Rais Magufuli akutana na Balozi wa Qatar Nchini na Spika Mstaafu mhe Anne Makinda Ikulu Dar

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiagana na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe Abdallah Jassim Al Maadadi baada ya kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 16, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge Mstaafu na mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Mama Anne Makinda Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni. PICHA NA IKULU.

Tanzania inatarajia kufungua Ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema hayo leo tarehe 16 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi.

Pamoja na kutangaza kuufungua Ubalozi wake nchini Qatar Dkt. Magufuli amemuomba Balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinayoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo Trilioni 57 na mpango wa kufufua shirika la ndege la taifa (ATCL).

"Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili" Amesema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Abdallah Jassim Al Maadadi amemshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na amemuahidi kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar na Jumuiya ya wafanyabiashara wa nchi hiyo ili waje kuwekeza Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Makinda amesema mazungumzo yao yameuhusu Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuhakikisha mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
16 Juni, 2016.
 
Safi sana jpm wakongwe wanamchango mkubwa watumie kuimarisha mambo kadha wa kadha katika serikali yako.
 
Japo litakalofuata ni kuteua barozi makini kuimarisha hayo mahusiano yetu na taifa hilo mhimu hapa Duniani.
 
Nadhani pia kwa siri wameongea kuhusu sakata la NS , Ukawa na maoni ya Bi Kiroboto Sr
 
Balozi-Qatar.jpg

TANZANIA inatarajia kufungua ubalozi wake nchini Qatar kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo huku ikitilia mkazo katika sekta za gesi asilia, utalii, usafiri wa anga na mawasiliano.

Rais, Dk John Magufuli alisema hayo jana Ikulu, Dar es Salaam alipokutana na kuzungumza na Balozi wa Qatar nchini, Abdallah Jassim Al Maadadi. Pamoja na kutangaza kuufungua ubalozi wake nchini Qatar, Magufuli amemuomba balozi huyo kufikisha ujumbe kwa Kiongozi wa Qatar, Shehe Tamim bin Hamad Al Thani na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar kwamba zipo fursa nyingi za ushirikiano zinazoweza kufanyiwa kazi, huku akibainisha uwepo wa gesi asilia zaidi ya futi za ujazo trilioni 57 na mpango wa kufufua Kampuni ya Ndege ya Taifa (ATCL).

“Najua Qatar ina uzoefu katika maeneo hayo na sisi Tanzania tungependa tushirikiane nanyi kuwekeza na kubadilishana uzoefu ili fursa hizo zilete manufaa kwa pande zote mbili,” alisema Rais Magufuli.

Naye Balozi Al Maadadi alimshukuru Rais Magufuli kwa nia yake ya kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano na nchi hiyo, na ameahidi kufikisha ujumbe kwa kiongozi wa Qatar na jumuiya ya wafanyabiashara Qatar waje kuwekeza Tanzania.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, Ikulu, Dar es Salaam.

Baada ya mazungumzo hayo, Makinda alisema mazungumzo yao yameihusu NHIF na kwamba amemhakikishia kuwa amejipanga kuona mfuko huo uliobeba matumaini ya huduma za matibabu ya Watanzania unaboreshwa zaidi na dosari zinazolalamikiwa na wanachama zinafanyiwa kazi.

Back
Top Bottom