Elections 2010 Shein ajitoa kinyanganyiro cha Urais Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Tatizo lako ni kwamba akili na macho yako yanadanganyika na ujanja wa CCM!! Hakuna Rais aliyepata kutawala Tanzania anaeendekeza UDINI na ukabila kama Kikwete; sina haja ya kudhihilisha hilo, mifano iko wazi ila nikuambia tu tabia yake ya kupeleka miradi ya kiwanja cha ndege , bandali na Viwanda ili mradi Bagamoyo ndiko anakotoka ni ashara tosha ya mtu anayejipendelea kwa maamuzi yake bila kuangalia faida kwa nchi nzima.

Ndio ilivyo kwa kila anaepata madaraka ya inji hii
Angalia kule Arusha,K/njaro...barabara hadi kwenye mikahawa.Mrema ndio alipeleka hadi getini kwake barabara inayotoka main road.Mambo ya KIA,AICC etc ni influence ya u home boy..na wa kule kusini ndio hivyo tena,,Mkapa kawakumbuka na the Mkapa road.

Kuna madai ya kwamba Daniel Yona na Mkapa walikuwa wana channel fedhwa za serikali including hizi za ufisadi kwenye makanisa na miradi yao....ndio maana versities ziliibuka kama uyoga under Mkapa admin
 
Siwezi shangaa kujitoa,maana ilionekana kabisa kuwa CCM-Bara ndiyo wanamtaka Shein ili hali CCM-Kisiwandui wakiwa hawamtaki hata kusikia,walikuwa wanamuambia wazi kuwa yeye si mwenzao na hata Katiba inasema wazi kuwa Rais wa ZNZ lzm awe na uwezo wa kupiga kura kwenye jimbo lolote kisiwani ZNZ;Shein hakuwa na sifa hiyo!

By the way,iweje hadi leo kwenye zama hizi za demokrasia,kikundi cha watu wa Bara overwhelmingly ndiyo wawachagulie ZNZ mgombea wao?Kumbuka mwaka 2000 Dr Ghalib Bilal alishinda kwa kura nyingi kura za wajumbe wa CCM-ZNZ lkn hawa CCM-Bara ikamchagua Aman Karume na kwa uwingi wao mjengoni wakamfanya ashinde;kama Shein kajitoa ni ishara ya wazi kuwa sasa CCM imeanza kuwasikia wapiga kura wa CCM-ZNZ na ni dhahiri sasa Dr Ghalib Bilal ambaye ni hasimu namba moja wa Rais aondokaye Karume atatangazwa kuwa mgombea wa CCM-ZNZ akiendeleza na kurithi makundi yake yale ya Karume vs Komandoo!

Swali,je ukifanyika uchaguzi wa uhuru na wa haki,Ghalib atamshinda Maalim?

Inawezekana kote ukawa sahihi lakini sehemu niliyoweka alama nyekundu unazungumzia siasa za wakati wa Komandoo. CCM ya sasa ni ya Dk. Karume na si Dk. Salmin na ndio maana Dk. Bilal amepita katika tundu ya sindano pale Kisiwandui kwenye kamati maalumu ya NEC ZNZ. Kama Maskani ya Kisonge ingekuwa ina kura ndipo Dk. Bilal angeshinda kwa kishindo maana wao ndio wameamua kufa nae. Kwa hakika ni kwamba kinyume chake ni kwamba sasa Shein ndio chaguo la CCM Zanzibar wakiungwa mkono kichini chini na baadhi ya viongozi wa bara na kwamba Bilal anategemea sana nguvu ya CCM bara kutoka kwa maswahiba wake wapya ambao wanatajwa kuwa na nguvu kubwa kisiasa ndani ya CCM na katika vyombo vya habari.

Kwa ujumla hata hii taarifa ya Shein kujitoa ni mkakati wa kundi hilo linalompinga Shein ambao ni makundi yote yameungana na kila kundi likiamini kwamba akitoka Shein wagombea wao watakua na nafasi sawa ya kuteuliwa. Ukimuondoa Shein, wagombea kama Bilal, Shamsi na hata Mohamed Aboud watapata uhai mpya na hivyo wapambe wao wanatumia kila njia kuwatisha kina JK kuona kwamba Shein anaondoka. Suala la kujiondoa kwa Shein ni mkakati uliopelekwa kwake ili eti ajitoe kulinda heshima yake maana amechafuliwa sana na akiendelea ataweza kuaibika, lakini kwa kuwa si utashi wake binafsi hana uwezo wa kujiondoa kwa wakati huu na kama itakuwa hivyo itakuwa ni baada ya JK na KArume kuzidiwa. Kwa sasa mbali ya Shein nguvu kubwa imehamishiwa kwa JK na Karume na kwenye kamati kuu ili kuhakikisha Shein anaondoka na makundi mengine kupata upenyo. Mohamed Aboud anaona ni wakati wa Wapemba na akitoka Shein yeye ndiye anayebaki kama Mpemba pekee anayeweza kupewa nafasi ya kumkabili Maalim Seif.

Hebu tusubiri tuone maana wameamua kuahirisha kamati kuu ifanyika siku moja na NEC ili uamuzi mgumu ukipitishwa na Kamati Kuu watu wakose muda wa kujipanga kuvuruga.

Tetesi nyingine ni kwamba Dk. Salmin Amour ametoa sharti kwamba apewe nafasi ya ugombea mwenza ili amuunge mkono Shein. Mwaka huu tutasikia mengi maana Komandoo kupanda ndege ya serikali aliyokodishiwa Shamsi ametangazwa kumuunga mkono SHamsi. Yeye binafsi hajaipenda hiyo.
 
Yaani masa umenikuna hasa natamani uwe shemeji yangu,unae dada?

Wote wanaoonekana kuwa na nguvu katika first eleven ya CCM Zanzibar hadi first 3 hakuna anayempata Maalim. huo ndio ukweli mchungu kwa CCM, niko Pemba naona hali ilivyo
 
Mkuu haitaki tochi hapo Dr. Salmini yupo hupo kwa mgombea wake Dr.Bilal na kwa taarifa yako wakati kikao cha kamati maalumu ya NEC kikiendelea Unguja, yeye komandoo alimfuata Jakaya Kikwete na kuteta naye, haijuulikani ni kitu gani wameongea ila watu wa jikoni wanadai kuwa ilikuwa ni mazungumzo ya "ahadi ni deni" ambayo yamemtega Kikwete, anayen'ngan'ngania Dr.Shein wakati yeye harakati zake na kila kitu wakati ule akiutaka urais zimeratibiwa na wao Zanzibar.
 
Yaani masa umenikuna hasa natamani uwe shemeji yangu,unae dada?

lol ... sasa wewe unataka uwe shemeji yake mara mbili? Masa alishajichukulia mtoto wa kizenji ndo maana mambo ya huko hayampigi chenga. Labda umwombe atangaze ndoa kama bado hajatangaza, maana uwezekano wa kubadilishana madada naona ni mdogo sana.

Note: nime-assume kwamba Mkuu Junius nawe watokea Zenji, assumptions zinaruhusiwa sometimes.
 
Yaani masa umenikuna hasa natamani uwe shemeji yangu,unae dada?

Usijali ndugu yangu ukweli ni huo! Nina mchumba Mzenj ndugu yangu sioni wala sisikii ishallah mwisho wa mwaka labda kitaeleweka. Nadhani tushafahamiana.
 
Wote wanaoonekana kuwa na nguvu katika first eleven ya CCM Zanzibar hadi first 3 hakuna anayempata Maalim. huo ndio ukweli mchungu kwa CCM, niko Pemba naona hali ilivyo

Ni kweli kabisa, mimi nashangaa sijuwi Kikwete na Makamba wanatapatapa kitu gani, wanachokitengeneza wao wanaona wanamkomoa Dr. Bilal hawajuwi kuwa wenye hila na mbinu chafu za kumshida Maalim Seif ni kundi la Dr. Bilal (fomer komandoo aide) na kitendo cha kumpa mpinzani wake wanayemuunga mkono wao bila ya shaka ni faida kwa Maalim Seif ambaye kawazidi kila kitu wagombea wote hao 11 wa CCM. Na kama uteuzi wa CCM utakwenda kasoro kidogo tu,basi wajuwe ndiyo mwisho wa kuiskia CCM Unguja.

