Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sokomoko, Oct 17, 2012.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Asalam alaikum,

  Habari za masiku ndugu zanguni.

  Naanza kwa jina la Mwenyezimungu muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake! mwenye kujua ya dhahiri na ya siri (yaliyo mioyoni mwetu) na rehma zimfikie kipenzi chetu Muhammad SAW.

  Je Ponda ni nani?

  Mimi awali nilikuwa najua Ponda na Kundecha kuwa ni wanaharakati wenye kupigania haki za waislamu lakini imeniuma sana kujua undani wa hawa watu! Mimi ni mwislamu na siku zote nilikuwa naona jamaa wanafanya kazi kwa maslahi ya umma wa kiislamu lakini kumbe kuna mambo nyuma ya pazia.

  Manji Vs Ponda & Co

  Kuna uwanja ambao ulikuwa mali ya East African Muslim Welfare Society na kurithishwa kwa bakwata sehemu ya eneo lile ambalo lipo maeneo ya chang'ombe bakwatwa ililiuza/gawa kwa jumuia ya shia ismailia ambao na wao walikuwa wana hisa kwenye East African Muslim Welfare Society na Ismailia wakamuuzia Manji.

  Mkiangalia hapo juu hakuna mgogoro wowote wa kati ya Manji na Waislamu ila kina Ponda inavyoonyesha walikodiwa ili kuweka mazingira ya kumfrastrate manji apauze kwa bei poa.

  Leo tumuulize Ponda alilipwa kiasi gani kuhakikisha Manji hapamiliki pale? na kwanini walinyamaza baada ya manji kukitema kiwanja kile? Kwa akili ndogo ya kuzaliwa utajua kuwa Ponda & Co walitumika kufanya umafia ili kiwanja kipatikane kirahisi.

  Kukamatwa kwa Ponda.

  Kuna eneo ambalo limebakia kwenye kiwanja cha East African Muslim Welfare Society ambacho kinasemekana kuuzwa miaka minne au mitano iliyopita Ponda na group lake walivamia siku ya Ijumaa na kujenga msikiti wa muda na kuweka mabaunsa na baadhi ya waumini kwa madai kuwa kiwanja ni cha waislamu! yale yale yaliyomkuta Manji! na habari za chini ya kapeti ni kuwa Ponda na watu wake wamelipwa 15 Mil kumobilize uvamizi ule!

  Huyu jamaa anatumiwa kwa kuwa anaushawishi kwenye jamii yetu ya waislam lakini leo hii kama Mungu atadhihirisha kuwa anayoyafanya hayafanyi kwa ajili ya waislamu ila kwa maslahi ya mabwana zake basi nadhani shingo yake itakuwa halali ya Waislamu. Kwani wale waliokamatwa jana usiku pale Chang'ombe wengi wao hakupata mgao wa tajiri anaepataka pale zaidi ya chai ya asubuhi chakula cha mchana na maji ya chupa!

  Najua kuna wanahabari humu jamvini mkimuhoji jaribuni kumhoji issue ya manji iliishaje? je walilipwa nini baada ya kufanikisha zoezi lile?


  Narudia waislamu ifike muda tuchukue muda wa kufikiria tusikubali kuburuzwa na viongozi wanaoangalia matumbo yao na kusababisha matatizo kwa waislamu wasiojua set up ya matukio husika.

  Ahsanteni sana na ni matumaini yangu mmepata kitu juu ya mada hii.


  Ikiwa Mufti alisema uuzwaji wa kiwanja namba 311 kwa kampuni ya Quality Group hautambiliki na Bakwata nadhani Ponda kama ana nia njema na waislamu basi angesaidia Bakwata kuweza kurejesha eneo hilo ambalo linakadiriwa kuwa na ukubwa wa hekari zaidi ya 6 ili kuweza kujenga chuo kikuu cha kiislamu. Lakini ikiwa Ponda anataka eneo la heka 3 ambalo limeuzwa kihalali kwa mujibu wa Mufti kwa kampuni ya Agritanza.

