Shellukindo adaiwa kuongoza uasi CCM

Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

nyie ccm mmeshindwa ku-address matatizo ya wananchi acheni kushikana uchawi; madaktari wamegoma nyie mnafanya mikutano kila siku isiyoisha wakati watu wanapukutika?

Mungu ameshawapiga pigo; pigo hili la kufarakana lazima linawamaliza tu mtake msitake; its external force from GOD na lazima mnasambaratika tu ifikapo 2012.

Hizi mzionazo ni dalili ya mwisho wa chama chenu ambacho badala ya kuwatetea wanyonge kimegeuka kuwa kijiwe cha kudai maslahi binafsi, posho na kuuza nchi kwa wawekezaji njaa. Mungu yupo na ndiye Jaji Mkuu - in GOD WE BELIEVE.

(mtanganyika asiye na matumaini ndani ya nchi yake tajiri)
 
Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

Habari za Jambo leo hizi.......
 
hivi kila anayekosa uwaziri ni lazima kuipasua ccm na viongozi wake, hivi chuki za kukosa kitu zitaisha lini? na kumbe hawawezi kuikosoa serikali wakiwa na madaraka
 
Chuki za kukosa zina mantiki kama walopata hawafanyi kazi na wasiopata wanaweza ku prove hilo, ndo demokrasia, walokosa wakapata, halafu wakashindwa kufanya kazi zao, then ni jukumu la wananchi kuwaondoa na kuwaweka watakaoweza, ndo demokrasia.
 
Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

Wewe kwa mambo yanavyokwenda unaonaje? Yuko sahihi ama la!
 
Huyu mama mbona kigeugeu!!mifano ya kigeugeu chake ni kama ifuatavyo,mwanzo alikuwa anampinga lowasa,mara akatangaza rasmi kuwa yupo kambi ya lowasa,akaibua suala la jairo lakini lilipoletwa bungeni akaanza kutetea tena,sasa ameanza na singo ya kikwete apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye,na anaendeleza uasi dhidi ya serikali,kisa posho!!siku akiwekwa kati ajieleze ataanza kutafuta mlango wa kutokea!!nec ya tarehe 12 tunaomba ajieleze kama anao ubavu wa kujisimamia,na wanaomuunga mkono nashindwa kuelewa uwezo wao make mwisho wa siku watakosa maelezo.
Yeah, huyu mama hana msimamo. Mwanzoni alikuwa kambi ya akina Sitta ila kwa sasa Lowassa damu. Vita vyake vya sasa kuanzia Jairo na hili la JK ku resign anavipigana kwa niaba ya Lowassa. Ila kubwa ni kwamba kama anatetea maslahi ya nchi hata kama anapigania kambi fulani hiyo hainihusu
 
NO POLITICIAN WHO IS THERE TO SAVE FOR THE INTEREST OF THE PEOPLE,EVERYONE IS THERE TO SAVE FOR HIS OR HER OWN INTEREST, naomba ifahamike hivyo :lol::yawn::yawn::yawn:
 
Kujihami kwa wasiokuwa na fikra pevu kwao huwa ni kuwa wanafanyiwa visasi. Lakini hawa wote siwaelewi maana huyu mama naye kigeugeu sana
 
...........kupiga propa za kukwamisha muswada ni zaidi ya uwendawazimu, kwa hili mama ametukosea watz, hata kama jk ana mapungufu yake, basi sio kwa hili, hapa naamini wengi tupo nyuma yake, kama wana hasira na posho waingie wodini kutibu.
Uasi wake ni upi. Mimina hapa ili tuwe na mapana ya kutosha katika kulielezea hilooo:A S-coffee:
 
Yeah, huyu mama hana msimamo. Mwanzoni alikuwa kambi ya akina Sitta ila kwa sasa Lowassa damu. Vita vyake vya sasa kuanzia Jairo na hili la JK ku resign anavipigana kwa niaba ya Lowassa. Ila kubwa ni kwamba kama anatetea maslahi ya nchi hata kama anapigania kambi fulani hiyo hainihusu
.........hana maslahi yoyote anayotetea zaidi ya tumbo lake, angekuwa anatetea maslahi ya taifa angekuwa mstari wa mbele kuufanya mswada wa katiba upite badala ya uasi wa kuukwamisha kwa sababu za kijinga kabisa, eti kufanya hivyo ni kupitisha mawazo ya cdm, kama yana maslahi kwa taif shida ipo wapi? kwani katiba ni ya cdm au watz?
 
Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

Ndugu yangu kashahama kundi huyo,sasa kabakiwa na ole sendeka tu ambae karudi kumsapoti Yero mwenzake baada ya kusuluhishwa.
 
Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

Muongo mkubwa wewe lini alikuambia anataka uwaziri, uwaziri serikali isiyokuwa na dira. peleka chuki zako kwa ndugu ya Jairo. nyoooooo
Bravo Beatrice umefanya kazi nzuri sana, may god bless you
 
Hili limama mi nililidharau pale lilipomsaliti mume wake aliyeshughulikiwa na kina lowassa ili aukose ubunge lenyewe eti baadae likahamia kwa lowassa bila haya.
 
Muongo mkubwa wewe lini alikuambia anataka uwaziri, uwaziri serikali isiyokuwa na dira. peleka chuki zako kwa ndugu ya Jairo. nyoooooo
Bravo Beatrice umefanya kazi nzuri sana, may god bless you

kwani wewe nae ni mtu?naona umeamua kuonyesha rangi ya uharo wako hapa.
 
Wewe kwa mambo yanavyokwenda unaonaje? Yuko sahihi ama la!

kama angekuwa mtu huru asiye katika kundi fulani wala hakuna mtu nyuma yake ingekuwa sawa mana hapangekuwa na chuki wala maslahi binafsi lakini kwa sasa hata afanye zuri hawezi kuaminika na jamii.
 
Huyu mama nae haeleweki,mara anapinga ufisadi,mara anasapoti mafisadi,yeye ni kimbelembele kupinga
mabadiliko ya kweli ya katiba,huyohuyo anaongoza kutetea nyongeza ya posho za wabunge wakati watanzania
wanakufa kwa mgomo wa maDR.Leave us alone hatumhitaji.
 
Inadaiwa kuwa Beatrice Shellukindo aka Jairo mbunge wa kilindi anaongoza uasi ndani ya wabunge wenzake wa CCM ili kuikomoa serikali kwa kuwa amenyimwa uwaziri.Shellukindo alikuwa na matarajio makubwa sana kupata uwaziri,alipoona ameukosa ameamua kula sahani moja na wale waliopo madarakani.

washirika wake ni ole sendeka,Ane kilango,mwakyembe na Sitta.

My take.hii ni chuki na hila ya kutaka wakose wote.

Ngumu kumeza, kajipange upya...

Beatrice Shelukindo (Kilindi), alieleza kutofurahishwa kwake na majibu ya Rais Kikwete kuhusu posho mpya za wabunge.
Mbunge huyo machachari alisema kuwa anashangazwa na serikali ya Kikwete kutokuwa na mawasiliano na viongozi wenzake kiasi cha kutoa majibu yanayotofautiana katika jambo moja, hali ambayo imewashangaza wananchi wengi.

Shelukindo alisema kauli ya Rais Kikwete kusema kwamba hajabariki posho mpya na kwamba hakuna mahali alipotia saini, imewaumbua Spika Anne Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambao walitamka hadharani kwamba Rais tayari ameshabariki posho hizo.

Shelukindo alisema pia kwamba Rais amewaudhi katika kushughulia sheria ya mabadiliko ya Katiba, kwani muswada ulioleta sheria hiyo ulipitishwa na wabunge wa CCM baada ya wabunge wa CHADEMA kuususia na kutoka bungeni, lakini baada ya Rais kukutana nao Ikulu, sasa Bunge zima linalazimika kuipitia sheria hiyo kuhalalisha mapendekezo yaleyale yaliyoletwa na CHADEMA.
Shelukindo alisema binafsi anakerwa na tabia ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda kuamua kutenda mambo kana kwamba hawawasiliani.

Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Shelukindo alifikia mahali akatishia kuwa kama Rais ndiye tatizo, wabunge wana uwezo wa kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Hata hivyo, kauli hiyo nzito ilipingwa vikali na Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka ambaye alimtaka Shelukindo afute kauli yake na kuomba radhi kwani lengo la kumchambua Rais Kikwete na serikali yake, halina nia ya kumuangusha, bali kuisaidia serikali yake.

Kutokana na kauli hiyo, Shelukindo aliomba radhi na kufuta kauli yake, lakini alisisitiza kuwa hakuwa na lengo baya. Sendeka alijikita kwenye suala la posho na kuwataka wabunge wenzake wa CCM kuachana nayo kwani inawajengea taswira mbaya mbele ya jamii.

Similar Discussions

Back
Top Bottom