Mimi nawashauri, kama lazima basi wampate mgombea wanaona ataendeleza maelewano ya Amani na Seif, na wao wanamuona Dr.Shein anawafaa kwa hilo, ijapo hauziki kwa wapiga kura wa CCM Zanzibar, basi cha kufanya wanaweza wakayalinda maridhiano hayo hata kama mgombea atakuwa Raza seuze yule wanayemtaka CCM Zanzibar, iwapo watambebesha mgombea yeyote azimio rasmi la chama la kuunga mkono kwa kura ya maoni kwa kutia NDIYO. Ikawa weshakinusuru chama chao na kifo cha dhahiri shahiri Unguja,maana Pemba hakipo na Unguja kipo nusu.
 
Kwa kweli kuna watu walisema CUF imekwisha kwa kuzungumza na Karume lakini sasa naona kama karata yao ni kali sana na inaona mbali sana na pengine ikatoa suluhisho la matatizo ya Zanzibar. Niko Pemba unaweza kulia,maana mandhari nzuri iliyopo haistahili kabisa kuwa sehemu duni katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki, ingekuwa mahali pema pa kibiashara ya utalii na biashara nyenginezo za huduma pamoja na kilimo.
 
Wote wanaoonekana kuwa na nguvu katika first eleven ya CCM Zanzibar hadi first 3 hakuna anayempata Maalim. huo ndio ukweli mchungu kwa CCM, niko Pemba naona hali ilivyo

Mkuu Halisi nimekuona muda mrefu sana hapa kwenye hii thread, nikataka kukuomba utupe ukweli wa hii news, na bahati nzuri naona umeweka wazi nini kinachoendelea kwenye anga za siasa chafu zikiongozwa na vigogo waliobobea kwenye hiyo fani kutoka bara.

Nina maswali kidogo kuhusu hiyo quote hapo juu na uchaguzi wa mwaka huu.

Mara ya mwisho kwenye reconciliation walisema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wajumbe wake pia watateuliwa kutoka CUF ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwenye chaguzi zitakazofuata. Na kumbukumbu yangu inasema kwamba Karume alimteua mjumbe mmoja akidai kwamba ni mwanachama wa CUF, lakini CUF walisema Karume hakutakiwa kuteua yeye moja kwa moja, alitakiwa awaambie CUF ili wampe jina maana wao CUF ndiyo wanawajua wanachama wao vizuri. Sikumbuki sakata hilo liliishia wapi. Maswali:

1. Je, kuna any developments kuhusu kuhakikisha kamba ZEC inajumuisha pia wana CUF ili kuondoa hisia za kuibiwa kura ama udanganyifu wa kura za maruhani?

2. CUF wamefanya maandalizi gani kuhakikisha kwamba mwaka huu wizi hauwezi kufanyika tena?

3. Kuna dalili zote za CCM kuanza njama za kuiba kura?

Najua unaweza usiwe na majibu ya kutosheleza, lakini hata hint tu zinatosha ili kupata feeling what is on the ground na tujue mapema kama mchezo mchafu utaendelea as usual ama mwaka CUF watashangilia badala kulia.

Ni hayo tu Mkuu, usiwe unapotea sana maana msimu wa news muhimu na za uhakika umewadia.
 
Tatizo, sera za CUF ni za chuki, ubaguzi, udini, nk.

Mkuu Buchanan,

Unao ushahidi wa haya uliyoyasema!!!!!!! Hizo sera za chuki na yote uliyoyasema ziko wapi? Hebu tutundikie hapa hata sisi tusiozijua tufumbuke macho!!!

Tiba
 
Urais Zanzibar rafu tupu:DK SHEIN ADAIWA KUJIONDOA

Kwa mtu mwenye ufahamu wa Katiba ya Zanzibar naomba atupatie kifungu ambacho kinamfanya Dr. Shein akose sifa ya kuwa mgombea. Habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi (angalia link) zinasema kwamba Katiba ya Zanzibar inamfanya Dr. Shein akose sifa za kugombea, na kwamba wapinzani wake wanaweza kutumia kifungu hicho ili kumuwekea pingamizi, but hawataji kifungu. Kama kuna anajua kifungu atuwekee hapa ili tukione na tukichambue.
 
