Sherehe za miaka 50 uhuru zina umuhimu gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sherehe za miaka 50 uhuru zina umuhimu gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by koo, Nov 5, 2011.

 1. koo

  koo JF-Expert Member

  #1
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wana jamvi heshima mbele.

  Naomba msaada kwa yeyote mwenye kuelewa nini mantiki ya kutumia pesa za walipa kodi kusherehekea miaka hamsini ya uhuru inatufaidisha nini na kuongeza nini inaelimisha nini na inalengo gani katika mkakati wa kukuza uchumi na kuondoa umasikini?

  Nimejiuliza sana pasipo kupata majibu wizara, Taasisi za uma, mashirika, mikoa na wilaya zote wanaadhimisha kwambwembwe na gharama kubwa najiuliza pasipo majibu je itatusaidia nini kutuonyesha posta ya mwaka 1970 kisha unatuonyesha posta ya mwaka 2011 tunafaidika na nini au kutuonyesha uzinduzi wa kiwanda miaka ya sabini inatusaidia nini? kwamawazo yangu hivi vitu vya kale wangeweza kuviweka maktaba watu waende kuvisoma huko kuliko kufuja pesa kutuhubilia miaka hamsini ya uhuru sijui wa nchi gani kwani tanganyika ilishakufa na kwaninavyo fahamu mimi tamaduni nikukumbuka siku ya kufa na sio siku ya kuzaliwa kwa kitu au mtu aliyekwisha kufa hata baba wa taifa tunakumbuka na kuheshimu siku yake ya kufa sio yakuzaliwa.

  Tanganyika ilishakufa iweje tunakumbuka siku yakuzaliwa kwake badala siku yakufa kwake? Jamani nisaidieni kwa wale mnaoelewa sababu za msingi kwa serikali kushupalia hii miaka hamsini ya uhuru nizipi? na je zinaendana na gharama zinazo tumika?

  Wizara ya kazi ilitumia milioni 120 kuhadhimisha miaka hamsini ya uhuru nini faida yake?
   
 2. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #2
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Tanzania ni nchi masikini lakini si kiasi cha kutosherehekea sherehe zetu za kitaifa. Kila nchi duniani ina siku yake ya kuzaliwa na inasherehekewa ipasavyo. Labda ungeleta hoja nyingine lakini kwa hili sidhani kama una pointi.
   
 3. s

  sanjo JF-Expert Member

  #3
  Nov 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Ni njia nyingine ya kufisadi hazina yetu. Tatizo la nchi hii tu wazuri sana katika kutumia (consumption) kuliko kuwekeza (investment). Bila kuwa na vipaumbele na uongozi wenye kuona mbali tutaendelea kudumaa tu kama siyo kurudi nyuma.
   
 4. koo

  koo JF-Expert Member

  #4
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Miaka yote tunasherehekea vizuri tena kwa gharama nafuu kwa siku moja na pasipo kuhubiri mwaka mzima nani asiyejua tunatimiza miaka hamsini ya taifa lisilokuwepo? Hatuna haja kupoteza muda kusimamisha shughuli muhimu eti kuhubiri miaka hamsini ya uhuru sijaona sababu kutumia mwaka mzima kwa shughuli isiyo na tija
   
 5. koo

  koo JF-Expert Member

  #5
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Naungana na wewe tumekua mafundi sana wakutunga shughuli zisizo na tija mladi zinaingiza pesa mimi nimeshaudhulia washa na semina nyingi zakihuni zenye mada zisizo jenga mladi waandaaji wajipatie chochote na hii imepelekea watendaji wengi kujikita kubuni shughuli zitakazo waingizia pesa pasipo kuongeza tija kiutendaji. Nadiliki kusema huyu aliyeleta wazo lakutumia mwaka mzima kuhubiri miaka 50 ya uhuru namashaka na uwezo wake wa kufikiri
   
 6. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #6
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Tunasherehekea miaka 50 ya uhuru. uhuru wa nchi gani? acha uliza uliza bana! Sema miaka hamsini ya uhuru inatosha. Kwani hujui Tanzania bara a.k.a Tanganyika?
   
 7. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #7
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  miaka hamsini ya nchi gani hiyo,mkuu nyiye watanzania v.i.l.aza kweli.
   
 8. koo

  koo JF-Expert Member

  #8
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha kukurupuka wewe Tanganyika ilishakufa kitambo sana na hakuna serikali ya tanganyika sasa uliwahi kuona wapi nchi ambayo haina serikali tanzania bara sio nchi na hakuna serikali ya tanzania bara sasa nchi gani isiyo na utawala wala wananchi kwasababu sijawahi kuona mwananch wa tanzania bara.
   
