Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 844
- 1,608
Sheikh Issa Ponda ambaye ni miongoni mwa Waislamu 12 waliofungua kesi dhidi ya Serikali (RITA, Msajili wa Jumuiya za Kijamii kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali) na BAKWATA leo Machi 12, 2026 amewavaa vikali BAKWATA juu ya matrilioni ya fedha wanayoyapata lakini wameshindwa kuendesha miradi mbali mbali ikiwemo shule za Kiislamu na miradi mingine, "wameshindwa kuendesha shule maaana shule ni mradi na ni huduma, ... mapato yenu yako wapi yale matrilioni mliyokuwa mnayapata?"