Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Wakuu,
Sijui kama kuna kitu sijaelewa ila naona kama taifa ni kama tumechanganyikiwa hivi au niseme tumepoteza muelekeo au ufahamu fulani.
Siku inapotengwa kitaifa kumuenzi mtu fulani maana yake siku ile inatakiwa kutumia kutafakari, kujadiliana na kuenzi mafundisho mema ya yule tunayemuenzi.
Sasa nashangaa kuona msururu wa viongozi ukienda Chato badala ya Butiama. Sioni viongozi na taasisi mbalimbali zikiandaa mijadala ya kuhusu mafundisho ya Nyerere.
Hii haitakiwi kuwa siku ya kwenda beach tu au kuangalia tu mpira. Kama fikra za Nyerere zinaonekana zimepitwa na wakati, au viongozi wanaona haya kumuenzi basi hii sikukuu ifutiliwe mbali. Wanaotaka kumuenzi watafanya hivyo kwa namna yao.
Kingine, siku ya kumuenzi ilitakiwa iwe siku yake ya kuzaliwa na si siku ya kufa maana alikufa kifo cha kawaida (tunavyofahamu sisi) ila hilo nitaliacha kwa mjadala mwingine.