Mzito Kabwela
Platinum Member
- Nov 28, 2009
- 18,908
- 7,751
Maoni Mujaarabkwa mwendohuu wa msomi wa physics, chemistry, biology, mahesabu, nk kuongozwa na huyu ni sawa na kipofu kumuongoza anayeona.
na huko mbeleni ni wazi uislamu tanzania utapungukiwa na wafuasi sababu ya kuongozwa na watu wasio na maono....
maoni ya kigalatia !
NENDENI SHULE siyo MADRASSA MAANA WAKRISTO NA WAISLAM wenzenu WANAAJIRIWA KWA VYETI VYAO SI DINI YAO
Mtu anaajiriwa kwa sababu ya CHETI chake na Uzoefu wake si Dini yake.
Anayefikiria ataajiriwa kwa sababu ya dini yake, katika Kazi arudi shule akachukue Cheti.... La sivyo MTABAKI MASKINI MPAKA KUFA...
juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO...
Kwahiyo kumbe kuna umuhimu wa kujua idadi ya waumini?Kweli lakini, mbona wakatoliki tunajijua tuko wangapi? kwa sababu kuna jumuia ndogondogo za wakatoliki na kwenye kila jumuia tunajua wako wangapi ambao hesabu hupelekwa kwenye vigango mpaka parokia na baadae taifa halafu vatican sasa hawa wala ubwabwa nao si wajihesabu kwenye vibanda vya kahawa na bao wako wangapi wapeleke idadi yao msikitini?
Maelezo yako yamejaa chuki mpaka unashindwa kufikiri vizuri na ukaishia kujikanganya. Unasema Waislam hawakusoma na wanaishia kunywa kahawa vijiweni lakini ukakiri kuwa Rais wa Nchi na Makamu wake ni waislamu, je una maana hao hawakuenda shule? Ni product ya vijiwe vya kahawa? Au hujui kuwa Dr Gharib Bilal ni Engineer wa Nuclear Energy pekee hapa nchini ( one of the most cumbersome Mathematical subject in existence) ila serkali inashindwa kumtumia kutokana na mfumo mbovu uliopo. Au una maana Judge Chande hana elimu? Kina Proffesor Lipumba na Maprofessa na Ma Drs wote wa Kiislamu waliotapakaa nchi nzima hawakusoma bali ni watu wa Madrassa na Vijiwe vya kahawa? Unasema Waislamu wanajilipua ovyo duniani, hivi ina maana wewe hukusoma na wala hujui historia ya watu wanaojilipua duniani au ni chuki zako dhidi ya Uislamu ndio zimekutia upofu? Tulia nikupe darasa, Wenye Historia kubwa ya kujilipua duniani ni Wajapani, wanajilipua kwa staili ya KAMIKAZE (Kamikaze Bombers) wanajilipua ili kuua watu wengi zaidi na kuteketeza mali au zana kubwa zaidi, hao wako kwenye orodha ya mashujaa wa nchi hiyo mpaka leo, na Japan ikivamiwa tena kivita mtawasikia tena, Kisha kuna HARAKIRI, hawa hujipasua matumbo hadi kufa kwa kutumia Upanga wa Samurai, ikiwa ni kuonesha kutubu kwa kushindwa majukumu au anaposhindwa kujiokoa kwa maadui. Je hao ni Waislamu? Hapa Tz kuna Waislamu wangapi waliojilipua kwa njia hiyo? Hivi wewe na akili zako, na wenzako wenye fikra Kama zako mnaona vijiwe vya kahawa ndio tatizo, ila Mabaa ya Pombe na wanaokunywa pombe mpaka wakajinyea hao ndio barabara? Mbona Mwl Nyerere alipenda sana kucheza bao na wazee wenzake kwenye hivyo vijiwe vya Kahawa? Alikuwa mpumbavu?Hakuna cha maana katika maelezo hapo juu. Maendeleo ya Nchi hayapangwi kwa kufuata itikadi za Kidini au Kikabila. Tatizo lenu kubwa ni uelewa mdogo mlionao na hii inatokana na kutokwenda shule; mmekalia madrasa na kunywa kahawa vijiweni.
Kama mnataka kujua Waislam mpo wangapi Tanzania jihesabuni misikitini mwenu. Kwani hamjui mna Misikiti
mingapi? Tafuteni idadi ya Waislam kila Msikiti kisha mzidishe kwa idadi ya Misikiti yote iliyopo Tanzania.
Hatuwezi kuiga kila kinachofanywa na Nchi zingine Dunian. Sasa Duniani kote Waislam wanaandamana na kujilipua ovyo. Je hilo mnalitaka na nyinyi mlifanye? Mbona mankuwa watu msiofikiria mambo vizuri
Rais wetu, Makamu wa Rais Mkuu wa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Wakurugenzi wengi ni Waislam. Hilo wewe hulioni? Umetaja NECTA, TRA mbona hujasema NSSF?
NSSF kuanzia Mkurugenzi Mkuu hadi Mfuta Meza ni
Mwislam nakushauri ufanye utafiti kwanza kabla ya kusema. Udhaifu wa NSSF umetokana na mambo yenu ya Udini. Mtu hapewi kazi kwa vigezo vya elimu ila kwa vigezo vya UDINI (Uislam). Hadi kwenye interview unaulizwa wewe ni dini gani. Achani kuwa walalamishi kila mara. Sensa haiwezi kutofanyika eti kwasababu yenu watu msioenda shule.
CIA Inadai mgawanyo wa dini Tanzania upo kama ifuatavyo
mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/tz.html
Tumuamini nani ?
Kwahiyo Wapagani ni WENGI? Unachekesha kweli..
Kwahiyo Wapagani ni WENGI? Unachekesha kweli..
Akutunae hakuchagulii tusi.
Upuuzi wote huu unalelewa na mheshimewa rais kikwete. Ukihofu sana kutekeleza majukum yake, is where everyone will come up with idears good and stupidy, it is the president and his ministers to act and protect the nation. You can not leave crazy people to mislead moral citizens.
Hakika nawaabien hizi zote ni chokochoko na ni kiinimacho THE OBJECTIVE BEHIND IS TO IMPLICATE AND ESTABLISHMENT OF SHARIA LAW and THE RULE OF MAHAKAMA YA KADHI.
kumbe wewe ulizaliwa baada kufa Nyerere !!!
Hili ni gazeti la 1993 soma historia hiyo
MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.
Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.
Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:
Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.
Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.
Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.
Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.
Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge;
wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili.
Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu.
Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka).
Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.
Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:
Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.
Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.
Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.
Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.
Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!
Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.
Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC".
Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
Juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO.
Alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo.
Akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! Kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania.
"SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.
HOJA YANGU Ndugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? Kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!
Naomba kuwasilisha!
Alonena ni suala zuri sana. vipengele muhimu va kuzingatiwa katika sensa ni pamoja na Umri, Dini, jinsia, hali za watu (ulemavu n.k) kwa ajili ya mipango ya nchi kwa maendeleo na ustawi wa jamii.
Ni vizuri kulijadili kwa kina kwa mustakabali bora wa nchi yenu katika mipango ya baadae.