Shekhe Arusha Amwagiwa Tindikali

Shekhe Arusha Amwagiwa Tindikali

Status
Not open for further replies.
Nina suali jengine iyo matatu ndio ndio madarasa uliyosoma?
 
Si awataje watu wana roho mbayaa hadi mtoto unammwagiaa! !!!!!!!!
 
..Sheikh Msikiti Mkuu amwagiwa tindikali

Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Bondeni mkoani Arusha, Mustaph Kiago (49) na mwanaye Khalid Mustapha (10), wamemwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali wakati wakiingia msikitini.

Sheikh Kiago amejeruhiwa shingoni na mtoto wake ameumizwa machoni na wote wanatibiwa hospitali ya mkoa ya ya Mount Meru .

Akizungumza na NIPASHE nje ya wodi ya watoto kwenye hospitali hiyo jana, Kiago alisema amemwagiwa tindikali hiyo jana saa 11.10 alfajiri wakati anashuka ngazi kuingia msikitini kuongoza sala ya alfajiri.

“Nilipomaliza ngazi ili niiingie msikitini nilimwona kijana nyuma yangu ameshika kopo lenye maji mekundu na ghafla alinimwagia usoni na mengine yalimpata mtoto wangu”, alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo alikimbia baada ya kuwajeruhi akitumia pikipiki iliyokuwa nje ya msikiti.

Aliendelea kusema kuwa baada ya mtu huyo kukimbia, alirudi ndani na kumchukua mtoto wake hadi hospitali ya Mkoa Maunt Meru na kugundua kuwa ameumia macho wakati yeye alichunika ngozi ya shingo na usoni.

Mustapha aliyekuja nchini hivi karibuni akitokea Misri, alisema ameumia macho na kwamba ana wasiwasi jicho la kushoto halitaona tena.

Sheikh huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni vita iliyoanza muda mrefu ambapo, Februari 7 mwaka huu, akiwa msikitini, alifuatwa na Sheikh wa Mwanza (jina linahifadhiwa), akiwa na watu kadhaa na kutakiwa kutangaza jihad misikiti yote ya Arusha.

Alifafanua kuwa alikataa kutangaza jihad ambayo ni vita ya silaha dhidi ya Waislamu na wasio Waislamu akisema;“Nilipinga kwa sababu hatuwezi kuvunja amani tulionayo kwa masuala ya dini, wakaniambia lazima wataniua,"alisema.

Alifafanua kuwa alipowapinga ikatokea vurugu kubwa pale msikitini ambapo miongoni mwa kundi hilo lililoongozwa na Sheikh wa Mwanza aliyemtaja (jina tunalo), alimrukia na kumpokonya kipaza sauti lakini naye akakimbilia kuzima umeme.

Alisema waumini waliokuwepo walituliza ghasia naye alikwenda kutoa taarifa polisi.

Alilalamika kuwa licha ya kufika asubuhi hospitalini mtoto wake hajapata kitanda hivyo alikuwa anamshughulikia kwanza mwanae.

Mtoto Khalid anayesoma darasa la tatu nchini Misri, hakuzungumza kwa kuwa hafahamu Kiswahili na anazungumza Kiarabu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Japhet Lusingu, akizungumzia tukio hilo, alisema polisi ina taarifa zake na inaendelea na uchunguzi.

Alisema mara baada ya tukio hilo, polisi ilijulishwa na kufika eneo la tukio na kufanya mahojiano na mashuhuda kisha kuchukua kopo linalosadikiwa kuwa lilikuwa na tindikali hiyo.

CHANZO: NIPASHE
 
Hii Habari nimeiona nikajiuliza maswali meni , yakiwemo haya .

1. Kama taarifa hiyo ilipaswa kutolewa na ni maamuzi kutoka ngazi za juu , kuliko na haja gani ya kumuhimiza sheikbh huyo tu kuitoa hiyo taarifa ,,, yaani kwann isingesmwa na mtu mwinginwe mkubwa kulioko yeye..kama walkua wanamaanisha.

2, Je ina maana angetangaza hiyohabari, hiyo vita ingeanza vipi na kwa namna ipi.. ?? yaani tamko la watu wachache liwe vita ya watu wote??
 
Kuna watu wamechoka na maisha, badala ya kutafuta vitanzi wakajinyonga wenyewe wakiwa vyumbani mwao basi wanataka na wengine ili wafe nao.......huyo sheikh kutoka Mwanza mpuuzi sana, nitashangaa kufikia kesho kama hajaitwa mbele ya vyombo vya usalama kueleza hiyo jihadi inatokana na nini hasa.......Pole sana Sheikh uliyemwagiwa Tindikali wewe na mwao, Mungu atawajalia mupone haraka.
 
Hii Habari nimeiona nikajiuliza maswali meni , yakiwemo haya .

1. Kama taarifa hiyo ilipaswa kutolewa na ni maamuzi kutoka ngazi za juu , kuliko na haja gani ya kumuhimiza sheikbh huyo tu kuitoa hiyo taarifa ,,, yaani kwann isingesmwa na mtu mwinginwe mkubwa kulioko yeye..kama walkua wanamaanisha.

