Sheikh yahya aokoka!!

Sheikh yahya aokoka!!

Jana kuna mdau alinipa taarifa za pale ubungo msewe lile kanisa pastor wao ndio yule mwenye hammer ya mil 250 damu ya mzee inasemekana aliyeokoka ni mfuasi wa sheikh mtajwa lakini sio mwenyewe sasa sijui kama sheikh mwenyewe alikuja mwisho wa ibada
 
Niliyoifahamu mie ni ya kuokoka kwa yule Sheikh Mtoto maarufu kama Sheikh Shariff ambaye aliitingisha inji hii kwa ufahamu mkubwa wa Qur'an akiwa na umri wa miaka tisa na akabatizwa kwa jina jipya la Michael Sylivester Sewando. Ilikuwa reported kwenye Msema Kweli, Sept las yr.

USIWE UNATU "CONFUSE" HAPA NA HII ILIYOWAHI KURIPOTIWA 3 WKs AGo:


Mchungaji ampa Sheikh Yahaya masharti matatu



Siku chache baada ya mtabiri mashuhuri wa Afrika Mashariki na Kati, Sheikh Yahaya Hussein wa Dar es Salaam kutangaza katika vyombo vya habari kuwa mwana CCM atakayejitokeza kuchuana na Rais Jakaya Kikwete katika kinyang'anyiro cha kugombea urais mwaka huu, atakufa ghafla, Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Glory of Christ Ubungo ametoa masharti matatu kwa mtabiri huyo vinginevyo naye atakufa ghafla.
Katika mahubiri kanisani hapo jana, Mchungaji Kiongozi, Gwajima alisema demokrasia ya Tanzania imo hatarini endapo mtu mmoja ataachiwa kuamua hatma ya taifa kinyume na mapenzi ya Mungu asiyekuwa na upendeleo kwa mtu yeyote.

"Baada ya kuendelea kutenda kazi zake zikiwa ni chukizo machoni mwa Mungu, leo ninatoa hukumu kutoka kwa Bwana, nanyi nyote mtachuja kuwa ni upi utabiri wa kweli kati ya Sheikh Yahaya na Mungu.

Ninamwagiza Sheikh Yahaya afanye mambo matatu la sivyo naye atakufa ghafla kama alivyowatishia Watanzania wenzake," alisema.
Sharti la kwanza alisema ni Sheikh Yahaya kwenda katika kanisa hilo la Glory of Christ na kuonana na mchungaji Gwajima yeye mwenyewe ili amwongoze kwa sala ya toba, kisha ampokee Yesu katika maisha yake.

Sharti la pili, Sheikh Yahaya ameamriwa kuanzia sasa aachane na utabiri wake ambao kwa miaka mingi alisema umewaumiza watu wengine wasiokuwa na hatia na kuwafaidisha wengine wachache kwa njia za giza.

Na sharti la tatu, Sheikh Yahaya ametakiwa, baada ya kuokoka, arudi katika vyombo vya habari kwa nguvu ileile aliyoitumia kutangaza utabiri wake wa mtu kufa ghafla na sasa awatangazie Watanzania mabaya yake yote aliyokwishayafanya kwa watu wa taifa hili hadi siku ya mwisho alipolazimika kuokoka.

Akifafanua juu ya masharti hayo, Mchungaji Gwajima alisema kimsingi yeye anamkubali Rais Jakaya Kikwete kuwa kiongozi wa taifa hili ila kinachomkera ni Sheikh Yahaya kuwatisha watu wengine wasitumie haki yao ya msingi katika kuikuza demokrasia hapa nchini.

Alipohojiwa kwa njia ya simu, Sheikh Yahaya ambaye alisema yuko nje ya jiji la Dar es Salaam kwa siku ya jana, alisema katika kipindi cha miaka 40 ya utabiri wake umekuwa sahihi siku zote na umaarufu wake ni wa kimataifa.

