Shemeji .
Sisi familia still yet tunakutambua wewe ndiyo mume wa dada yetu .
Pamoja na hilo Shemeji , umekua ukimtesa mno dada yetu , na ukware wako .
Mara kadhaa mkeo katuletea mashtaka yako ya ukware , tukakaa vikao na mkeo aka'submit ushahidi uliokubana kila idara , na unakosa pakuchopokea .
Kinachotuskitisha Sie familia ya mkeo , badala upangue hoja ziletwazo vikaoni na mkeo , wewe unasambaza habari kwa ndugu , majirani , marafiki, eti Dada yetu na sie tunakunyanyasa na kukudhalilisha eti kwa vile wewe na mkeo mnaishi ktk moja ya nyumba ya familia yetu .
Shemeji wewe kuishi kwenye nyumba yetu na mkeo , kunahusiana nini na umalaya wako?
Ukafanye uasherati huko , kisha mkeo akuheshimie ? Eti usiguswe !
Ukiguswa tu , kosa! Unanyanyaswa!
Shemeji hiyo defence mechanism tumeishaichoka!
Hebu badili gea (sio Gea Habibu) mpya !
Shemeji hukui ? Au mpaka utuulie Dada yetu ?
Jirekebishe Shemeji !
Acha hizo .