime mfuate taratibu insurance yako imtengenezee au kama ana comp insurance itamtengenezea.

Ukimgonga mtu ukiona matengenezo gharama sana subiri trafiki aje insurance italipa.
Asante mkuu,ndo maana nilikutag maana najua speech zako zinaekeweka,....ila cjaelewa hapo.....VP km wote wawili mna third party insurance?
 
dereva anaendesha magari 3
1. la kwake
2. mbele yake
3. la nyuma yake
hapo sasa ukigonga gari kwa nyuma ww ndo mwenye makosa chakufanya ita wahusika wapime alafu bima ya gari itamalizana mbele kwa mbele na alieumia
Yes nafahamu hilo LA kuendesha magari ma3 mkuu,ila kibinaadamu tu huwa kuna wakati viajali vidogo vidogo vinatokea,....nimeuliza maana kuna mshikaji wangu aliigonga BMW X5 ya mtu, akavunja taa zote za BMW na kuiharibu sura yote ya BMW,jamaa alikubali kosa na hv sasa anadaiwa madeni mtaani karibu 3m aliyokopa kutengeneza BMW,ndo maana nikaona niulize,na ile BMW ilikuwa na comprehensive insurance lkn jamaa alikataa katukatu na kutaka gari yake itengenezwe.
 
Ukimgonga mtu kwa nyuma wewe ndio una makosa. Kama una insurance hata third party subiri trafiki aje apime mfuate taratibu insurance yako imtengenezee au kama ana comp insurance itamtengenezea.

Ukimgonga mtu ukiona matengenezo gharama sana subiri trafiki aje insurance italipa.

Mpaka Mahakamani baada ya hukumu ndipo Insurance italipa sio otherwise japo kibongo bongo jamaa anakupoza nawe unampoz Trafiki anaandika aliekugonga kakimbia unaenda Bima wnakuandikia upeleke Gari kwa Mchina nae huko anaongeza Gharama za Matengenezo cha juu anampa 'veko' wa Trafiki na Yule Afisa wa Bima then mnamalizana, ni mwendo wa kugawana Umaskini!

Niliwahi kupata ajali nikastukia dili kwa Wachina baada ya kugundua Matengenezo waliyoandika ni karibu Mara mbili ya yake halisi nilikomaa mpaka wakaniachia Kama laki mbili na nusu nami ya kupoza Machungu
 
Back
Top Bottom