"Kamwe sitakwenda katika kanisa hilo, pia siko tayari kufuata sharti hata moja kutoka kwa mchungaji huyo.
Nimeanza utabiri kabla ya yeye kuwa shemasi wa kanisa hivyo endapo nitakufa najua ni siku zangu zimefikia mwisho wala si vinginevyo," Sheikh Yahaya alisema.

Akitoa mifano ya utabiri wake ambao aliosisitiza kuwa sahihi mara zote, alitabiri msiba wa Mzee Rashidi Mfaume Kawawa kwa maelezo kwamba taifa litapata msiba mkubwa. Pia alisema aliwahi kutabiri kifo cha kiongozi mashuhuri ambaye kifo chake kingewakutanisha watu wa mataifa mbalimbali, dini, rangi na vyama mbalimbali vya siasa na kwamba kiongozi huyo alikuwa hayati Mwalimu Nyerere.
"Je, sikutabiri kuwa ndani ya CCM utazuka mtafaruku na kusababisha ufa ndani ya chama hicho kitu ambacho ninyi waandishi mmekishuhudia hivi karibuni?
Mimi siwezi kuongea kashfa yoyote dhidi ya mchungaji huyo bali ninachosema akipenda apeleke malalamiko yake Ikulu, kwani nako huko wapo watu wa kumjibu waliozishuhudia kazi zangu kwa miaka yote," alitamba Sheikh Yahaya.
Alisema alitarajia kiongozi huyo wa kanisa aempe mwaliko rasmi waonane mahali popote siyo hapo kanisani ili waelezane masula ya nyota kwa undani badala ya ‘kumtisha'.

CHANZO: NIPASHE
 
Hata kama itakuwa ni utani,kwetu wanaamini kwamba ukiona watu wanasemasema kwamba fulani kafa wakati yuko hoi ujue siku yoyote anakaa kimya. Lisemwalo lipo na kama halipo laja.

Sio ajabu Yahaya kuokoka,wapo kibao kama yeye na waliomzidi waliookoka ili kuthibitisha fuatilia historia ya Mtume Paulo wa kwenye Bilia. Aliokoka akiwa njiani kuwapeleka wakristo kuchinjwa sababu ya imani yao.

Unamkumbuka Ibrahim Yohana wa miaka ya1980 hapa DSM aliyeokoka Dodoma akiwa safarini kutoka Mwanza kwenda DSM akiugua kansa lakini dereva wa locomotives? Wapo wengi wengi wengi wanaokoka, inadhhirisha Mungu ni Kiboko yao! Yahaya sio mpinga Kristo, ni mtabiri tu na mtaalam wa Kurhan. Mbona hamkushangaa Sheikh Mwaipopo aliposilimu akiwa mchungaji?

Mungu peke yake ndiye ajuaye nani ni mtumishi wake, anamgeuza mtu kutegemeana na shughuli anayotaka kumpa mtu huyo. Jina la Bwana libarikiwe.

Leka
 
Mi naamini c kwasababu eti kwa Mungu hamna lisilowezekana. Ila kwa sababu wasanii wawili wameamua kuunganisha nguvu zao hapo ntakubali.
 
Cha msingi aombe Mungu ampe kujua mapenzi yake na siyo kuja na hoja za kutisha watu kwa kutumia nyota
 
Niliyoifahamu mie ni ya kuokoka kwa yule Sheikh Mtoto maarufu kama Sheikh Shariff ambaye aliitingisha inji hii kwa ufahamu mkubwa wa Qur’an akiwa na umri wa miaka tisa na akabatizwa kwa jina jipya la Michael Sylivester Sewando. Ilikuwa reported kwenye Msema Kweli, Sept las yr.

USIWE UNATU "CONFUSE" HAPA NA HII ILIYOWAHI KURIPOTIWA 3 WKs AGo:
Je hii habari ya shehe Sharif kumrejea Mungu wa kweli zina ukweli ndani yake ? nazisikia kama udaaku mitaani, kwani anaishi wapi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom