Sheria ikoje hapa tafadhali nisaidieni

Sheria ikoje hapa tafadhali nisaidieni

Kampungapunga

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2018
Posts
313
Reaction score
1,100
Wadau nauliza mnisaidie hivi sheria ikoje inapotokea umemfumania mkeo live na jamii ikajua, ukaamua kuachana na mwanamke wako. Je? mtagawana mali zote ulizovuna naye au atabeba msaraba wake kwakua yeye ndo msababishi.

Naomba majibu kwa wanaojua tafadhali.
 
Inabidi upige picha akiwa anavunja amri ukiwa na mashahidi then nenda mahakamani kadai taraka.
 
Kama ni mke wa ndoa mkiachana kisha mkienda Mahakamani mtagawana mali ambazo mmechuma mkiwa pamoja 50/50 lakini mali alizokukuta nazo hazimuhusu ktu vilevile ukiishi na KE miaka 2 Kisheria anahesabika kama Mkeo so naye mtagawana kama Mke wa ndoa
 
Wadau nauliza mnisaidie hivi sheria ikoje inapotokea umemfumania mkeo live na jamii ikajua, ukaamua kuachana na mwanamke wako. Je? mtagawana mali zote ulizovuna naye au atabeba msaraba wake kwakua yeye ndo msababishi.

Naomba majibu kwa wanaojua tafadhali.
Mkuu,
Anataka kugawana nini, alifanya hivyo ili agawane?
Kwanza una haki ya kumnyang'anya hata nguo ulizonunua aende!
Wewe ulikuwa unaendesha maisha nae kwa amani yeye Ame default mkosaji kisheria hana fidia.
Akitaka wapeleke wote mahakamani kama wazinzi na mwanaume umdai fidia na achukuwe mzigo wake huutaki tena.
 
Nadhani hukumu yake ni kitu kama faini isiozidi elfu sabini.
 
Kabla ya kuvunja ndoa lazima kuwe na sababu na ili sababu zako ziwe na mashiko mahakamani ingekuwa vizuri utafute mwanasheria akueleweshe na akuandikie vizuri maana kama ni umemfumania kuna sababu nyingi unaweza kuziandika ambazo katika ugawaji wa Mali ukapata kikubwa kuliko yeye ila pia mahakama inaangalia kama mna watoto pamoja kwaiyo Mali zitagawanywa kwa kuangalia VP watoto watapata mahitaji yao hasa elimu na malezi
 
Back
Top Bottom