Shemeji yangu anatongoza ovyo wadogo zangu.

Shemeji yangu anatongoza ovyo wadogo zangu.

Kwa kuwa yupo Idle hivyo muacheni apate mahali pakutuliza mawazo huku akingojea kupata kazi.
 
Hahahahaha! ni kicheko cha huzuni sio furaha...

Hivi kwa nini mumeo anakutupia wewe jukumu la kuongea na binti na si yeye kuzungumza na nduguye?

Jaribu kumuomba mumeo akae kitako na kakaye na ampe masharti ya namna ya kuishi kwake/kwenu.

Kama mumeo hatakuelewa mueleze mama yenu si mpo naye hapo
 
Mnaanzaje kuishi na mtu mzima aliyekuwa na maisha yake ndani ya nyumba yenu kwa muda usiojulikana? Hayo matatizo mnayataka wenyewe kati yako na huyo mume wako.

Muelezeni ukweli akatafute maisha mahali pengine ili na nyinyi muendelee kuyajenga maisha yenu. Yaani mnamkubalia mtu ale, aende chooni, aangalie tv huku miguu ikiwa juu ya meza! kirahisi rahisi tu! Hilo ni jambo lisilo wezekana kutokea kwenye familia zinazojielewa.
 
haya maisha ya hivyo kwa sasa hayapo kwa kweli!
kwa haraka haraka ndoa yako tu itakuwa na matatizo vinginevyo umeamuua kuwa mtumwa na kujitoa ufahamu kwa ajiri ya mume na watoto.
mmeo atakuwa anamsikiliza mama kuliko wewe na kwa lugha nyingine anachosema mama ndio final!
kwa lugha isiyoeleweka na wengi ipo ndoa kati ya mama na mtoto na kufanya huyo shemeji yako kuwa na uhalali wa kuwa hapo na hakuna unachoweza kufanya.
mama akiamua kijana aondoke ataondoka vinginevyo siku sio nyingi rangi za familia utaziona mengine nitakushauri pm kama iko wawzi
 
Mtoeni nduki maana ni FISI, baadae atakuna na wanao wakikua
 
Pole sana.
Hapo mi naona mtu wa pekee wa kushughurika nae ni huyo binti tu, kaa nae umpe ushauri madhara ya kuwa na uhusiano katka umri mdogo pia madhara ya kuwa na mahusiano na huyo shemeji yako. Mwisho muweke wazi akiwa na mahusiano au akipata mimba unamrudisha kijijini na uwe unaongea nae mara kwa mara. Ukimgusa shemeji yako utanzisha vita ya tatu ya dunia
 
Huyo atakua ni kiduku. ha ha ha. Ushauri wa kumpangishia sehemu utakufaa Sana.
 
Wanawake sijui mnakwama wapi yaan umeshindwa kumueleza haya yote mmeo unaelala nae kitanda kimoja et unakuja na speed ya supersonic jf..

Kwanza ni vizuri ukatambua ndugu wa pande zote hatakiwi kupewa samaki hale bali anatakiwa kupewa ndoano akavue samaki anakopajua yeye!...zaidi ya hapo subirini mmoja achomoe betri!
 
kila mgeni wa kike anayekuja hapo kwako mtaarifu kuwa huyo shemeji yako ni muathirika wa gonjwa sugu amekuja hapo mnamuuguza.
 
Hakuna kitu kibaya kama ngono na huo ni umaskini mbaya sana
Huyo akizidi kukaa hapo hata mwanao ipo siku ataanza kumfundisha akiwa bado mdogo kwani tabia haibadiliki

Mwambie ukweli aende akatafute sehemu ya kuishi na huo uwe msimamo wako kwa mume wako

La sivyo utakuja juta sana baadae najua wengi wanasema una wivu ila hawajui maumivu unayoyapata kwa kufuga FISI
 
Ni shida sana jitahidini kadri muwezavyo wewe na Mume wako mumpatie kazi za kufanya.
 
Kwanza hongera kwa kuweza kuishi na ukoo mzima
255768825726_status_6e290c13ae4c4692b712a1e5d540f1db.jpeg
 
Your next kwenye menu .....toeni mtu mzima huyo ataanza wagombanisha mmoja baada ya mwingine
 
Ongea na mume wako kama mama mwenye nyumba,mjibane vyovyote iwezekanavyo mumpangie sehem mbali na hapo kwenu akafie huko....Mkimuendekeza huyo atakuja kukutia mimba mpaka wewe mwenyewe.
Dooh!
Atatoa dose mpaka kwa mwenye nyumba[emoji23][emoji23]
 
Tatizo naliona kwa mumeo, mwambie awe mwanaume
Cha msingi ni kujitahidi huyo shemeji yako aondoke hapo, mwanaume anashindaje ndani akiangalia tv tu, si akabebe hata zege huko!!!
Zungumza na mumeo.
 
Fanyeni kikao cha familia...

Wewe, mmeo, binti na dada wa kazi.

Hapo hamna mawasiliano...unalalamika moyoni shemejiyo hayajui malalamiko yako.

Mwambieni kila kitu...mmeo awe mzungumzaji mkubwa maana ndiye baba mwenye nyumba. Mwelezeni uhalisia bila kuficha lolote.

Najua atanuna ataona kama mnamsimanga ila ndiyo ukweli.

Mabadiliko yakiwepo ni kheri...mkiona hayaonekani shemeji yako akaishi pengine mbaki na watoto. Mnaishije na baba wa watu??? Mzee kabisa tena ndugu wa mume...bora mngeishi na mdogo wako wa kiume sio kaka wa mume...wanajeuri na mila nyingi za kitanzania kaka wa mume ni sawa na baba mkwe ni mtu wa heshima.

Heshima za kimila sijui zinaenda wapi walai....mimi kabila langu hata mke wa mdogo wangu kwake nalamishwa kusubiri chakula. Na wazee wetu waliziweka hizi mila hivi walijua matokeo.
 
Back
Top Bottom