Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,790
Katika kunogesha maudhui ya kipindi cha "Amani na viashiria vya kuvunja Amani' ndani ya (Morning Trumpet)cha leo asubuhi kinachorushwa na Azam TV, Al-Hajj Sheikh Mussa pamoja na udhaifu aliouonesha wa kukosa hekima na busara kwa kuwa alilalia upande ya ukereketwa zaidi katika majibu yake ukilinganisha na wajumbe (mapdre) wengine, alimfananisha JPM kuwa sawa na Khalifa wa pili katika uislam baada ya Mtume Muhammad (SAW) Omar bin Al Khattab (634-644).
Omar bin Khattab alisifiwa sana kwa ujasiri, ukali, busara na usujaa wake vitani. Katika Encyclopedia Britannica imemuelezea Omar kuwa -" A strong ruler, stern toward offenders, and himself ascetic to the point of harshness, he was universally respected for his justice and authority"
Hata hivyo Omar aliuwawa msikitini na Mtumwa wa kipersia, Piruz Nahavandi (au Abu Lulu), kwa kisu na muuaji nae kujiua baada ya kuwaua watu wengine tisa wakati akijaribu kutoroka.