Yaleyale ya CCM "yenyewe" huko nyumbani.UBISHI na kuona kila anayewakosoa ni adui wa "umoja na mshikamano wa kitaifa (kifisadi)".
Sawa,mie sio mwanachama mwenzenu lakini ni Mtanzania mwenzenu.Na ni kwa minajili hiyo ndio maana nawaeleza matarajio yetu kwenu wana-chama tawala mlio nje ya nchi.Hivi kweli kabisa mnajifanya hamuelewi,kwa mfano,kuwa ishu za rada,richmond,epa,kiwira,nk ni matokeo ya siasa za kulindana ndani ya tanzania?Hivi mnajifanya vipofu wa kufahamu kuwa Tanzania yetu haistahili kuwa hapo ilipo (masikini wa kupindukia) licha ya neema lukuki tulizojaliwa ikiwa pamoja na "upole wa walalahoi wanaoibia raslimali zao mchana kweupe kwa kisingizio cha uwekezaji"?
Uhuru bila wajibu ni upuuzi.Na japo mna uhuru wa kuwa wanachama wa chama chochote kile,hata ingekuwa BNP,lakini mishipa yenu ya aibu (kama ipo na inafanya kazi) inapaswa kuwajibika as well as brains zenu.Kinachowafanya muonekane vituko ni umahiri wenu wa kutuwekea mipicha yenu ya kila kikao badala ya ku-address nini chama chenu kilifanyie taifa.Nyie ni wasaliti wa Watanzania wenzenu.Na msijilinganishe na wana-CCM walioko nyumbani kwa vile wao bado wako kizani.Ninyi mmebahatika kuwa nje ya kiza hicho,lakini unfortunatelymmebakia kuwa so much obsessed na kuonekana kwenye picha mkipeana mikono na viongozi kuliko kusaidia uboreshaji wa CCM from makucha ya mafisadi into chama cha kuwatumikia Watanzania.
Vox populi vox dei,ndugu yangu.Hamjiulizi kwanini wengi wetu tunawashangaa?
Kaka you made my day nimecheka sana hahahaha!!! Umenikumbusha mbali tangu nilipokuwa sekondari safi sana