Sheria inasemaje ukigonga gari kwa nyuma?

Habari za leo wanajamvi,kuna utata naupataga kwenye hili swala,labda wajuzi wa sheria za usalama barabarani watatusaidia,....
Mara nyingi inajulikana kuwa ukigonga gari lingine kwa nyuma inakuwa kwamba ww mgongaji ndio una kosa,je ni sheria ww ngongaji ndio utengeneze gari la mwenzako?,i mean sheria hasa za usalama zinasemaje?,maana wengine wanasema kuwa bima ndio zinatengeneza gari zote mbili,je unaweza kukomaa na mwenye gari ili ulipe faini ya polisi then kila mmoja akatengenezewe gari lake na kampuni ya bima?,...hapo naongelea Third part insurance.Naomba wataalam wa sheria za barabarani watusaidie.

Umeshamaliza makato yako ya Mkopo wa hilo Gari Mkuu?
 
Kuna nafasi imewekwa kisheria kati ya gari moja na lingine. Sikumbuki ni mita ngapi, ila nadhani ni mita 20. Sina uhakika.

Kwa maana hiyo ukiligonga gari la mbele yako, ina maana hukuzingatia taratibu na sheria za ile nafasi. Kwa maana hiyo unakuwa una kosa.
Kwenye foleni mita 20 au umemanisha mm?
 
Hehehee! Imebidi nicheke. Hilo swala la umbali salama kati ya gari moja na lingine barabarani ni debate ya muda mrefu, na mpaka sasa hakuna jibu sahihi kutokana na sababu nyingi tofauti tofauti kama zifuatazo
1. Road conditions - (good roads, rough roads, mjini au highway etc)
2. Spidi kati ya gari moja na lingine
3. Aina ya gari na braking distances (mfano, gari dogo linaweza simama mapema kuliko kubwa, magari ya kisasa yana braking technologies zinazoweza saidia likasimama umbali mdogo saana kuliko ya kizamani)

Wataalamu wanashauri kutumia muda wa sekunde kupima huo umbali salama. So unapokua kwenye mwendo kasi wa kati ya 50kph to 90kph hakikisha unaacha muda wa sekunde 2 mpaka 3 kati ya gari lako na la mbele. Kwa 90kph to 120kph sekunde 4 mpaka 5. Ikizidi hapo, au wakati mvua inanyesha, jiwekee angalau sekunde 7 mpaka 8. Upimaji wa hizo sekunde ndio balaa jingine.
 
Mpaka Mahakamani baada ya hukumu ndipo Insurance italipa sio otherwise japo kibongo bongo jamaa anakupoza nawe unampoz Trafiki anaandika aliekugonga kakimbia unaenda Bima wnakuandikia upeleke Gari kwa Mchina nae huko anaongeza Gharama za Matengenezo cha juu anampa 'veko' wa Trafiki na Yule Afisa wa Bima then mnamalizana, ni mwendo wa kugawana Umaskini!

Niliwahi kupata ajali nikastukia dili kwa Wachina baada ya kugundua Matengenezo waliyoandika ni karibu Mara mbili ya yake halisi nilikomaa mpaka wakaniachia Kama laki mbili na nusu nami ya kupoza Machungu
Sio lazima mpaka mahakamani. Kama una comp insurance kuna form sikumbuki namba ngapi ukiipata tu hio unaanza kutengenezewa gari. Nafikiri third part ndio hadi hukumu itoke.
 
Asante mkuu,ndo maana nilikutag maana najua speech zako zinaekeweka,....ila cjaelewa hapo.....VP km wote wawili mna third party insurance?
Mkiwa na third party aliegonga itabidi agharamie matengenezo ya gari yake. Third party ina-cover utakaowasababishia madhara wewe mwenyewe utajijua.
Kwa maana hii ukiwa na third party ukanigonga na una makosa insurance yako itanitengenezea mimi na wewe utajigharamia. Hapa ndio hukumu ya mahakamani ni lazima.
 
Back
Top Bottom