Malick M. Malick
JF-Expert Member
- Apr 2, 2013
- 658
- 312
MIAKA 63 ya UHURU na 4R za Rais SAMIA
Na MALICK MALIKI,Chamwino,DODOMA
Nelson Mandela aliwahi kusema ‘’Fedha haziwezi kutuletea mafanikio,ila uhuru wa kuzitafuta ndiyo utakaotuletea maendeleo’’ pia baba wa Taifa Mwl J.K Nyerere aliwahi kusema maneno ya fauatayo ‘’Maendeleo ya kweli ndiyo msingi wa amani ‘’
April 26,2024 Rais wa Tanzania DR SAMIA SULUHU HASSANI akihutubia wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wakati wa kilele cha sherehe za miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa uhuru Dar es salaam aliwataka watanzania katika kutekeleza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulioasisiwa mwaka 1964 watanzania hatuna budi kutekeleza kwa vitendo falsafa ya 4R
Rais Samia ameutambulisha uongozi wake ndani ya ulimwengu wa falsafa yake ya R nne [4R] zikiwa na maana ya Maridhiano[Reconciliation ],Mabadiliko [Reforms],Ustahamilivu[Resilience] na Kujenga upya [Rebuilding]
Rais wetu alilisitiza kuwa watanzania tukiziishi hizi falsafa za 4R hayo ndio yatakayo endelea kujenga amani na utulivu wa kudumu nchini kwetu na kuleta maendeleo endelevu .
Rais wetu mama Samia kwa nyakati tofauti ,amekua akisisitiza wasaidizi na watendaji wa serikali na viongozi wa chama cha mapinduzi [CCM] kusimamia 4R katika utekelezaji wa majukumu yao ,akisema ndiyo mwelekeo wa kujenga Taifa lenye umoja na mshikamano
Pia leo tukiwa kwenye kumbukumbu ya miaka 63 ya uhuru wa Tanganyika Rais ametoa ujumbe kupitia mitandao ya kijamii akiwatakia heri watanzania na mnukuu’’ Kheri ya Miaka 63 ya uhuru kwetu sote .Tutumie siku hii njema kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hatua kubwa tunazoendelea kupiga kimaendeleo kama Taifa .
Tujivunie ,na kwa Pamoja tuendelee kufanya kazi ya kuzilinda na kuzitunza tunu za AMANI ,UMOJA na MSHIKAMANO ambazo ndizo nguzo za mafanikio yetu
Watanzania wenzangu sote tunajukumu la kuzilinda 4R katika Maisha yetu ya kila siku,kila mtanzania akiishi kwenye falsafa hizi za 4R utailinda amani,tukilinda amani tunapata nafasi ya kuendeleza nchi yetu kwa maendeleo na pia maendeleo binafsi,kukiwa na amani ,Watoto wetu watasoma kwa utulivu,wafanya biashara watafanya baishara,wagonjwa watapata matibabu kwa utulivu ,tutakua huru kutembea kokote kufanya shughuli za maendeleo waswahili wana msemo wao ’’ bora ugali dagaa kwenye amani kuliko wali nyama vitani’’ kauli hii kila mtu atafakari
Watanzania wenzangu tuzitafakari pia nukuu ya Mzee Mandela amesema ukiwa huru ndio unakua huru kutafuta fedha [Maendeleo] na Baba wa Taifa kasema maendeleo ya kweli yapo kwenye amani
Kila mmoja amsisitize mtanzania mwenzake kuziishi 4R kila ukitaka kufanya jambo lolote wafikirie watanzania wenzako katika miaka 63 ya uhuru wetu ,je jambo lako unalofanya linailinda amani yetu ,ukiona alilindi amani liache.
# TUITUNZE AMANI YETU KWA WIVU MKUBWA ,AMANI YETU ndio UHURU WETU