Mkuu Buchanan,

Unao ushahidi wa haya uliyoyasema!!!!!!! Hizo sera za chuki na yote uliyoyasema ziko wapi? Hebu tutundikie hapa hata sisi tusiozijua tufumbuke macho!!!

Tiba
Mkuu Tiba, achana naye huyu si jukwaa lake hili kaja tu, asikutibue!
 
Urais Zanzibar rafu tupu:DK SHEIN ADAIWA KUJIONDOA

Kwa mtu mwenye ufahamu wa Katiba ya Zanzibar naomba atupatie kifungu ambacho kinamfanya Dr. Shein akose sifa ya kuwa mgombea. Habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi (angalia link) zinasema kwamba Katiba ya Zanzibar inamfanya Dr. Shein akose sifa za kugombea, na kwamba wapinzani wake wanaweza kutumia kifungu hicho ili kumuwekea pingamizi, but hawataji kifungu. Kama kuna anajua kifungu atuwekee hapa ili tukione na tukichambue.

Mkuu katiba hapa sina ila kwanza tuanzie kwenye nukuu hizi,wakati naitafuta:
Duru za siasa kutoka mjini Zanzibar na Dodoma kwa nyakati tofauti, zimethibitisha kwamba wapinzani wa Dk. Shein anayepewa nafasi kubwa kutokana na kuungwa mkono na vigogo wa serikali, wamekamia kutumia sheria ya Katiba ya Zanzibar kumuengua kwenye kinyang’anyiro hicho.

Vyanzo vyetu vya habari vilisisitiza kuwa Katiba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ya mwaka 1984, ndiyo itakayotumika kumbana Makamu huyu wa Rais wa Muungano.

Kwa mujibu wa Katiba hiyo toleo la mwaka 2003, iliyopitishwa Julai 17, sura ya 15, kifungu cha pili kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa Rais wa Zanzibar.

Kifungu hicho chenye sehemu (a) hadi (d), kinataja sifa za mtu anayefaa kuwa rais wa Zanziabr kuwa ni pamoja na kuwa Mzanzibari wa kuzaliwa, awe ameshatimiza umri wa miaka 40.

Sifa nyingine ni kwamba awe na sifa za kumuwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na sifa ya mwisho inamtaka awe mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa rasmi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa 1992.

“Katika kifungu cha 2(C), kinachosema awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ndicho kitakachotumika kumbana Dk. Shein maana hana sifa hiyo,” alisema mmoja wa makada wa CCM.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na kwamba awe Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 21.

Sifa nyingine ambayo wapinzani wa Dk. Shein wamejipanga kumnyuka nayo ni ile ya kifungu cha 68(b) ambacho kinasema awe amejiandikisha au ana sifa za kujiandikisha katika jimbo la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.

Kifungo hicho kinadaiwa kinaweza kuwa kitanzi kwa Dk. Shein kwani hakujiandikisha katika jimbo lake la uchaguzi kama mpiga kura katika uchaguzi wa Baraza la Wawakilishi.

“Kwa hiyo, Dk. Shein ana mtihani mzito wa kuteuliwa maana hakujiandikisha katika jimbo lake kama mpiga kura. Amekiweka chama na yeye mwenyewe kwenye wakati mgumu sana wa kufanya maamuzi,” alisema mmoja wa wajumbe wa NEC ya CCM.
source:tzdaima
 
Na baadhi ya maoni ya wanasheria haya hapa:

Wakati huo huo, Mwanasheria Mkongwe Zanzibar, Hamid Bwezeleni, amesema katiba na sheria ya uchaguzi ni vitu vya msingi vinavyopaswa kuzingatiwa katika mchakato wa kumtafuta mgombea urais kati ya wagombea waliojitokeza.
Alisema suala la wagombea waliojitokeza kuwa na sifa za kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapigakura Zanzibar bado lina nafasi kubwa kwa vile limeelezwa ndani ya sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar na Katiba ya mwaka 1984 ya Zanzibar.
Bwezeleni ambaye amewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, alisema kifungu cha 26 (1) (2) (c) cha katiba ya Zanzibar kimeeleza wazi kuhusu sifa za mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar.
Alisema mgombea urais wa Zanzibar anatakiwa awe na vigezo kama vilivyowekwa kwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi vya kuwa na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa katika uchaguzi huo.
Aidha, alisema sheria ya uchaguzi kifungu cha 13 (6) kimeeleza wazi hakuna Mzanzibari yeyote atakayeruhusiwa kupiga kura katika jimbo ikiwa jina lake halijaorodheshwa ndani ya daftari, jambo ambalo alisema linahitaji kuangaliwa kwa umakini, kwa kuwa halina tofauti na masharti yaliyowekwa kikatiba kama ilivyo katika sifa za mgombea wa urais.
Kauli ya Mwanasheria huyo imekuja baada ya suala la kuwepo kwa wagombea ambao hawajaandikishwa katika daftari la kudumu kujitokeza katika kikao cha Kamati Maalum ya NEC Zanzibar kilichokutana Jumamosi iliyopita chini ya Mwenyekiti wake, Rais Karume.
source:nipashe
 
Urais Zanzibar rafu tupu:DK SHEIN ADAIWA KUJIONDOA

Kwa mtu mwenye ufahamu wa Katiba ya Zanzibar naomba atupatie kifungu ambacho kinamfanya Dr. Shein akose sifa ya kuwa mgombea. Habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Mwananchi (angalia link) zinasema kwamba Katiba ya Zanzibar inamfanya Dr. Shein akose sifa za kugombea, na kwamba wapinzani wake wanaweza kutumia kifungu hicho ili kumuwekea pingamizi, but hawataji kifungu. Kama kuna anajua kifungu atuwekee hapa ili tukione na tukichambue.

Kwanza sina hakika ya upya wa hiyo story

Dk. Shein kitanzani

Ina maana imekuwa ikipikwa kila siku na huenda pia kwa siasa za Tanzania ndio mkakati uliopo wa kumburuza hadi wamtose, sina hakika kama JK anaaminika katika siasa za nchi hii, anaweza kuzidiwa. LOlote linaweza kutokea kuanzia saa hizi usiku na kesho asubuhi.
 
Mkuu Halisi nimekuona muda mrefu sana hapa kwenye hii thread, nikataka kukuomba utupe ukweli wa hii news, na bahati nzuri naona umeweka wazi nini kinachoendelea kwenye anga za siasa chafu zikiongozwa na vigogo waliobobea kwenye hiyo fani kutoka bara.

Nina maswali kidogo kuhusu hiyo quote hapo juu na uchaguzi wa mwaka huu.

Mara ya mwisho kwenye reconciliation walisema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wajumbe wake pia watateuliwa kutoka CUF ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwenye chaguzi zitakazofuata. Na kumbukumbu yangu inasema kwamba Karume alimteua mjumbe mmoja akidai kwamba ni mwanachama wa CUF, lakini CUF walisema Karume hakutakiwa kuteua yeye moja kwa moja, alitakiwa awaambie CUF ili wampe jina maana wao CUF ndiyo wanawajua wanachama wao vizuri. Sikumbuki sakata hilo liliishia wapi. Maswali:

1. Je, kuna any developments kuhusu kuhakikisha kamba ZEC inajumuisha pia wana CUF ili kuondoa hisia za kuibiwa kura ama udanganyifu wa kura za maruhani?

2. CUF wamefanya maandalizi gani kuhakikisha kwamba mwaka huu wizi hauwezi kufanyika tena?

3. Kuna dalili zote za CCM kuanza njama za kuiba kura?

Najua unaweza usiwe na majibu ya kutosheleza, lakini hata hint tu zinatosha ili kupata feeling what is on the ground na tujue mapema kama mchezo mchafu utaendelea as usual ama mwaka CUF watashangilia badala kulia.

Ni hayo tu Mkuu, usiwe unapotea sana maana msimu wa news muhimu na za uhakika umewadia.

