Tuzo za Pongezi kwa Viongozi wa UWT Taifa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941

TUZO ZA PONGEZI KWA VIONGOZI WETU WA UWT TAIFA

Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) na Makamu Mwenyekiti wa UWT Ndg. Zainab Khamis Shomari (MNEC) tarehe 01 Disemba 2023 wamepokea Tuzo za Pongezi kutoka kwa Viongozi wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kuwapongeza viongozi hao kwa uongozi wao katika kipindi cha mwaka mmoja.

"Katika kipindi cha siku 365 mimi pamoja na viongozi wa UWT tumejitahidi kuyafanyia kazi maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa.

"Kupitia kazi zilizofanywa na UWT ngazi mbalimbali Tawi, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa tumeweza kuingiza wanachama wapya wa UWT takribani 514,882 kwa kipindi cha kuanzia Disemba 2022 - Septemba 2023" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

"Mikoa iliyofanya vizuri sana kuongeza wanachama wa UWT ni Dar es Salaam, wanachama 40,046. Kagera, wanachama 35,936. Arusha, wanachama 25,801 na Tanga, wanachama 23,418. Naipongeza sana mikoa hii kwa kazi nzuri wakiongozwa na Dar es Salaam" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

"Idadi ya wanachama wapya wa UWT ni ongezeko la zaidi ya asilimia 596.7 kulinganisha na wanachama wapya 86,288 walioingia kwa kipindi cha 2017-2022. Hali hii inaonyesha uimara wa Jumuiya yetu na mapenzi ya wanawake kwa UWT. UWT moto moto" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

"Tumeweza kufanya ziara ya kujitambulisha katika Mikoa na Wilaya na Kata za Dodoma, Tanga, Mjini na Kaskazini Pemba Zanzibar, Dar es Salaam na Mwanza. Jumla ya Mikoa 6, Wilaya 10, Kata 25 na wadi 2 mara baada ya kuchaguliwa" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

"Tumeweza kufanya ziara za kazi katika Mikoa ya Njombe, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Singida, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kagera, Kaskazini Pemba, Kusini Pemba, Mjini, Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja na Dodoma" - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

"UWT imefanya ziara kwenye Jumla ya Mikoa 17, Wilaya 75, Kata 848 na Wadi 96. Hivyo kufanya Mikoa ambayo tumefika kwa kujitambulisha na pia kufanya ziara kufikia Mikoa 20, Wilaya 85 na Kata 873, Mikutano ya hadhara 848 - Ndugu Mary Chatanda, Mwenyekiti UWT Taifa

UWT IMARA. JESHI LA MAMA. KAZI IENDELEE.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 20.50.41.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 20.50.41.jpeg
    199.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 23.36.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 23.36.01.jpeg
    188.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 23.37.40.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 23.37.40.jpeg
    231.6 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 22.49.01.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 22.49.01.jpeg
    233.9 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 22.48.16(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 22.48.16(1).jpeg
    173.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-12-01 at 20.50.39.jpeg
    WhatsApp Image 2023-12-01 at 20.50.39.jpeg
    560.7 KB · Views: 1
Safi sana UWT

Sasa mna jukumu la kuwalea mabinti zenu ili na sisi vijana tushawishike kuoa. Mnaongeleaje ongezeko la single mothers mtaani?

Tumechoka kampeni za kataa ndoa na kujichukulia sheria mkononi. Pia mkalisheni chini mkuu wa mkoa mmpe madhara ya kuvunja madanguro.
 
Back
Top Bottom