 9. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #9
  Nov 5, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lakini kweli naanza kuelewa sasa. Hivi tunasherehekea uhuru wa nchi gani ikiwa Tanganyika iliungana na Zanzibar kupata Tanzania? Huu undumilakuwili utaisha lini au ndiyo tuseme muungano ni hewa tu.
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Hapo utaambiwa sherehe imegharimu bilioni tano, kumbe tatu zimemegwa kapewa ridhiwani kuendeleza biashara za baba. ****** amelaaniwa sana.
   
 11. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #11
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  kama za EPA zimefanywa vile sembuse hizi za ubwete zisizo na shaka, acha kabisa hii nchi imeisha
   
 12. K

  Kiluvya2011 JF-Expert Member

  #12
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamani hakuna mtu anayeweza ashinza harakati za ukombozi?...maana inchi bila kuondolewa kwa utawala wa ccm hatutaendelea kamwee
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  kwa taarifa yako tu hii ni topic muhimu. haihitaji majibu mepesi mepesi mithili ya waimba taarabu.

  nenda library uje na nondo au ukae kando watu watoe hoja.
   
 14. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #14
  Nov 5, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,795
  Trophy Points: 280
  Unaonaje hizi gharama kubwa za kusheherekea miaka 50 ya uhuru ziwekezwe kwenye mpango wa kuimarisha uchumi wa TZ kama ilivyopendekezwa na World Bank thidi ya kuporomoka kwa shilingi ya Tz??
   
 15. koo

  koo JF-Expert Member

  #15
  Nov 5, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inabidi kujiuliza kwa kina zaidi haya maadhimisho yanafaida gani kubwa kwa taifa yanaleta nini hadi kughalimu wananchi mamilioni ya shiling na mahubiri yasiyokwisha leo kunaofisi ukienda unakosa huduma eti watendaji wako kwenye maadhimisho ya miaka hamsini ya uhuru kumbe wanatumbu pesa za umma pasipo sababu jamani tuamke mambo haya hayana tija tuyaache.
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Wizara ya fedha walikata kama wiki mbili pale mnazi mmoja uku wakiwachezesha dance watoto wa Jitegemee Sec School wale kama sikosei meanwhile uchumi wa nchi unasua sua!
  Am sure ukijumlisha ela zote watakazotumia zitafika mabilioni kadhaaa
  Ivi na hawa donors hawaoni haya na bado wanaendelea kutoa misaada?
   
 17. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #17
  Nov 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mimi ninajiuliza mwenyewe, hivi tunasherekea miaka hamsini ya uhuru wa nchi gani?
  kwa kweli bora kuwa maskini lakini ukawa na shule kichwani!!! Most of Watz hawana shule vichwani dat y!! wananchi tupo tupo tu ili mradi. Sorry jamni.
   
 18. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #18
  Nov 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,548
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Ni usanii mtupu!!! Tanzania haikuwahi kuwa koloni la Taifa lolote duniani. Wakisema tunaasherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika hapo wataeleweka badala ya kuendeleza huu usanii kwa miaka 50 sasa.
   
 19. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #19
  Nov 5, 2011
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Haijalishi kuwa miaka 50 ya Tanganyika au Tanzania, suala muhimu ni je kuna ulazima wa kutumia gharama kubwa kufanya sherehe hizo? Kwa nini tusisherekee kama kawaida hiyo siku ya 9 December? Sasa hivi kila taasisi na idara za serikali zote zinagharamia hizo sherehe tena sio siku 2 au 3 ni muda mrefu! Hapo hapo tunalalamika hazina ya serikali iko hoi, serikali inakabiliwa na madeni from left, right and centre! Watu wapo tu wanashindana kutumia pesa ovyo kucheza ngoma!
   
 20. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #20
  Nov 5, 2011
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Zina umuhimu wa kujipima kama kweli kuna linaloridhisha kutokana na UHURU. Miaka yote hii lakini bado tunahitaji misaada hata kuendesha nchi yetu. Ule Uhuru tuliosoma shule na college hatujaufikia na kwa mienendo iliyopo hivi sasa tutakuwa tegemezi hata kama ikifika miaka mia. Tumekuwa sana tukijali quantity bila ya kujali quality. Mwalimu Nyerere alisema"KUPANGA NI KUCHAGUWA" Sisi hadi leo hatjajipanga. Yapasa tujipange.
   
Loading...