  Kuna gazeti lilimnukuu mnunuzi/mmiliki wa eneo lililovamiwa na Ponda na wenzake akisema Ponda alitoa wazo wa kumrudishia pesa walizolipa Bakwata na kuifanya iwe siri bila Bakwata kujua. Mmmiliki huyo alipouliza je heka zake 40 alizotoa kwa bakwata kama sehemu ya "deal" ile watamrudishia? Inasemekana Ponda hakuwa na jibu.

  Inavyoonekana Ponda anatumiwa na "wakubwa" wanaomezea mate eneo hilo. Na kama hali ipo hivyo basi Ponda anawajibika moja kwa moja mbele ya Mungu kuwa anasababisha madhila kwa waislamu wanaomtetea wakijua kuwa anafanya kwa ajili ya dini ilihali anafanya kwa maslahi yake mwenyewe. Inasikitisha sana kuona kuwa Mungu amempa kipaji cha kuwashawishi waislamu lakini anakitumia kwa maslahi yake binafsi na sio kwa ajili ya kuwaendeleza waislamu kielimu na kiuchumi.

  Nawakilisha.
   
 2. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  KAZI ILIOKUWA IFANYWE NA BAKWATA inafanywa na taasisi nyengine. sHEIKH PONDA KAZA BUTI WAISLAM TUPO NYUMA YENU
   
 3. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  The Return of Sokomoko :nerd::nerd::nerd::nerd::nerd:

  Sasa tunaanza mambo ya UDINI
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono japo naendelea na utafiti wangu kuhusu huyu mrundi,hiyo avatar yako inaonyesha unatekeka kirahisi na wageni,wale vilaza kutoka mombasa naona wameshakula kichwa kwako.
   
 5. LoyalTzCitizen

  LoyalTzCitizen JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 1,806
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Hivi uislamu inaruhusu kujenga misikiti ktk ardhi ya dulma!? hivi hata huyo Mungu unayemuomba atakusikiliza kweli??? dahh! jamani sasa naona kila kukicha watu wanazua mitazamo yao ktk kubadirisha makusudio ya dini zetu.
   
 6. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Sheikh ponda yuko kituo cha polisi kipi?? Ili wadau tumpelekee ubwabwa nyama.
   
 7. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 180
  Ponda ni wa kupuuzwa, nashukuru umeliona hilo mkuu. huyu jamaa ni tatizo. Msisahau huyo ndiye aliyekuwa anahamasisha Muslims wasishiriki sensa ya watu na makazi 2012. Huku akijua ni kosa kutokuhesabiwa, yeye na familia yake wakahesabiwa wenzake aliowadanganya wakalala selo. Huyu jamaa tatizo
   
 8. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sijui dhulma gani unaongea. nadhani ukisema ujue unachosema. kile kiwanja cha waislam lkn BAKWATA Wakaamua kukipora na kama kawaida yao eti kuwakomoa waislam. lkn kwa bahati hakujua mnunuzi kwamba kauziwa Hewa. na msikiti ule utajulikana kama Masjid Sheikh Suleiaman takadiri. Mufti wa kwnza tz
   
 9. Malaria Sugu

  Malaria Sugu JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 2,653
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lkn waislam wengi wasomi wanamkubali kwa kuwafumbua macho watz maambo yanayoendelea hapa tz. pengine namfananisha na dk slaa.
   
 10. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  mimi nitajitolea ndizi, ghahawa, tende, harua na kashata
   
 11. m

  mikogo Senior Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 175
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  No comment
   
 12. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #12
  Oct 17, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,874
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  kwani bakwata wao ni wakristo?
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Oct 17, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Yuko nyumba za wageni anakula kitimoto kwa konyagi muda huu asipate kitambi
   
 14. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #14
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,410
  Trophy Points: 280
  Oysterbay
   
 15. mkada

  mkada JF-Expert Member

  #15
  Oct 17, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 999
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Ponda ni adui wa uislam na ukristo pia.He is the enemy of my religion and yours, tuungane pamoja tumshinde huyu shwetani.
   
