Shemeji ananitaka

Shemeji ananitaka

Hajanivutia na hata kama angekuwa anavutia kwasababu ni shemeji nisingeweza
Hivi unavyomuita SHEMEJI, yeye na huyo rafiki yako wameoana au wanakulana tu? Mi nnavyoelewa shemeji ni mtu ALIEOA ndugu yako. Otherwise hao saa yoyote wanaweza kuachana.. na kwavile wewe pia hujaolewa... unaeza shangaa huyo shemeji ndio anakuja kuwa mume wako.
 
Habari za muda mrefu wana jukwaa. Iko hivi nina rafiki yangu yeye ana mtoto mmoja yaani single mum, sasa ana mwanaume wake. Huyo mwanaume wake kipindi wanaanza mahusiano hata mimi nilikuwa nawaona mpaka sasa wamefikia kama miaka kadhaa ya mahusiano yao.

Huyu mwanaume siyo baba wa mtoto wake, sasa huyu shemeji kuna siku moja alichukua namba yangu nikiwa pale kwa rafiki yangu, yeye rafiki yangu alikuwa jikoni anapika, mimi nilijua kachukua kwa nia nzuri tu awe anakuja ofisini labda kuniungisha.

Sasa tulikuwa tunawasiliana akawa ananiita mke mdogo, mara ananiambia nimzalie mimi namwambia siwezi kufanya hivyo wewe ni shemeji yangu nakuheshimu, anasema kwani kuna ubaya. Mara kuna kipindi anakuja ofisini ananiambia wameachana na rafiki yangu mara warudiane.

Huyu shemeji nimemuona ni mtu wa ajabu sana kwa kitendo cha kunitaka kimapenzi kwani huko kote hajaona wanawake hadi aje kwangu, kwa rafiki wa mtu wake, wanaume hamna haya kabisa.

Mimi sijawahi kumwambia rafiki yangu na nimekata mazoea nao wote wawili, maana rafiki yangu akijua tu nilikuwa nachat na mtu wake atakasirika mno maana ana wivu balaa.
Cc. holoholo
Nomadix
Ndiyo umeamua unitangaze hadharani? Sasa utake usitake lazima tu utanipa kipochi manyoya na sitaacha ng'oo kukuomba kila siku.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is work.
 
Hivi unavyomuita SHEMEJI, yeye na huyo rafiki yako wameoana au wanakulana tu? Mi nnavyoelewa shemeji ni mtu ALIEOA ndugu yako. Otherwise hao saa yoyote wanaweza kuachana.. na kwavile wewe pia hujaolewa... unaeza shangaa huyo shemeji ndio anakuja kuwa mume wako.
Hapana nitakuwa nimemkosea kabisa rafiki yangu siwezi kufanya hivyo kwanza huyu shemeji anaonekana hana hiyo mipango ya ndoa bado anaenjoy life la ujana japo ana kama 33 hivi
 
Hapana nitakuwa nimemkosea kabisa rafiki yangu siwezi kufanya hivyo kwanza huyu shemeji anaonekana hana hiyo mipango ya ndoa bado anaenjoy life la ujana japo ana kama 33 hivi
Wee bana we..😄 maisha ni safari ndefu. Miaka 10 ijayo, huyo shemeji alishaachana na rafki yako siku nyingi, na wewe mlishazinguana na huyu jamaa yako wa sasa.. utashangaa penzi lenu na shemeji jinsi litakavyopamba moto 🔥🔥 Saa hiyo wote mnatafuta chaka la kustaafia 🤣🤣
 
Back
Top Bottom