Shekhe Mziwanda, na Shekhe Jongo, wanakosea kumuombea mabaya Tundu Lissu, huku wakisahau jinsi Lissu alivyotetea Mashehe wa Uamsho, na Answar Sunna

Shekhe Mziwanda, na Shekhe Jongo, wanakosea kumuombea mabaya Tundu Lissu, huku wakisahau jinsi Lissu alivyotetea Mashehe wa Uamsho, na Answar Sunna

Tukiamua kuwa wakweli Waislamu type ya hao Masheikh wanasababisha Waislamu wana uwezo mdogo wa kujenga hoja.

Ilitakiwa iwe Muislamu ndugu yake Muislamu mtenda haki na sio tu Muislamu ndugu yake Muislamu.

Watu wanauwawa, wanatekwa tunapaza sauti kwa uongozi uliopo madarakani wanatuita Wagalatia wana chuki na Kiongozi Mwislamu, kweli? Reasoning ya aina gani hii?

Kama Wakristo tulivyomkataa Pengo kipindi kile analeta Uchawa kwa Serikali ndivyo kila Mwislamu anavyotakiwa kuwakataa Masheikh wa namna hii.
 
Huu ni ushahidi ufike kwa Shekhe Mziwanda, na Shekhe Jongo.

Msikilizeni Tundu Lissu akitetea Mashekhe wa Uamsho, na Answar Sunna.

Je, ni uungwana Mziwanda, Jongo, na Mwaipopo, kumshambulia Tundu Lissu?



View: https://www.youtube.com/watch?v=WcWTRjKreWc



View: https://www.youtube.com/watch?v=0WazpC_VdZE


Hawa unaowasema ni mashekhe wa wapi? Maana kuna mashekhe ubwabwa pia. Maamuma. Hawajui lolote linaloendelea duniani, zaidi ya kuwa na emotions, kila wakati ukweli unaposemwa dhidi ya mtu wanayeona wana interest naye.

Cha mno wanachofanya ndio hicho cha kutoa vitisho fake..mara ntasoma itikafu...mara ntaita majini...mara ntasoma albadili.

Hakuna kitu chochote. Ingekuwa hayo mambo yanafanya kazi, Israel wangekoma
 
Na Wanasiasa ni kundi la wasomi?, acha dharau kama wamekosea niwao siyo wote tumia busara.
 
Back
Top Bottom