 16. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #16
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mkuu elewa kuna tajiri anataka lile eneo kina ponda wametumiwa na zimetoka 15 mil ku mobilize kwa kuwa wanaushawishi mkubwa watu kama wewe ndio wale mnaokamatwa mkafunguliwa kesi halafu mkakosa wadhamini maana hata hujui what is behind the scene!

  Ni hivi kina Ponda walitakiwa wadeal na viongozi wa bakwata na sio alienunua ili bakwata arjeshe pesa kwa mununuzi na ardhi irudi bakwata. Hayo ndio waliyoambiwa na mnunuzi lakini kina Ponda hawataki wanataka pesa irudishwe na waliowatuma ardhi iende kwa aliewatuma.

  Kwa kifupi kina Ponda wanalipwa kwa ile kazi wewe kalaga bhaho eti utajengwa msikiti utaitwa jina la mufti wa kwanza. Mambo yataenda kimya kimya kama ilivyokuwa kwa manji watu watakula mshiko hakuta jengwa msikiti wala madrasa!
   
 17. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #17
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Wasomi hao wamuulize ile vita kuhusu uwanja uliouzwa kwa manji ambao ni sehemu tu ya sehemu hiyo hiyo wanayoidai leo waliimalizaje? je walitumiwa na anaemiliki sasa na wakanyamazishwa kwa pesa? je wameikodisha na wanalipwa rent? au walilipwa kiasi gani kwa shughuli ile? maana inasemekana hii kazi mpya wameshapokea 15 Mil kwa mtu anaepataka pale.

  Fungua macho hakuna issue ya uislamu hapa kuna vigogo wanapigana vikumbo kuchukua ile ardhi kina Ponda wanatumiwa kufanikisha mission refer to Manji vs Waislam saga.
   
 18. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #18
  Oct 17, 2012
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135

  Nadhani wewe ndio hufahamu omba ujulishwe kiwanja kile kilitolewa na Nyerere kujengwe chuo kikuu cha kiislam wakati wa East African Muslim Welfare Society. Wakati huo Waislam walikuwa wanajumui moja tu! yaani madhehebu yote yalikuwa chini ya chombo kimoja nachi ni East African Muslim Welfare Society baada ya kuvunjwa ile ardhi ilihamishwa na kumilikiwa na chombo kipya nacho ni Bakwata wakati huo Ponda hajulikani hata! Baadae Bakwata ikakiwanya kiwanja kile kwa jumuia za kiislamu zilizokuwemo kwenye East African Muslim Welfare Society. Dhehebu la Ismailia lilipewa eneo waliloliuza kwa muumini wao Yusuf Manji kwa ridhaa yao wenyewe! Yusuf Manji hakulinunua eneo lile kutoka kwa Bakwata kina Ponda wanajua hili lakini wanawatumia watu wenye ubongo mdogo kama wewe kufanya fujo ili wao wafaidike!

  Kipande kingine waligaiwa Madhehebu ya Ibadhi, Ibadhi nao wakauza kwa muumini wao na kipande kingine walipewa Sunni wamejenga shule ya DYCCC, kipande kingine kuna Markaz kilichobakia kikawa cha bakwata ambacho wameuza na kupewa kiwanja kingine che ukubwa wa hekari 100! ili lile lengo la kujenga chuo cha kiislamu litekelezwe kule kwenye zile heka mia moja. Kina Ponda wanajua hilo lakini hawataki wanataka aliewatuma ndio amilikishwe pale na wao walipe ujira wao!
   
 19. Democracy999

  Democracy999 JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2012
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 947
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi Ponda ni mtu au nguruwe?
   
 20. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Asante mkuu kwa elimu hii kwetu sisi ambao tulikua hatujui kinachoendelea!
   
Loading...