Mkuu maswali yako yanahitaji majibu makini sana kama yalivyo maswali makini na muda huu sitoweza kufanya hivyo. Kwa kuwa umeelekeza moja kwa moja kwangu, naliachia jamvi linisaidie tukianzia na mkuu Junius
 
Tatizo lako ni kwamba akili na macho yako yanadanganyika na ujanja wa CCM!! Hakuna Rais aliyepata kutawala Tanzania anaeendekeza UDINI na ukabila kama Kikwete; sina haja ya kudhihilisha hilo, mifano iko wazi ila nikuambia tu tabia yake ya kupeleka miradi ya kiwanja cha ndege , bandali na Viwanda ili mradi Bagamoyo ndiko anakotoka ni ashara tosha ya mtu anayejipendelea kwa maamuzi yake bila kuangalia faida kwa nchi nzima.
Nitajie mambo matatu ambayo kikwete amewapendelea waislamu?
 
Mkuu Junius,

Hiyo nukuu niliisoma, lakini kama ilivyo kawaida ya waandishi wetu wa habari huwa wanatuandikia bila kuweka wazi kila kitu na matokeo yake wanatuongezea kazi nyingine ya kutafuta more info ambazo hatuna. Niko interested na kipande hiki:

“Katika kifungu cha 2(C), kinachosema awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, ndicho kitakachotumika kumbana Dk. Shein maana hana sifa hiyo,” alisema mmoja wa makada wa CCM.

Halafu wanaendelea kusema kwamba:

Kwa mujibu wa kifungu hicho, sifa za mtu anayefaa kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ni pamoja na kwamba awe Mzanzibari aliyetimiza umri wa miaka 21.

Swali ni kwamba ina maana Dr. Shein siyo mZanzibari? Ina maana hajafikisha miaka 21? Kwa kutumia hicho kifungu cha 2(C), ni sehemu ipi ya kifungu inayomfanya Dr. Shein akose sifa?

Ndiyo maana nikaomba mwenye ufahamu wa Katiba ya Zanzibar ama mwenye soft copy atuwekee hicho kifungu.

Nimeshituka niliposoma kwenye gazeti la Mwananchi kwamba Dr. Shein alikutana na JK na Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Swala hili limekuwa serious kiasi cha kuhitaji ushauri wa Mwanasheria Mkuu? Au ndio habari za udaku wa magazeti kwa kutumia propaganda za mafisadi?

The bottom line ni kwamba CCM kwa upande wa Zanzibar wanatembea kwenye kamba nyembamba, options zote walizo nazo zinawaweka pabaya na kumpa advantage Maalim Seif na CUF kwenye uchaguzi wa Rais wa Zanzibar. Otherwise labda wajiandae kwa massive rigging, maana itabidi waibe kura nyingi sana ili waweze kushinda.
 
Nina maswali kidogo kuhusu hiyo quote hapo juu na uchaguzi wa mwaka huu.

Mara ya mwisho kwenye reconciliation walisema kwamba Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), wajumbe wake pia watateuliwa kutoka CUF ili kuhakikisha kwamba haki inatendeka kwenye chaguzi zitakazofuata. Na kumbukumbu yangu inasema kwamba Karume alimteua mjumbe mmoja akidai kwamba ni mwanachama wa CUF, lakini CUF walisema Karume hakutakiwa kuteua yeye moja kwa moja, alitakiwa awaambie CUF ili wampe jina maana wao CUF ndiyo wanawajua wanachama wao vizuri. Sikumbuki sakata hilo liliishia wapi. Maswali:

1. Je, kuna any developments kuhusu kuhakikisha kamba ZEC inajumuisha pia wana CUF ili kuondoa hisia za kuibiwa kura ama udanganyifu wa kura za maruhani?

2. CUF wamefanya maandalizi gani kuhakikisha kwamba mwaka huu wizi hauwezi kufanyika tena?

3. Kuna dalili zote za CCM kuanza njama za kuiba kura?

Najua unaweza usiwe na majibu ya kutosheleza, lakini hata hint tu zinatosha ili kupata feeling what is on the ground na tujue mapema kama mchezo mchafu utaendelea as usual ama mwaka CUF watashangilia badala kulia.

Ni hayo tu Mkuu, usiwe unapotea sana maana msimu wa news muhimu na za uhakika umewadia.
Mkuu Halisi, Keil
Wapo watu wanaweza kutusaidia kitaalamu zaidi. Ila ninachoweza kudadavua katika maswali hayo ni kama ifuatavyo:
Itakumbukwa katika muafaka wa mwanzo au wapili ilitakiwa pawepo mabadiliko ya tume kwa kuingiza wajumbe kutoka vyama vya siasa na hili lilifanyika kwa CUF kuingiza wajumbe wawili na CCM kadhalika. CUF iliwapeleka ndg. Nassor Khamis Mohammed(mwanasheria) na ndg.Ayoub Bakar na CCM ikawakilishwa na ndg. Khatib Mwinchande na Said Bakari Jecha ambaye amewahi kuwa kitengo cha usalama wa taifa na waziri katika wa SMZ kama sikosei na bado ni mjumbe wa tume.

Cha ajabu licha ya kuwa wajumbe wa CUF wamo humo lakini bado ZEC imekuwa ikiongozwa na makada wa chama cha Mapinduzi na usalama wa taifa. Tokea tume iundwe Wenyeviti wake wote wamekuwa ni makada wa CCM kuanzia jaji Zubeir Juma Mzee, Mzee Masauni (baba yake Masauni aliyefukuzwa ubosi UVCCM)...na huyu wa sasa Khatibu Mwinchande ambaye awali alikuwa mjumbe wa tume hiyo kwa tiketi ya CCM sasa ndo mwenyekiti wake. Uadilifu wa tume bado una mashaka na wajumbe wawili wa CUF humo hawawashi wala hawazimi.

Kuhusu maandalizi ya kuzuia wizi wa kura kwa CUF hali imekuwa ngumu, kwa sababu moja kubwa, CCM wana mbinu nyingi za kuiba kura, hawaibi kwa kuziongeza zao, wanaanza kuzipunguza za CUF...mfano kuwakataa kuandikisha wapiga kura wake ,ukizingatia tume ni yao wao na mchakato wa kupandikiza wapiga kura hewa huwa ni rahisi kwao, bila shaka haya yote tumeyashuhudia katika hatua ya ku up date daftari la wapiga kura.

Ilichofanya CUF,kama kawaida ya Maalim Seif, ambaye ni ukweli usiofichika kuwa hakuna mwanasiasa yeyote anaeziweza siasa za visiwani kama Maalim Seif, amecheza karata yake ambayo mimi naiita "confusion card" nyinyi iiteni "MARIDHIANO BAINA YAKE NA KARUME". Karata hii tayari inafanya kazi yake vizuri sasa hivi, kwakuwa imeshakigawa chama cha mapinduzi vipande vipande. Ni triki ambayo imeshakigawa chama cha mapinduzi Zanzibar na kumchanganya mwenyekiti wake Kikwete.

Hapa binafsi nayakumbuka maneno ya Maalim Seif aliyosema katika mkutano wa hadhara Kibandamaiti,baadha ya kutanganza kumtambua karume,alisema"wanaosema injini ya Maalim Seif imechemsha wanajidanganya....injini ya Maalim haijachemsha bado ipo fit na subirini mtaona..." nakweli sasa tunaona, kirusi cha MARIDHIANO kinaichachafya CCM yote.

Hapa CUF wanafaidika vipi?
Kama DR.Shein atalazimishwa kupita basi hivyo hivyo atalazimishwa kuwa rais Zanzibar na serikali ya mseto itaundwa hata kama kura ya maoni itasema HAPANA. Kwa hiyo maalim kurudi ikulu ni suala la kusubiri tu,ukizingatia CUF inaweza kum KNOCK OUT,Dr.sheni kwa kumuwekea pingamizi kugombea, ambayo ipo wazi kuwa hana sifa yakuwa mgombea baada ya kupoteza ile ya kuwa mwakilishi.

Kama Bilal atapitishwa itachukuwa mda kidogo CCM kupotea kwa kuwa migogoro ya siasa haita kwisha iwapo kura ya maoni italazimishwa kuwa HAPANA, nikimaanisha karata ya CUF itabaki kwa kura ya maoni tu na mkakati mweingine ambao ni siri ya chama.
Nafikiri kwa suala la tatu litakuw limejibika kwa lapili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom