Barua ya wazi kwa Lowassa na Rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa Lowassa na Rostam

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MzeePunch, Aug 22, 2009.

 1. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  BARUA YA WAZI KWA ROSTAM na LOWASSA:

  Kwa niaba ya Watanzania wote wanaoipenda nchi yao, nawaamuru kusoma barua hii niiandikayo kwenu kupitia mtandao huu wa Great Thinkers. Kama hamtasoma humu naamini vibaraka wenu wata-print na kuwaletea muisome.

  Tumefuatilia nyendo zenu kwa muda mrefu na kugundua kwamba ninyi na vibaraka wenu ndani na nje ya NEC ya CCM mmekuwa mkifanya hila na fitina kubwa dhidi ya wana wa nchi hii wanaopinga vitendo vyenu vya kifisadi.

  Mmekuwa mkifanya vikao vingi vya kupanga njama za kuwachafua wanasiasa na watu wengine wanaoheshimika kama wapiganiaji wa kweli wa haki za Watanzania walio wengi ili kudumisha ukandamizaji wa wanyonge huku mkilinda maslahi yenu binafsi.

  Lakini nimekasirishwa zaidi na kitendo chenu cha hivi karibuni cha kuwahonga wajumbe wa mkutano wa NEC ili wasaidie kutekeleza hila zenu za kutaka kumwondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Samwel Sitta, ili muendelee kuitafuna nchi bila usumbufu. Tuliwafuatilia kwa karibu sana kuanzia kule Zanzibar, tulikuwepo pale Hoteli ya Lamada, Dar es Salaam na baadaye Dodoma jinsi wapambe wenu wakiongozwa na Guninita mlivyokuwa mnatapanya pesa kwa wajumbe wapumbafu ili waisaliti nchi yao kwa hila zenu.

  Tumerekodi majina na kauli za hao vibaraka wenu wote wa NEC ili tuzifanyie kazi baada ya kuona Idara ya Usalama wa Taifa iliyopaswa kufanya kazi hiyo imelala. Majibu mtayapata baada ya muda si mrefu kwani bado tuna kazi ya kuufahamisha umma wa Watanzania ili watambue jinsi mlivyo watu hatari!

  Tunafahamu pia jinsi mnavyomtumia Kingunge Ngombale Mwiru kuupinga Waraka wa kanisa Katoliki kwa sababu umeanisha sifa za viongozi ambao watanzania wanawataka -- yaani viongozi waadilifu. Kwa kuwa nyie hamna sifa hizo mmeona waraka huo ni tishio kwa matamanio yenu ya kutaka kuwa madarakani. Tena wewe Lowassa nasikia eti unataka kuwa Rais baada ya Kikwete! Thubutu!

  Tunawaamuru kuacha mara moja kuwapotosha Watanzania kwa kutumia magazeti yenu yanayoongozwa na vibaraka wenu katika kumwaga sumu mbaya kwa wananchi wetu.

  Mmejifanya kuwa kimya kwenye vikao halali lakini ni wazungumzaji wazuri sana kwenye vikao vyenu vya siri mnavyovifanya hadi usiku wa manane.

  Kwa barua hii, mtambue kwamba Watanzania mliowanyonya kwa muda mrefu sasa wameamka na wako tayari kurejesha UHURU wao ili waweze kumiliki kikamilifu raslimali lukuki za nchi yao walizojaliwa na Mungu. Tanzania ni nchi tajiri sana lakini ina watu maskini kupindukia kutokana na kuporwa raslimali zao na watu walafi msiotosheka kama ninyi na marafiki zenu wachache.

  Ni matarajio yangu kwamba ujumbe huu utasaidia kuwarekebisha ili muache njama zote za kishenzi mnazopanga, ikiwa ni pamoja na kuthubutu kuwaharibia wapiganaji wetu hodari kama Samwel Sitta, Ole Sendeka, Dk Mwakyembe, Anne Kilango, Beatrice Shelukindo, Lucas Selelii, Godfrey Zambi, Fred Mpendazoe na wengine.

  Nasema ole wemu!
   
  Last edited: Aug 23, 2009
 2. s

  skasuku Senior Member

  #2
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu MzeePunch, wewe andika haya kama hisiao zako sio kuhusisha "Watanzania" kama ulivyo anza. Kama unauhakika na unacho andika kwa nini usiweke wazi, au ungesubiri ukiwa na nondo zote ndio uweke hapa.

  Hii imekaa kizushi...
   
 3. S

  Shangazi JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 307
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  SKASUKU UMETUMWA! AU ni mmoja wa vibaraka wa mafisadi. Ukishabikia jambo kumbuka hata siku ya mwisho utaulizwa na Mungu. Unaleta mambo ya Kingunge ya kusema waraka mbaya. Sema kifungu gani katika waraka wa mzee punch una uzushi?

  Naunga mkono waraka wa Mzee Punch. Naomba kutoa hoja
   
 4. s

  skasuku Senior Member

  #4
  Aug 22, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwanza kabisa ni uzushi kwa MzeePunch kusema anawakilisha Watanzania wote. Na pili aliyoyaandika ni hisia zake yeye mwenyewe. Tatu, anatishia toto kwamba ana nondo zaidi... hizo nondo zipo wapi.

  Na wewe Shangazi, acha kudandia gari usie jua limetoka wapi na lina kwenda wapi. Wacha kwanza mtu aweke sera zake hapa .. then... fanya maamuzi.

  Hizi kelele za Fisadi mwishoe hizi vita za kupinga ufisadi zitakosa makali. Hapa sio kijiwe cha chini ya muembe... tuwe na focused approach yaku point out the fisadiz na vielelezo vyake.

  Kwa mwenendo huu basi wote sisi ni mafisadi. Sasa nani atarusha jiwe la kwanza?
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Aug 22, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Mzee Punch maneno mazito sana mkuu wangu tumwombe mungu mwenye wingi wa rehema awajalie afya njema wapiganaji wote.Hii vita ni yetu wote watanzania tunaotaka Tanzania ibaki na amani na ustawi mkubwa wa kiuchumi unaotokana na rasilimali tulizojaliwa na mwenyezi mungu.

  Mtanzania anayekataa kuhusiswa na waraka wako Mzee Punch bila shaka tunajua yuko upande upi !!!!!!!!!!!!!!!.
   
 6. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2009
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Mjue kwamba watu wengine wamepigwa mihuri ya UFISADI kwenye roho zao, kelele zetu za mwizi hawakusikia nafikiri hata hiyo barua hawataisoma. Dawa yao ni moja, nayo ni kupigwa mawe na wananchi wenye hasira kali.
   
 7. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Wewe Skasuku ndio unaonekana mzushi zaidi, lete hoja kupinga hoja na sio braaabraaa za eti acha kudandia gari, hebu tupe Aproach muafaka unayodhani it will work kwa hawa jamaa
   
 8. S

  Simoni Member

  #8
  Aug 22, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Pamoja na usemi kuwa madaraka yana tabia ya kumfanya mwenye madaraka hayo awe fisadi. Kwa mazingira yaliyopo Tanzania ni kuwa wanaotafuta nafasi za uongozi wa kisiasa wamo ambao kwa asili na hulka yao ni mafisadi. Imedhihirika kuwa badala ya madaraka kumfanya mwenye madaraka hayo awe fisadi mambo ni kinyume chake kuwa madaraka yana tabia ya kumvuta fisadi upande wake. Wenye akili timamu huvutwa na mambo mengine muhimu zaidi ya madaraka.
  Kwa mfumo tulio nao sasa ni kuwa kwa vile ufisadi umekuwa ni sehemu ya utamaduni na tabia ya taifa letu, waadilifu hawana ubavu wa kugombea nafasi ya uongozi ila wenye nguvu ya fedha. Miongoni mwao wamo walio mafisadi. Na hao wakishinda chaguzi na wakipewa nyadhifa hapo ndipo nchi inafisidiwa. Lowasa Oyee!! Rostam Oyee! Makamba Oyee!! Makongoro Mahanga Oyee!! Guninita Oyee!! Kingunge Oyee!!
   
 9. UramboTabora

  UramboTabora Member

  #9
  Aug 22, 2009
  Joined: Sep 11, 2008
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Skasuku

  acha blaaaaaaaaah blaaah,humu hatuongelei kudandia gari.Lete maoni yako kama mtu mzima ya jinsi gani ya kupambana na hawa jamaa mafisadi watu usiku kucha wanakuna vichwa kujua jinsi gani ya kuwamaliza kisiasa, hilo ndilotunataka kusikia.

  kwa upande wangu mimi naona jinsi ya kuwamaliza ni ifikapo mwezi 10 mwakani wananchi wa majimbo yao wawateme hilo ndilo wazo langu.ngoja tusikie na wewe unasemaje
   
 10. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Magazeti kila ukurasa imeandikwa kuhusu NEC ya Lowasa na RA Redio zinahubiri, Tv haziko nyuma, Watu wameona kwa macho yao kuhusu hili, na pia Spika kwao kivumbi kinatimka kwa kumpa pole jamani SKASUKU bado huamini au na wewe ndo vibaraka wa Fisadi!! Tema mate chini wacha watu waongee na pia hata mawe yataongea!
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180


  Nadhani wewe ni Rostam mwenyewe au Lowassa, na kama si hivyo wewe ni kibaraka wao mkubwa kwani unaandika mambo yasiyo mbele wala nyuma!! YAANI MPAKA LEO HII UNAULIZA UPEWE USHAHIDI KUHUSU UFISADI WA LOWASSA NA ROSTAM? Unaishi dunia gani isiyojua RichMonduli na Kagoda?
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,413
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Mtawatambua kwa matendo yao.
   
 13. Kifaru Kajeruhi

  Kifaru Kajeruhi Member

  #13
  Aug 22, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili jitu SKASUKU kweli nimeanimi jina la kasuku halina maana na kazi yao aidha kuropoka bila kujua maana au kuiga. Acha kuongea vitu vya kitoto wewe unataka kuwafanya watu kuwa hawajui hayo mafisadi yanafanya nini...nakupongeza sana Mzee punch hasa kwa ujasiri wako wa kuandika mada ndefu na inayohamasisha....lete data mkuu...achana na wapumbavu ambao wanataka kupotosha ukweli kuhusu kinachoendelea.

  Endelea kutuwakilisha watanzania kwa sababu una kila haki ya kuwazungumzia watanzania...Huyu skasuku aache kabisa JF akaandike kwenye blog za mafisadi.

  Halafu huyu Urambo Tabora ana point sana...uko juu
   
 14. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Unajuwa si vizuri kutia chumvi ili ukubalike kwenye kundi fulani. Jee hayo magazeti yalishawahi kutaja majina ya hao watu waliomsulubu Spika Sitta?
  Msimshambulie huyu mwenzetu bure eti kwa vile hakubaliani na namna vita vya ufisadi inavyoendeshwa.
  Hivyo kwa kusikia taarifa za magazeti na kuwatajataja kina Lowassa bila ya kutowa ushahidi ndio tunasaidia vita vya ufisadi? Tumekuwa kama tukatwanga maji na ushahidi ni huko kusulubiwa kwa Spika.
  CCM haijawahi kuwa safi na hata hao wanaojiita wapambanaji si safi kwani ni wao wanaojilimbikizia mali. Hivyo utaniambia niamini kuwa mtu anaepigania alipwe Millioni 9 kwa mwezi huku mimi nikilipwa laki mbili huku akinyamazia kimya ni mpiganaji wa masilaha yangu au anatumia makosa ya mwengine ili abaki kwenye bunge. Kama hawa wapiganaji ni wa kweli basi si watumie nguvu zao kuleta maendeleo badala ya kukaa kule jengoni wakila milliono tisa, double posho kwa kamati, visemina vya kulipwa na kadhalika. Na waje huku chini na wao waone joto ya jiwe.
   
 15. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Barua hii wewe haikuhusu kwani unadhihirisha kwamba ni mmoja wa vibaraka wa hawa mafisadi. Hii imeandikwa kwa niaba ya Watanzania wapiganaji wanaoipenda nchi yao. Yawezekana nawe ni mmoja wa wale wa NEC walioambulia vijisenti.
   
 16. s

  skasuku Senior Member

  #16
  Aug 23, 2009
  Joined: Apr 19, 2008
  Messages: 113
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kazi kweli tunayo. Kama mwenendo ndio huu basi fisadiz wataendelea kupeta! Nilifikiri kuna u-seriousness katika kupinga, kuwaadhibu na kuwaangamiza "hawa" mafisadi.

  Majina uliyoyataja kwamba ni wapiganaji hodari, mbona karibu wote wana "Shutumiwa" kwamba ni mafisadi. Sasa kutokana na kutokua na vipimo vya "Fisadi" basi tutaendelea na blaa blaa kama kawaida.

  Kama kumtaja fisadi ni rahisi kama vile kutaja wachezaji wa Simba au Yanga... basi mbona kila mtu ana "views" zake tofauti kuhusu nani ni fisadi..?

  - Maoni yangu ni kutokuwapigia kura hawa wote ambao wana dalili za kiufisadi, hapo ndio tutakua tumewapiga bao la kisigino. pia kuna nji zengine ambazo wachangiai wengine wametoa hapa...
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Na wewe ni pumbafu tu kama lowasa
   
Loading...