Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,893
- 16,317
UISLAM SIO UGAIDI NA WAISLAM SIO MAGAIDI: Sheikh Najih Shaker Al-Baldawi ni shujaa wa Iraq aliyemkumbatia "Suicide Bomber" kisha kuokoa maisha ya wenzake.
UTANGULIZI: Kwa msio nifahamu mimi Infantry Soldier ni mkristo ila ninafahamu fika ya kuwa uislamu si ugaidi na wala waislamu si magaidi bali wahalifu wachache hujificha katika kivuli cha uislamu ili kutenda ugaidi na kuua watu.
Uislamu ni dini safi tena ya watu waungwana sana inayohubiri amani na upendo kama ilivyo dini ya kikristo.
BACK TO THE STORY: Mnamo tarehe 07 mwezi wa July mwaka 2016, takribani watu 56 waliuawa na wengine 75 kujeruhiwa baada ya kundi la magaidi kuvamia jengo la makumbusho ya Sayid Mohammed bin Ali al-Hadi, sehemu takatifu ya waislamu wa dhehebu la shiha huko mjini Balad katika nchi ya iraq.
Waliwashambulia mahujaji wa kishiha waliokuwa wakisherehekea sikukuu ya Eid al-Fitr, ambao inatamatisha mwisho wa mwezi mtukufu kwa waislam wa Ramadan. Kulikuwa na washambuliaji watatu (3) wa kujitoa mhanga (Suicide Bomber) na mmoja wao waliuawa na mlinzi wa makumbusho hayo.
Kulikuwa na washambuliaji wengine pia ingawa ISIL walivurumisha mashambulizi ya mortar. (Wanajeshi mtakuwa mnazifahamu vizuri sana hizi mortar)
Mtu aliyeuawa baada ya kumzuia muuaji wa kujitoa mhanga asiingie katika eneo hilo takatifu alijulikana kwa jina la Najih Shaker Al-Baldawi. Alimkumbatia moja ya wauwaji wa kujitoa mhanga na hivyo kupunguza nguvu ya mlipuko wa bomu katika suicide vest.
Al Baldawi, mkazi wa kawaida kabisa na mwenyeji wa mji wa Balad alifanikiwa kuokoa maisha ya makumi ya idadi ya watu wasiokuwa na hatia na hatimae kuitwa shujaa baada ya kupata umaarufu mkubwa huko mashariki ya kati.
Source: Nenda website ya Google kisha search neno "Najih Shaker Al-Baldawi"
Usipite bila kusema Allahu Akbar