Shekhe aipinga vikali chanjo ya malaria mbele ya Waziri wa Afya, kisa ushoga; hamuogopi mtu yeyote!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,850
18,260
Shehe mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amesikika na kuonekana hadharani akipinga vikali chanjo ya malaria kwa watanzania kwa kuhofia kuwa huenda imechanganywa na homoni za ushoga. Alitamka maneno hayo mbele ya Waziri wa Afya, huku akishangiliwa na kutuzwa na waislamu wenzake waliohudhuria mhadhara huo. Waziri alikaa kimya bila kujibu chochote akiashiria kuwa amekubaliana na maoni ya shehe.


Kitendo cha shehe huyo kukataa chanjo kinatokana na kushamiri vitendo vya kishoga siku za hivi karibuni ambapo mwanaharakati aitwaye Catherine Kahabi alizitaja hadharani taasisi zinazofadhili vitendo vya kishoga hapa nchini.

MAONI YANGU
Nawakubali sana waislamu kwa misimamo yao isiyoyumba, hasa pale unapotaka kuwachomea jambo au hoja kengeufu. Kama wakristo wangekuwa na misimamo isiyoyumba kama hii ya waislamu, nchi hii ingekuwa mbali sana kimaendeleo. Tatizo wakristo ni wapole sana. Mambo yanapokuwa magumu utawasikia wakisema: “Tunamuachia Mungu”. Waislamu hawana ujinga huo. Wakiamua kuwasha moto wanawasha kweli kweli bila kurudi nyuma mpaka kieleweke. Hapa ndipo waislamu na wakristo wanapotofautiana katika mambo ya muhimu na msingi katika ujenzi wa taifa letu tukufu.


====
Kulingana na habari ya BBC News Swahili, chanjo mpya ya malaria ambayo inajulikana kama RTS,S imeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Chanjo hii inakusudiwa kuwalinda watoto dhidi ya ugonjwa wa malaria. Kwa sasa, chanjo hiyo imefanyiwa majaribio katika nchi za Malawi, Ghana, na Kenya. Inakadiriwa kuwa chanjo hii inaweza kuzuia visa vya malaria kwa asilimia 40, na asilimia 30 ya visa hatari zaidi vya ugonjwa huo. Zaidi ya watoto 800,000 wameshapokea angalau dozi moja ya chanjo hiyo. Chanjo inahitaji dozi nne ili kuwa na ufanisi, na watoto wanachukuliwa kuwa katika hatari kubwa ya kufariki kutokana na malaria. Gharama na ununuzi wa chanjo hiyo bado hazijathibitishwa, na jumuiya ya kimataifa ya ufadhili italazimika kujadiliana jinsi ya kununua na kusambaza chanjo hiyo. Ingawa chanjo ya malaria inaleta matumaini, mamlaka za afya zinaonya kuwa ni muhimu kuendelea na hatua zingine za kinga kama vile kulala ndani ya vyandarua vilivyotibiwa na dawa za kuua mbu wanaosababisha malaria.
 
Kwani wewe unaamini chanjo za Malaria zina "hormone" za ushoga? Angekuja na scientific proof kutoka mahabara angalau alichokuwa akikisimamia kingeeleweka
Mkuu mimi nimeleta maoni ya shehe na aliyatamka mbele ya Waziri wa Afya. Sasa kama angekuwa hayuko sahihi mbona waziri alikaa kimya? Mimi na waziri nani mwenye facts na utaalamu zaidi?
 
Haya mambo asili yake sio uislamu ni kutafuta masifa yasiyokuwa na ulazima sasa hapo wanaenda kumtuza kwa point ipi aliyoongea? halafu tangu lini sisi waislamu tumeanza kuiga iga mambo ya ajabu kama haya, haya mambo ya kutuzana kwenye kofia si huwa kwenye taarabu huko?.
 
I think sababu ya msingi ya kutilia shaka chanjo ya malaria inapaswa kuwa efficacy ya hii chanjo ni ya chini sana kulingana na ushahidi wa clinical trials. Hayo mambo ya hormones za ushoga ni paukwa pakawa za watu wasio na maarifa mtambuka.
Amejitia uana-sayansi na kutoa kauli kingizi mbele ya waziri wa Afya!
 
Back
Top Bottom