Shemeji yangu huyu ananitega!

yaani mmh! shemeji huyu tabia yake inanifanya nampenda zaidi ya sana kwakweli. Mbaya zaidi ni mrembo navutiwa nae hadi napitiliza, kwani ananionyesha upendo ambao hata mke wangu huwa hanionyeshi na sijawahi kuupata. Nampenda sana shemeji yangu, ila tu najilinda nisifanye dhambi ya kumtamani naku do nae!

Usiendekeza ee moyo utakavyo kutuma;
unadanganya jaribu kushinda;
usiposhinda huna budi kuumia;
utajitwika kilema pasipo kujua
Msondo Ngoma Band.

Bazazi ni Bazazi!
 
Mimi naishi na mke wangu na tumejaaliwa kupata watoto wawili. Shemeji yangu baada yakumaliza shule, kaja kuishi nasi nyumbani kwangu, nimemtafutia chuo na anasoma nakurudi nyumbani, lakini maisha yake yamenifanya nizidishe upendo kwake. Kwakuwa mke wangu nimfanyakazi huwa sanyingine anaondoka mapema nakuniacha mimi, mimi ni mfanyabiashara na huwa nasafiri maramojamoja mikoani hivyo nirudipo nyumbani toka mikoani nabaada ya kusambaza biashara zangu, muda mwingi huwa nachelewa kutoka nyumbani na saanyingine nakuwepo tu nyumbani kwaajili yakupumzika jioni ndo huwa natoka. Sasa shemeji yangu huwa ananisalimia kwakupiga magoti mpaka chini na kama hiyo haitoshi hunipelekea sabuni na mswaki aliouwekea dawa ya mswaki, kama hiyo haitoshi hurudi tena nakuniita kwa sauti ya upole, shemeji nenda kaoge tena akiwa amepiga magoti! Baada yakutoka kuoga nikiingia chumbani nakuta kitanda kimetandikwa kwa umaridadi na ameniandalia nguo ambazo nitavaa iwapo kama nitatoka, nakuta chai imeshatengwa mezani nakaribishwa kwakupigiwa magoti. Nanawishwa mikono kwa maji ya moto, chakula kinaombewa halafu nakaribishwa kwa sauti nzuri, yaani mmh! shemeji huyu tabia yake inanifanya nampenda zaidi ya sana kwakweli. Mbaya zaidi ni mrembo navutiwa nae hadi napitiliza, kwani ananionyesha upendo ambao hata mke wangu huwa hanionyeshi na sijawahi kuupata. Nampenda sana shemeji yangu, ila tu najilinda nisifanye dhambi ya kumtamani naku do nae!

ni kwambie kitu!!! jaribu kumueleza huo ujinga uliojengeka kichwani kwako, kama si wewe utakaekua unampigia magoti kumwomba asimwambie mama nani hii, hizo ni heshma tu. halafu hapo kwenye RED unapata wapi hiyo dawa ya mswaki? manake hata wangu unhitaji
 
Mie sina tatizo na mambo mengine kama 'kupigiwa magoti', 'kuwekewa sabuni bafuni' na kadhalika. Tatizo KUBWA nilionalo ni VIPI shemejio aingie CHUMBA CHAKO na kukutayarishia nguo za kuvaa weweeeeeee?

Yaani una kila dalili za kuibomoa ndoa yako, ila na huyo shemeji yako kwa nini anakuandalia mpaka nguo? ina maana kama si yeye na iwapo mkeo yu safarini nidada wa kazi huwa anaandaa au?

Kiukweli hapo unakosea kila kitu kina mipaka na huo mswaki anaupata wapi mpaka kukuwekea dawa? mambo mengine yanatia kichefuchefu kuhadithia hebu rudisha akili yako na uanze kufikiria kuwa na nyumba yenye master bedroom ila unakoelekea siko.

Na mkeo anajua kwamba mpaka nguo unaandaliwa na mswaki unatiwa dawa?? kama anajua na hakemei basi yeye ndie chanzo cha wewe kutamani kutoka nje ya ndoa.

Tafakari na uchukue hatua.
 
hebu usituletee tamaa za kijinga hapa.kupiga magoti kwa baadhi ya makabila ni kawaida sana hata hivyo naona mipaka ipo wazi sana au mkeo ni mvivu sana.amwangalie kuku wake atanyonyolewa manyoa maana ashaanza kumwagiwa maji ya moto ya tamaa..
 
Back
Top Bottom