Sherehe za uchumba na send off ni kwa ajili ya nani?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,597
46,224
Kuna umuhimu wowote au mantiki ya kufanya shere ya uchumba na send off kwa watu walioishi muda mrefu pamoja kama mume na mke na kupata watoto kabla ya kuoana kidini?

Hili jambo ni kama aina fulani ya kufuata mkumbo wa jamii tu bila kushirikisha vichwa vizuri. Haiingi akilini kabisa.
 
Mkuu siku hizi mambo mengi yanafanywa kwa kufuata mkumbo tu hata hizo ndoa zenyewe nyingi ni za kufuata mkumbo

Inasemekana eti hata shela jeupe ilikuwa ni mahususi kwa ajili ya mwanamke anayeolewa akiwa bikira lakini siku hizi hata mwanamke aliyekwishazaa anapoolewa anavaa tu imeshakuwa kama utamaduni
 
Hayo mambo bado yapo? Au tunasubiria serikali iingilie kati?.
😂

Jirani yangu alikuja kuomba mchango wa harusi yake, mkewe akaja kwa mama watoto kuomba mchango wa kitchen party, sendoff na ubatizo wa watoto wao na sherehe ilikuwa inafanyika siku hiyo moja
 
Mimi kama Master of Ceremony (MC) naweza nikakujibu kwamba, kwa watu walioishi pamoja hakuna mantiki yyte kufanya sherehe ya uchumba (engagement party) mnavishana Pete leo wakati mmeshajuana nje ndani, mmeshafyatuana staili zote zinazopatikana sayari hii.......kwa maoni yangu (na huwa nawashauri na wengine) hizo gharama za kuandaa hiyo sherehe ni bora wangepewa hawa wakaenda kufanyia mambo mengine ya ustawi wa familia yao.

Hawa wa Send off party, sio mbaya kufanya maana ni sherehe ya kumuaga rasmi mtu kutoka kwenye familia yao kwenda kuungana na familia nyingine

Ila
Ila
Ila
Ila........kama mnaona mfuko hauruhusu kufanya ivo sio mbaya mkaipotezea tu, au familia za pande zote wakaunganisha nguvu wakafanya sherehe moja tu ya ndoa takatifu
 
Back
Top Bottom