2, Je ina maana angetangaza hiyohabari, hiyo vita ingeanza vipi na kwa namna ipi.. ?? yaani tamko la watu wachache liwe vita ya watu wote??
huyo sheikh kama kuna kitu anakificha!!!kwa taratibu za misikiti haiwezekani eti aje mgeni tena toka mkoa mwingine aingie msikitini kisha akunyang'anye kipaza sauti atake kuongea ,hilo halipo ,!!!huko mwanza je jihadi ishatangazwa?mpaka aje mkoa mwingine?msimulizi akiwa mmoja habari huwa haikamiliki,nimebaki na maswali mengi bila majibu.
 
Kama Nipashe kweli wamefikia kuandika habari kama hizi basi kwaherini..
 
Tatizo la wale majamaa majina yao yoote yanafanana, sasa utamfaamuje Abdul ambae siye Abdala bin Abdula wa Abdulahim ibn Abdulai?
 
Mustapha%20Kiago.jpg

Mustapha Kiago

Sheikh wa Msikiti Mkuu wa Bondeni mkoani Arusha, Mustaph Kiago (49) na mwanaye Khalid Mustapha (10), wamemwagiwa kimiminika kinachodhaniwa kuwa ni tindikali wakati wakiingia msikitini.

Sheikh Kiago amejeruhiwa shingoni na mtoto wake ameumizwa machoni na wote wanatibiwa hospitali ya mkoa ya ya Mount Meru .

Akizungumza na NIPASHE nje ya wodi ya watoto kwenye hospitali hiyo jana, Kiago alisema amemwagiwa tindikali hiyo jana saa 11.10 alfajiri wakati anashuka ngazi kuingia msikitini kuongoza sala ya alfajiri.

“Nilipomaliza ngazi ili niiingie msikitini nilimwona kijana nyuma yangu ameshika kopo lenye maji mekundu na ghafla alinimwagia usoni na mengine yalimpata mtoto wangu”, alisema.

Alisema mtuhumiwa huyo alikimbia baada ya kuwajeruhi akitumia pikipiki iliyokuwa nje ya msikiti.

Aliendelea kusema kuwa baada ya mtu huyo kukimbia, alirudi ndani na kumchukua mtoto wake hadi hospitali ya Mkoa Maunt Meru na kugundua kuwa ameumia macho wakati yeye alichunika ngozi ya shingo na usoni.

Mustapha aliyekuja nchini hivi karibuni akitokea Misri, alisema ameumia macho na kwamba ana wasiwasi jicho la kushoto halitaona tena.

Sheikh huyo alisema chanzo cha tukio hilo ni vita iliyoanza muda mrefu ambapo, Februari 7 mwaka huu, akiwa msikitini, alifuatwa na Sheikh wa Mwanza (jina linahifadhiwa), akiwa na watu kadhaa na kutakiwa kutangaza jihad misikiti yote ya Arusha.

Alifafanua kuwa alikataa kutangaza jihad ambayo ni vita ya silaha dhidi ya Waislamu na wasio Waislamu akisema;“Nilipinga kwa sababu hatuwezi kuvunja amani tulionayo kwa masuala ya dini, wakaniambia lazima wataniua,"alisema.

Alifafanua kuwa alipowapinga ikatokea vurugu kubwa pale msikitini ambapo miongoni mwa kundi hilo lililoongozwa na Sheikh wa Mwanza aliyemtaja (jina tunalo), alimrukia na kumpokonya kipaza sauti lakini naye akakimbilia kuzima umeme.

Alisema waumini waliokuwepo walituliza ghasia naye alikwenda kutoa taarifa polisi.

Alilalamika kuwa licha ya kufika asubuhi hospitalini mtoto wake hajapata kitanda hivyo alikuwa anamshughulikia kwanza mwanae.

Mtoto Khalid anayesoma darasa la tatu nchini Misri, hakuzungumza kwa kuwa hafahamu Kiswahili na anazungumza Kiarabu.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Japhet Lusingu, akizungumzia tukio hilo, alisema polisi ina taarifa zake na inaendelea na uchunguzi.

Alisema mara baada ya tukio hilo, polisi ilijulishwa na kufika eneo la tukio na kufanya mahojiano na mashuhuda kisha kuchukua kopo linalosadikiwa kuwa lilikuwa na tindikali hiyo.

CHANZO: NIPASHE

We ukishaona SHEIKH au IMAM anatokewa na Matukio mabaya kama haya Ujue ni MSEMA KWELI NA NI MCHAMUNGU WA KWELI!

Na sio wale VIBARAKA au Viongozi ubwabwa, kazi yao ni kufuata maslahi ya kidunia tu na kushibisha matumbo yao kwa Mali za HARAM!

Na hata historia inatukumbusha kuwa Wasema kweli na Wadai haki Lzm wapitie Misukosuko kama HII!

MwenyeziMungu atamlipa Ujira mwema kwa Kazi yake.
Na Atampa afya ya haraka yeye na mwanae aliyemwagiwa hio acid!
Insha Allah.
 
Inanikumbusha jihad ya west Africa iliyoongozwa Ufo Fodio ambayo ilifanya Fulani kuwa kabila lililopata nguvu.
Ni zaidi ya hatari.
 
Jihad ya nini wakati makanisa yalikwishachomwa moto na viongozi wa kikristo kuuawa na wakristo wakakaa kimya? Wanataka kumuua nani tena?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom