Sheria inasemaje pale mtu anapokutwa na hatia?

Konseli Mkuu Andrew

JF-Expert Member
May 10, 2013
740
855
Salaam Wakuu,

Niende kwenye maada tajwa hapo juu.

Nafahamu kwa sheria za Tanzania Mahakama ndiyo imepewa mamlaka ya kumkuta mtuhumiwa na hatia na si chombo kingine.Swali langu ni kuwa Mahakama baada ya kumpa kifungo huyo aliyekuwa mtuhumiwa kuna namna yoyote na kutunza mali anazoziacha kama nyumba, viwanja, gari n.k hadi pale kifungo chake kitakapo kwisha?

Maana kuna msemo upo huku mtaani kuwa mtu aliyetoka jela huwa kama na laana au mkosi fulani mana huwa hana ramani yoyote pindi atokapo jera nami nipingana na huu msemo wafungwa wengi wanapofungwa mali wanaziacha huwa zinapotea potea hovyo hovyo maana waliobaki huwa na uhuru wakijua hawezi kutoka tena na matokeo yake huwa ni wakati mgumu pindi wafungwa hao
wanapomalizia vifunngo vyao.

Kuna umuhimu sasa tuwe na sheria inayoipa Mahakama jukumu ya kutunza mali zinazoachwa na wafungwa kama mhusika atakubali iwe hivyo.
 
Hii ni kweli kabisa suala hili ni vizuri tuliangalie kwa makini ili tutokomeze umasikini endelevu

Mtu akitoka jela tu anakuja kuanza moja uswahilini
 
Hii ni kweli kabisa suala hili ni vizuri tuliangalie kwa makini ili tutokomeze umasikini endelevu

Mtu akitoka jela tu anakuja kuanza moja uswahilini
Yeah mkuu inatakiwa mtu akikutwa na hatia awe anaulizwa pale pale Mahakamani kama atataka jukumu la utunzwaji wa mali zake liwe chini ya Mahakama hadi atakapo maliza kifungo chake ili kuwapa fursa wanapotoka wawe na pa kuanzia.
 
Mimi naona baada ya hukumu mtuumiwa aiombe mahakamani mali zake ziwe sehemu ya pato la serikali au taasisi yeyote ya kiserikali mpaka mwisho wa uhukumu yake.

Pamoja na kutoa mwongozo endapo atapatwa na umauti mali zake ziende wapi.
 
Mfano mme kafungwa miaka 6, je mke anaweza kufanya maamuzi ya kuuza mali ya mfungwa kama nyumba au gari bila makubaliano
 
Mfano mme kafungwa miaka 6,je mke anaweza kufanya maamuzi ya kuuza mali ya mfungwa kama nyumba au gari bila makubaliano
Naona hiyo ipo hapa huku uswahili maana tunapenda kurahisisha mambo yaani ukienda jela na lako limekwisha
 
Mfano mme kafungwa miaka 6, je mke anaweza kufanya maamuzi ya kuuza mali ya mfungwa kama nyumba au gari bila makubaliano
Shukuru hata kauza gari, wengine miaka 6 wakitoka wanakuta mke kashaolewa tena na ana watoto kama wanne.
 
Back
Top Bottom